Mambo ya mila yananinyima usingizi.... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mambo ya mila yananinyima usingizi....

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Nyadhiwa, Jul 24, 2010.

 1. Nyadhiwa

  Nyadhiwa JF-Expert Member

  #1
  Jul 24, 2010
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 266
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Nahitaji ushauri wenu wana JF, mimi nina rafiki ambaye tulifahamiana toka niko sekondari kama family friend. Tulipoteana kwa muda wa miaka 8 hivi kisha tukaaza kuwasiliana tena mwaka huu (family friendship) tukaaza kuwa na mawasilanao ya kimapenzi ingawa tuko mabara tofauti tukitafuta elimu. Tunapendana sana na ameamua kuniomba afanye taratibu za kuoana ili tukirudi tu Tanzania tuoane.

  Niliamua kuuliza nyumbani (Aunt yangu) kama tunaweza kuoana na huyo kijana nikajibiwa kuwa huyo kijana ndo awaulize wakubwa wa kwao. Tatizo ni kwamba inasemekana kwa mila zetu, haturuhusiwi kuoana watu tunaotokea eneo moja nami hizo mila sizijui, naye anasisitiza kuwa inawezekana, sasa ooooooh hata sijui nifanyeje hapa make sijampata mwingine ila yeye.

  Msaada tafadhali
   
 2. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #2
  Jul 24, 2010
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,646
  Likes Received: 1,472
  Trophy Points: 280
  pole, lakini sikiliza

  unavijua vikwazo vya ndoa yeyote ile....? kwa ufupi tu ni kwamba, kama huyo kijana sio kaka yako wa damu, sio binamu, sio mjombako, sio shemeji yako......basi we endelea na maandalizi ya harusi..in fact kwa mila zetu huwa tunachangia harusi so lete kadi hapa siye tuje tule mchele
   
 3. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #3
  Jul 24, 2010
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,113
  Likes Received: 3,035
  Trophy Points: 280
  pole sana...lakini kwani mkioana nini kitatokea?...hayo ni mambo ya kizamani kama mnapendana mimi sioni tatizo.....oaneni
   
 4. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #4
  Jul 24, 2010
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Kama inawezekana au haiwezekani kwa mujibu wa mila zenu, mimi ushauri wangu kwako ni zitupilie mbali hizo mila zisizo na kichwa wala miguu. Kama ninyi si ndugu wa damu na mmefikiana sioni ubaya wowote wa ninyi kutokufanya kile ambacho mioyo yenu inataka.

  Haya mamila ya Kiafrika bana aaaah....wewe watu wanaoana na mabinamu zao huko Mashariki ya kati sembuse ninyi mliotoka eneo moja?

  Fuata mila zilizo na maana. Za kipuuzi zipuuze.
   
 5. Nyadhiwa

  Nyadhiwa JF-Expert Member

  #5
  Jul 24, 2010
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 266
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Hakuna undugu hata kidogo mbali na kuwa baba yangu na kaka yake (marehemu kwa sasa) walikuwa ni marafiki sana
  hali iliyopelekea familia hizi mbili kufahamiana sana na kuwa kama ndugu.
  Hizi mila zimekuwa kikwazo sana hasa ukizingatia hatuzujui vema.
   
 6. Pretty

  Pretty JF-Expert Member

  #6
  Jul 24, 2010
  Joined: Mar 19, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 135
  ......Ehhhheee shosty weka mila pembeni wala sio ndugu huyo, kama unampenda na unamuhitaji chukua chako mapema. Mambo ya mila kama hizi yamepitwa na wakati.
   
 7. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #7
  Jul 24, 2010
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,601
  Likes Received: 82,165
  Trophy Points: 280
  Mila nyingine jamani ahhhhh! hazistahili kuendelea kudumishwa kabisa maana zimepitwa na wakati. Kila la heri katika maandalizi ya ndoa yenu. Wakati mwingine inabidi mngangamare ili kuzishinda mila ambazo zimepitwa na wakati.
   
 8. malisak

  malisak JF-Expert Member

  #8
  Jul 24, 2010
  Joined: Mar 16, 2006
  Messages: 425
  Likes Received: 302
  Trophy Points: 80

  achana na mila potofu hizo zimeshapitwa na wakati wewe angalia unachopenda(mapenzi) kwanza kama kijana umemridhia mkubalie kwani mnataka kutenda dhambi?,si mnataka kutafuta kheri oaneni na mungu atawalinda na hizo imani,labda kama hujaridhika mwenzoio nilitaka kujinyonga walipokataa niolewe na barafu wa moyo wangu mbona walinikubalia wenyewe.chezea.
   
 9. B

  Babuyao JF-Expert Member

  #9
  Jul 24, 2010
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 1,734
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Kwa kuwa mila yenyewe huijui sana (maelezo yake na sababu zake), jaribu jkuulizia kule nyumbani wakueleze sababu ya katazo hilo: yawezekana ni sababu nzuri na nzito kabisa, huwezi kujua. Wakishakueleza - ukiona ni sababu isiyo na uzito - unaweza pia kuwaelimisha wazazi na wana-ukoo juu ya kilicho cha kweli: kwamba kutoka sehemu moja si kizuizi cha ndoa kama si undugu wa damu. Wakikuelewa utakuwa umepata pasi ya kuingia ndoa bila bughudha au kuwatia simanzi wazazi wako. Huenda katazo hilo linasababishwa na kutaka kuzuia tabia fulani mbovu au ugonjwa fulani wa kurithi ambao eneo lenu upo. Kwa hiyo kwa kutaka kutomeza polepole tatizo hilo wazee wakaweka katazo hilo ili kuwafnya watu wa eneno lenu waende mbali kuoa na kuchanganya damu na watu wengine wasio na athari hizo mbaya za eneo lenu. Huu ni mfano tu.
   
