Mambo ya msingi kwa mke au mume

Mambo ya msingi kwa mke au mume

Mukwano jebaleko

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2015
Posts
402
Reaction score
214
Mambo haya yanaweza kuchangia ndoa yako kudumu kwa kwa muda mrefu

1:Upendo
Upendo ni neno dogo lakini limebeba uzito mkubwa sana...hivyo ni muhimu kumpenda mwezi wako kwa maneno na matendo

Angalizo:unapo mwambia mwenzi wako unampenda basi ni vema ukajitahidi pia kuonyesha unampenda kwa matendo(mtendee mema

2:Msamaha

Kwa watu mmpendanao kukoseana ni moja ya maisha yenu,ili mdumu katika umoja wenu hamna budi kusameheana kila mkoseanapo

Angalizo:utafiti unaonyesha wanaume wengi si wepesi wa kushuka (kuomba Msamaha) na hii ni kwasababu wanajihesabia haki..Mara nyingi hupenda kusema yaishe;swali yanaishije bila kusamehewa?omba kwanza Msamaha..

Msamaha ni tiba ya mahusiano kuwapo na tofauti

3:Tendo la ndoa

Hakikisheni mnafanya tendo la ndoa lenye tija kwa pande zote:

Ni rahisi mwanaume kufika kileleni kuliko mwanamke,hivyo mwanaume hakikisha unamfikisha mwenzio kunako takiwa afike

Angalizo:usipo muwezesha mwenzio kufika anakotakiwa kufika unamtengenezea mazingira ya kutafuta mbadala

4:Shukrani

Neno Asante nalo ni dogo lakini lina nguvu na umuhimu mkubwa sana;jifunze kushukuru kwa kila jambo jema utendewalo na mwenzi wako hata kama ni haki yako.

Asante humfanya akupae aone umethamini kile alichokupa

5:Uchumi

Ni muhimu kushirikiana katika kujenga Uchumi imara wa familia,Hii itawasaidia kuweza kukabiliana na changamoto mbalimbali zitakazo wakabili.

Angalizo:Epuka kuwa na mtu anaejua kutumia tu ila kutafuta hujui utateseka,na kunauwezekano ukiwa hauna mkaingia kwenye migogoro

6:Muda wa pamoja

Kuna umuhimu mkubwa wa kutenga muda wa kukaa pamoja na kujadiliana na kupanga mipango yenu

Si lazima mjadiliane nyumbani,mwaweza kuwa na outing
Hata mkalala huko Baada ya kumaliza mkarudi nyumbani

7:kuwa na mitoko(outing)

Mara nyingi wapenzi wanapo anza kuishi pamoja huwa wanakumbwa na tatizo la kuishi kimazoea,na hii imesababisha watu kufurahia maisha ya uchumba na si maisha ya ndoa

Kumbuka mkiwa Wachumba mlifanya outing ngapi?kama ulisha wahi kutoka na mkeo/mmeo basi ni vema ukampa hiyo nafasi kila upatapo nafasi na shekels

8:Siri

Jifunze kumtunzia Siri mwenzi wako,sio Vizuri kuyasema mapungufu yake kwa watu

Nb:hata ukikosewa usikimbilie kwa ndugu na hii ni kwasababu hata ikitokea nyie mmepatana ndugu wanaweza kuwa bado na chuki au kinyongo ya kile ulicjotendewa

9:Marafiki

Marafiki wamekua na faida na wakati mwingine wameleta hasara
,ni muhimu sana kuwa makini na Marafiki

Jamaa yangu alimuamini sana rafiki yake,Baada ya muda rafiki akaanza kumtongoza mke,je Unadhani nini kiliendelea

Marafiki wanaotafuta kuona unasonga mbele ni bora zaidi kuliko wanaotaka kuona hauendelei,tena ni heri kuwa na rafiki mmoja kuliko elfu wanao kusimanga

10:kusali pamoja

Naamini mtakua na imani yenu ambayo mnaamini mkimwomba Mungu atasikia,ni jambo la busara sana kumkabidhi Mungu mipango yenu

Hii itawasaidia na kujikinga na kila baya lipangwalo juu yenu

NAWASILISHA.
 
Ndoa yeyote ili idumu inahitaji wanandoa
1.kupendana
2.kuaminiana
3.kuheshimiana
4.kuvumiliana
Mambo mengine ni mbwembwe tu
 
Back
Top Bottom