Mambo ya kuzingatia mwili ukiwa na afya njema

Sengulo

New Member
Oct 15, 2020
2
45
Mambo kumi muhimu ya kuchunga kiwiliwili bado kinasiha kamili
Kushika Miko au kujichunga na vitu au mambo fulani wakati bado unaafya yako ni Bora kuliko kutumia dawa unapopata ugonjwa.
Mwenye akili kamili ni yule anayefikiria mambo kabla hayajafanyika ili kujichunga yasikupate. Utabibu umegawanyika sehemu mbili. Sehemu ya Kwanza ni kuhifadhi siha kabla bado hujashambuliwa na magonjwa. Sehemu ya pili ni kuidumisha siha ambayo imekupotea kwa kufanyakitu dawa.

Chunga mambo kumi
Yapasa ufahamu kwamba kuhifadhi siha ambayo unayo hivi sasa, lazima uchunge mambo kumi nayo ni
1. Kuchunga vyakula
2. Vinywaji
3. Harakati za kiwiliwili (i.e. exercise).
4. Mapumziko
5. Usingizi
6. Kuwa macho
7. Jimai
8. Matamanio

(Maongezi zaidi kuhusu chakula) “Maida (matumbo) ndio nyumba ya maradhi, na kushika Miko ndio dawa kubwa”.
Wenyekazi ngumu hawadhuriwi na vyakula vizito, lakini pia yataka ale kwa kiasi azidishe Mara tatu katika mchana na usiku.
Ukila Anza na maombi na ukimaliza mshukuru yeye. Jiepushe na Kula vyakula vibichi au ambavyo havikuivishwa sawasawa. Na Kula baada ya kula ya kabla ya chakula Cha mwanzo hakijafanyiwa kazi.

Matabibu wote wamekubaliana juu ya maMimimbo yanayosababisha maradhi
Wameafikiana kwamba mambo sita ndio sababu ya maradhi mengi Sana;
1. Kukithirisha jimai
2. Kunywa maji usiku mwingi
3. Kulala kidogo sana usiku
4. Kulala Sana mchana
5. Kula tena baada ya kuwa umekwisha kushiba.
6. Kuzuilia mkojo.

Mambo haya sita yamekubaliwa na matabibu kuwa wanazuoni was kirumi, kihindi na kifursi kuwa yanasababisha maradhi. Matokeo hupatikana kwa kufanyakitu mazoea, mfano kuzoea kuzuia mkojo na mengineo.

KUNYWA MAJI
Mtu yatakiwa anywe maji anaposhikwa na kiu. Ahakikishe kwamba maji ni safi, maji Bora yawe baridi, na atoe pumzi nje ya kikombe au glass anayotumia asitoe pumzi ndani ya chombo anachokunwea maji. Mfano Kama wanavyokunywa watoto wadogo Sana was miaka miwili au mitatu mpaka mitano, si vizuri kutia pumzi ndani ya kinywaji. Na anywe Mara tatu, asifululize kunywa kwa upumzi mmoja, na Kila akirudisha kunywa Anza kwa jina la mwenyezimungu na umshukuru ukimaliza kunywa.

Usinywe maji yaliyo Moto Ila kwa udhuru maalum usinywe maji yenyevumbi ambayo si safi, Wala maji yanayonuka uvundo, ni vibaya.
Na usinywe maji katika chombo ambacho hakioneshi maji ndani yake mfano Kama maji yaliyo katika kibuyu au chupa nyeusi, ni hatari huweza kuwa mna vidudu vya mbu au mna kitu kibaya kimekufa ndani yake. Ikiwa hapana budi kunywa maji ya kutoka chombo hicho, basi usinywe Kwanza yatie katika chombo kilicho wazi Kama glasi au kikombe nk. Ili upate kuyaona yalivyo, yawe safi na hayana harufu mbaya.

Kunywa maji asubuhi kabla hujala chakula au unapoamka kutoka usingizini usiku, huzima joto la matumbo. Usinywe maji baridi baada ya kula matunda au baada ya chakula Cha Moto au baada ya vyakula vyenye chumvi nyingi au vyakula vyenye kutia kiu na vilevile usinywe maji yenye baridi nyingi, Bora ikiwa huna budi yavute kidogo kidogo ili yashike joto la kunywa, lakini usikukumie.
kunywa maji kwa kuyavuta kidogo kidogo yaani kunywa maji kwa Mara moja husababisha kuumwa na ini.
Maji ya kunywa lazima yafunikwe hasa usiku yasilale wazi, maji yaliyolala wazi ni Bora yamwagwe.

MAPUMZIKO au kujituliza
Mta akiwa anapumzika ama atakuwa amekaa tu au amejinyosha au apumzike kwa namna yeyote nyengine. Lakini haitakiwi adumu katika Hali moja tu mpaka achoke. Isiwe mfano ni kitako tu a ni kujinyosha tu mpaka achoke, lazima ajibadilushie, huweza kuleta madhara katika kiwiliwili chake.