 10. malisak

  malisak JF-Expert Member

  #10
  Jul 24, 2010
  Joined: Mar 16, 2006
  Messages: 425
  Likes Received: 302
  Trophy Points: 80
  Hakuna cha mila wala nini na ampe mwenzie kunyimana si vyema
   
 11. Nyadhiwa

  Nyadhiwa JF-Expert Member

  #11
  Jul 25, 2010
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 266
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Mtazamo wako ni mzuri...
  Sababu kuu niliyoambiwa ni kutoka sehemu moja tu hakuna lingine.
   
 12. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #12
  Jul 25, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Duh, binadamu kweli ni mgumu kumridhisha, mi nilidhani kwa familia kuwa na urafiki ni nafasi nzuri ya kuunganisha urafiki zaidi kwa kuozeshana..lakini kumbe I wasn't smart enough..lol
   
 13. Nyadhiwa

  Nyadhiwa JF-Expert Member

  #13
  Jul 25, 2010
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 266
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Asante NN
  Nitajitaidi ili niweze kukabiliana na hiyo hali kwa maana wamekuwa wakijaribu kunikatisha tamaa sana juu ya huyu kijana.
  MAra waseme kwanza kijana mwenyewe anamaringo, mara mweusi.... wakati mimi hayo hata siyaoni kwa huyu kijana.
  Wanataka tu kuumiza roho yangu make toka nimeambiwa hayo maisha yangu yamekuwa ni magumu sana.
   
 14. Lady N

  Lady N JF-Expert Member

  #14
  Jul 25, 2010
  Joined: Nov 1, 2009
  Messages: 1,919
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  acha na mila, pata kitu roho napenda veve!
   
 15. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #15
  Jul 25, 2010
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Sasa hii ya kuwa "mweusi" wanapitiliza. Imekaa kiubaguzi baguzi wa rangi.
   
 16. Da Womanizer

  Da Womanizer JF-Expert Member

  #16
  Jul 26, 2010
  Joined: May 24, 2010
  Messages: 1,561
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Ndo maana watu wana-bleach ngozi cku hzi. Yaani huwezi amini watu ujinga umewajaa vichwani unaweza kubaki mdomo wazi halafu sasa unakuta ni mtu ana madigirii kama 100 hvi.
   
 17. K

  Kanyafu Nkanwa JF-Expert Member

  #17
  Jul 26, 2010
  Joined: Jul 8, 2010
  Messages: 812
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Bleaching noma sana. Inapunguza mvuto ambao ulitegemewa. Kitu black bwana,,, kila kitu black, isipokuwa meno tu, ni mvuto wa hakika hasa. Lakini wako wanaopenda bleach, anyway.

  Na nyie mnaotaka kuoana, mngetiana mimba kwanza, ndo muibikie pale front. Alafu msikilizieni atayekuwa wa kwanza kusema hapana!
   
 18. Gwamahala

  Gwamahala JF-Expert Member

  #18
  Jul 27, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 3,577
  Likes Received: 924
  Trophy Points: 280
  Angalia hapo kwenye bold dada!
  Wewe umetuambia una miaka nane hujaonana naye afu hata kwa sasa mnakaa mabara tofauti,kuna uwezekano mkubwa kuwa hayo mapungufu wanayokuambia ndugu zako ni ya kweli.Be careful sometimes love can make you BLIND...
   
 19. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #19
  Jul 27, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Ukirudi tu hakikisha anakupa mimba kwanza . alafu mambo mengine yatajiset yaani hiyo mimba itwakuwa catalyst ya kuondoa vikwazo.
  Kwa nn wakuchagulie sausage ya kula? Kamata kitu roho inapenda bana

  Sehemu moja ina tatizo gani? Au ndo zile Mila Mfano
  Kwamba labda yeye ni Mjaruo wanahisi hajatahiriwa na wewe labda ni Mkurya ..........
   
 20. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #20
  Jul 27, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,183
  Trophy Points: 280
  Ukifuata mila sana utakuwa huoi/ huolewi.

  Mila nyingine hazitaki uoe karibu na kwenu, nyingine hazitaki uoe mbali na kwenu etc.

  Jambo la kujiuliza ni kwamba, mila hizi zina maana kwako au hazina? Anayeoa/ kuolewa ni wewe, usitake kufuata mila za watu ambao hawatalazimika kuishi na mume/mke wako wakati kwako wewe utakayeishi naye hazi make sense.

  Tunahitaji mila zenye maana, vile vile tunahitaji kuachana na mila zisizo na maana. Na anayetakiwa kuamua ni muoaji/ muolewa, si mwingine yeyote.
   
Loading...