Mambo ya Ngoswe...

Jidu

JF-Expert Member
Mar 9, 2011
1,232
754
[h=3]ASKARI ALIYEFANYA MAPENZI NA MTUHUMIWA WA KIKE KATIKA KITUO CHA POLISI AFUKUZWA KAZINI [/h]
Na Ezekiel Kamanga, Mbeya.
JESHI la polisi Mkoani Mbeya limefukuza kazi Askari wake Enock Daffa (22) kwa tuhuma za kufanya mapenzi na mtuhumiwa wa kike mwenye umri wa miaka 25 katika kituo cha polisi cha mji mdogo wa Tunduma Wilaya ya Momba Mkoani hapa.
Kwa mujibu wa kamanda wa polisi Mkoa wa Mbeya Athuman Diwani askari huyo alitenda kosa hilo Novemba 21,2012 na kwamba mtuhumiwa aliyefanya naye mapenzi alikuwa anakabiliwa na kosa la wizi.

Kamanda Athumani alisema kuwa mbali ya kufukuzwa kazi askari huyo tayari amefikishwa katika mahakama ya Wilaya ya Mbozi ili sheria iweze kuchukua mkondo wake.

Aidha alisema kuwa hali kama hiyo haitaweza kuvuliwa na jeshi la polisi na kwamba atakayebainika kufanya tukio kama hilo adhabu yake itakuwa ni kufukuzwa kazi.

Kamanda huyo alitopa wito kwa askari polisi kufanya kazi kwa kufuata sheria na kanuni za jeshi la polisi kama mwongozo unavyowaagiza ili kuinda maadili ya jeshi la polisi ambacho ndicho chombo kinachotumika na wananchi katika kuzisimamia sheria.

Akizungumzia tukio hilo baba mzazi wa askari huyo alisema kuwa kitendo alichofaya mtoto wake si cha kiungwana ambaco kimetia fedheha familia yake lakini pia kwa jeshi la plisi ambalo limepewa dhamana ya kutunza usalama wa raia na mali zake.
 
Back
Top Bottom