USINGIZI
Usingizi ni utulivu was viungo na haraka yaani viungo kuwa havikushughulika na chochote, mfano macho yamefumba hayaoni, masikio hayasikii na hivyo hivyo viungo vyote huwa vitulivu nk.

Usingizi unafaida mbili, moja wapo ni viungo kustarehe na kutulia kwa taabu ambazo kiwiliwili hupata kinapokuwa macho na raha ya nafsi (ubongo) kwa shida na taabu za fikra na hamu na mengineyo. Kwa hivyo ikiwa uko katika usingizi huwa na raha Sana.
Na faida ya pili ni kwamba harara (joto) jingi huingia katika kiwiliwili wakati was usingizi na hiyo harara hufanyisha msaada was kukipika chakula matumboni na anapoamka huwa chakula matumboni kimekwisha fanya kazi.

Na kiasi kizuri Cha usingizi ni muda was masaa sita ya usiku au masaa manane. Ama mchana hata muda was saa moja tu au kupunguza wakati wa kabla just kupinduka (midd day siesta) usingizi unaoitwa qaylulah usingizi huu was qaylulah husaidia Sana.
Watu wanaoamka usiku was manane kwa ajili ya kufanyakitu ibada ya mwenyezi mungu Kama vile kula daku husaidia saumu.

WAKATI MTU YUKO MACHO
Mtu muda ambao yuko macho, hakulala, wakati wake hafai kuupoteza bure “Mimi sipendi kumuona mtu amekaa ovyo Hana kazi yoyote hajishughulishi na kazi ya dining Wala ya kidunia” mtu akiwa usingizini ndio wakati ambao amepumzika, Hana shughuli yoyote ya kidini Wala ya kidunia, lakini akiamka yafaa ajishughulishe nanmambo ya kidini au ya kidunia, asikae ovyo, kukaa ovyo ni kuupoteza umri wako.


JIMAI
Jimai yataka pale ambapo mtu anahisi shauku na manii ya karibu. Kwa hivyo awapo katika Hali hiyo ya kuhisi ahitaji jimai na manii ya karibu, kwa hivyo itafaa ayatoe kwani wakati Kama huo kuyazuia manii kutoka kunaweza kusababisha madhara makubwa.
Wala jimai haikuwekewa wakati maalumu ila wakati wake ni pale unapohisi hamu na manii yako tayari, hata Kama ni mwaka mzima Mara moja ukiwa huna shauku.

Ama wengine wenye tabia ya damawii au balghamiy ikiwa wanaweza basi pia yataka wasizidi wiki moja Mara mbili au Mara tatu tu. Na I we siku mbalimbali. Haifai kufanyakitu Mara mbili kwa siku moja. Kwani Kisha itakuletea madhara makubwa, hasa zaidi kwa wale wenye kazi za taabu. Kazi ngumu sababu manii hutoka katika damu ile Safi iliyotoka katika chakula kizuri.

Mtu akiweza kufanyakitu jimai humaliza manii Kwanza kishahutoka kwa damu ya vyakula anavyokula na huenda ikawa ni sababu ya maangamivu. Na wenye kufanya Sana jimai humletea uzee upesi akakosa nguvu na hutokwa na nywele za mvi katika umri mdogo.
Na jimai ina namna nzuri na mbaya ambazo hazifai. Namna nzuri ni mwanamke alale chali na mwanaume awe juu yake. Na si nzuri namna yoyote isiyokuwa hiyo.

Na acheze cheze nae kwa muda kama kumkumbatia, kumbusu na kadhalika Kama hivyo ili kufanya awe na hamu pia ya kutaka jimai. Anapokuwa tayari ndipo inapofaa kufanya. Na unapotoa manii usitoe dhakari yako, subiri kwa mda na use umemkumbatia vizuri. Unapokuwa kiwiliwili chako kimetulia Tena hapo ndipo utoe dhakari yako. “Mtu akifanya jimai asioge mpaka (Kwanza) akojoe asipofanya hivyo hurudi ndani baki ya manii na humsababishia maradhi yasiokuwa na dawa na akimaliza jimai ajipumzishe”.

Imepokelewa kwa mtu mzee ambaye aliishi miaka Mia na hamsini na akawa kiwiliwili chake kizuri mwenye shahawa kubwa (matamanio makubwa) akaulizwa juu ya kuwa Ana umri mkubwa na shahawa yake bado in nguvu akasema “Mimi sikutangamanisha chakula juu ya chakula (hakula ila baada ya kuwa na njaa) na sikufanya jimai ila baada ya kuwa moyo wangu unahamu nayo na nikisha kufanya hupunguza harakati zangu baki ya siku ile yote".

