Mambo yameiva bongo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mambo yameiva bongo

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Lutala, Sep 14, 2010.

 1. Lutala

  Lutala JF-Expert Member

  #1
  Sep 14, 2010
  Joined: Jun 17, 2010
  Messages: 845
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  Kada wa UDP auawa kinyama
  NA ANCETH NYAHORE
  14th September 2010
  B-pepe
  Chapa
  Maoni
  Kada wa Chama United Democratic (UDP), kinachoongozwa na John Cheyo, ameuawa kikatili na kichwa chake kutenganishwa na kiwiliwili.
  Hata hivyo, jeshi la polisi na uongozi wa UDP, wametofautiana kuhusu jina halisi la marehemu.
  Wakati polisi imemtaja marehemu huyo kwa jina la Magembe Nteni, UDP imesema jina lake halisi ni Rubedi Ntemi(35).
  UDP imelishutumu Jeshi la Polisi kwa kile kilichoelezwa kuwa ni kupuuzia taarifa zinazotolewa na chama hicho kuhusu kuwepo uchochezi wa kisiasa unaosababisha vitendo vya uhalifu dhidi ya wanasiasa.
  Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Shinyanga, Daud Siasi, marehemu alikuwa mkazi wa kitongoji cha Ng’omango-Mbungani, kijiji cha Mwamigagani kata ya Mwalushu wilayani Bariadi.
  Marehemu alikuwa Katibu Uenezi wa UDP katika kata ya Mwalushu wilayani humo.
  Alikutwa amekufa kwa kuchinjwa shingo na watu wasiojulikana na ambao walitoweka na kichwa chake.
  Siasi alisema tukio hilo lilitokea kati ya Septemba 6 na 7, mwaka huu, baada ya wananchi kukitambua kiwiliwili cha mwanasiasa huyo.
  Alidai uchunguzi wa awali ulionyesha kuwa mwanasiasa huyo alichinjwa kutokana na tuhuma za kuwa na uhusiano ya kimapenzi na mke wa rafiki yake, aliyemtaja kwa jina la Ngisa Mahila.
  Siasi alidai kuwa uchunguzi huo ulibaini kwamba mwanamke huyo, Nkwaya Doto, alikuwa na ujauzito wa Ntemi.
  Kwa mujibu wa Siasi, Mahila alimshauri Ntemi waende kutembea pamoja hadi maeneo yenye vichaka, mahali ambapo mwili wake uliokotwa ukiwa hauna kichwa.
  Kamanda huyo alidai kuwa Mahila ambaye hivi sasa anashikiliwa na polisi, alifanya njama hizo baada ya kugundua kuwa, mke wake (Doto), alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na Ntemi.
  Mbali na Mahila, polisi inamshikilia Mboje Makano, mkazi wa kijiji cha Mwamigagani kwa tuhuma hizo.
  Wakati polisi wakihaha kukitafuta kichwa cha Ntemi na kuchunguza tukio hilo, UDP imelilaumu jeshi hilo, kwa kupuuza tahadhari iliyowahi kutolewa na uongozi wa chama hicho.
  Katibu Mwenezi wa UDP, Isaac Cheyo, alisema tahadhali hiyo ni pamoja na hoja iliyotolewa bungeni na Mbunge wa Bariadi Mashariki aliyemaliza muda wake, John Cheyo.
  Alisema Cheyo aliwahi kuhadharisha kuhusu nyendo za baadhi ya viongozi wa siasa hasa katika Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilayani Bariadi, kwamba hazionyesha dalili nzuri.
  Hata hivyo, Siasi, amekanusha madai hayo na kusema hadi kufikia jana, alikuwa hajapata barua yeyote kutoka UDP kuhusu ushiriki wa wanasiasa kuchochea vurugu na uhalifu.
  Badala yake alikitaka chama hicho (UDP) kutambau kwamba makosa ya jinai kama vile mauaji, hayana kambi ama itikadi ya kisiasa.
  “Hayo mambo ya chama usiyapokee…achananeni nayo…sisi polisi tunapochunguza matukio ya mauaji hatuna chama na hadi sasa sijaiona barua yoyote hapa ya UDP,” alisema.
   
 2. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #2
  Sep 14, 2010
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,377
  Likes Received: 3,140
  Trophy Points: 280
  sio njama za ccm hizi?........nina wasiwasi ccm wameanza kuonesha sura yao ya upande wa pili kwa wagombea wa upinzani na naamini tutasikia vifo vingi na ccm kwa kuwa sheikh yahaya ni mchawi wao km mwenyewe anavyojipambanua naamini wataua hata mgombea urais ili kutimiza azma ya yahaya aliyesema watakufa.......watz tuamke tuwakatae akina yahaya kwenye jamii zetu/........
   
Loading...