Ukimtaka mkeo kwa jimai usimuingilie mwanzo wa usiku sababu maida huwa bado yamejaa chakula na si vizuri na huhofiwa kwa mwanaume kupata maradhi Kama ya kichwa kuuma upande mmoja, polio, vijiwe vya kibofu, kutokwa tokwa na mkojo, kudhoofika nuru ya macho na kudhoofika kwa ubongo.

Jimai ni nzuri mwisho wa usiku (saa zamanane). Jimai mwisho wa usiku ni Kama dawa ya kiwiliwili. Usimuingilie mwanamke mpaka ucheze cheze nae na umshike vilembwe vya matiti, umfyonze midomo yake ili ipate kuja manii yako au yake pamoja. Na anapokuwa tayari utamjua kwa uso wake au macho yake.

Na usimuingilie akiwa na hedhi Hadi atwaharike. Baada ya jimai matabibu wanasema haifai kunywa maji baridi, husababisha magonjwa, lakini ni vizuri kunywa maji ya tamu yaliyo baridi, au unywe maji yaliyochangamanishwa na asali.

VIUNGO vya KIWILIWILI KILICHO na AFYA KAMILI
Kiwiliwili Cha mwanadamu hakiendelei na Hali moja Kila siku, Bali hubadilika badilika, hutokelewa na mambo ya dharura. Kwa hiyo yataka mtu auzoweze mwili wake kwa tabia za kuweka katika Hali ya usafi. Aoge Kila siku, atie mafuta kichwani, mafuta ambayo ni mazuri kwa kiwiliwili ni mafuta ya simsim na mafuta ya zeti, apake na kiwiliwili pia na asubuhi aoge na achane nywele zake na kufanya hivyo ni Sunnah, na huondosha hamu na huzuni. Na siku za baridi aoge kwa maji ya Moto kiasi na siku za joto kwa maji baridi.
Mtu akiwa na dhiki za moyo na kutokwa na jasho jingi kwa kazi ngumu aliyoifanya aoge huondosha dhiki za moyo.

HEWA
Mwanadamu lazima ahitaji hewa ili upate kuishi. Bila hewa Safi mwanadamu hawezi kuishi atakufa. Hewa inamanufaa makubwa kwa roho na kiwiliwili. Hewa ikichanganyika na moshi au harufu mbovu yenye kunuka uvundo ni hatari kwa kiwiliwili vile vile hewa ikiwa na joto jingi au inabaridi Sana ni hatari kwa maisha.

Mambo yanayo husika na nafsi
Afya za moyo (nafsi) ni hamu na ghamu na raha ya nafsi na furaha. Mtu akiwa na hamu na Jambo muhimu sana na asiyapate huwa na ghamu, na pengine mtu huweza kufa. Na hamu na ghamu zikizidi katika nafsi ya mtu humkondesha. Mtu ajaribu asijitie hamu, aondoshe hamu na ghamu ila kwa Jambo ambalo si zito kulipata na akilipata asifurahi. Furaha ya kupita kiasi, kwani furaha nyingi nayo huweza kusababisha kifo.

Vile vile hasira nyingi pia ni mbaya Hasira hasara huweza kusababisha matokeo mabaya. Kwa hivyo yataka mtu azime ghadhabu (Hasira) zake kwa maji.
 

safuher

JF-Expert Member
Feb 11, 2019
10,151
2,000
Kila akirudisha kunywa Anza kwa jina la mwenyezimungu na umshukuru ukimaliza kunywa.
Hii imekaaje mkuu,kuna ushahidi wowote juu ya mafundisho ya mtume kuwa kila ukirudisha useme bismillah ama mwanzo wake tu ukisema inatosha ?
.

Kwa nijuavyo Bismillah ya kwanza tu inatosha haijalishi mafundo utakayopiga.

Kwa sababu tukienda hivyo maana yake hata ukisema bismillahi kabla ya kula kila tongi useme bismillah yani kama umepiga matonge 20 unatakiwa uwe umepiga bismillah 20 nazo.

Ikoje hiyo mzee ?
 

Sengulo

New Member
Oct 15, 2020
2
45
Hii imekaaje mkuu,kuna ushahidi wowote juu ya mafundisho ya mtume kuwa kila ukirudisha useme bismillah ama mwanzo wake tu ukisema inatosha ?
.

Kwa nijuavyo Bismillah ya kwanza tu inatosha haijalishi mafundo utakayopiga.

Kwa sababu tukienda hivyo maana yake hata ukisema bismillahi kabla ya kula kila tongi useme bismillah yani kama umepiga matonge 20 unatakiwa uwe umepiga bismillah 20 nazo.

Ikoje hiyo mzee ?
Hapana, Moja inatosha mkuu
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom