Mambo ya kuzingatia kulinda heshima yako

Villky_J

JF-Expert Member
Mar 14, 2017
492
609
Habari wana JamiiForums,

Leo nina kitu kidogo cha kuwashirikisha kutokana na utafiti wangu mdogo nilioufanya wa kutembelea ndugu, jamaa na marafiki ambao hatukuonana kwa muda kidogo. Nilichobaini ndugu zangu tujifunze kuficha siri zetu za kimaisha ikiwemo changamoto mbalimbali kwani si kila utakaemuelezea ukiamini ni ndugu na rafiki wa karibu anaweza kuwa msaada kwako lahasha bali yanayoweza kutokea ni kama yafuatayo-:

1. Wengi hupokea kama taarifa tu ya umbea, hivyo ni mwanzo wa kujua undani wa maisha yako na hupata nafasi ya kwenda kuwaeleza wengine. Kwani kwa kufanya hivyo ni sawa na kuanika matatizo yako mbele ya jamii nzima.

2. Hufurahia miyoyoni mwao, kwani binadamu tunapenda kumuona mtu akianguka zaidi kuliko kufanikiwa.

3. Ni mwanzo wa kupata maswali ya kebehi yatakayokufanya kuvunjika moyo zaidi kuliko ya ulivyokuwa awali. Hivyo basi wanakuwa ni chanzo wa kuongeza tatizo na sio kulitatua.

4. Utawapa ujasiri wa kukuuliza mambo mengi ya undani ambayo walitamani kukuuliza mwanzo wakashindwa, hivyo kuwafanya kujua vingi kukuhusu wewe, na ukishawaeleza huguna na kukucheka kimoyomoyo. Mpaka hapo jua heshima yako ipo mikononi mwao.

5. Utawafanya wakudharau kwani kile walichokuwa wanahisi unaweza kuwa nacho watakuwa wamepata uhakika kwamba huna, hivyo hata kukusema na kukunyanyasa ni rahisi kwani watajua huna lolote hivyo huna cha kuwafanya. Hivyo ni sawa na jeshi lililogunduliwa ni aina gani ya silaha za kivita linamiliki kwani ulinzi wake ni hafifu hivyo wakati wowote laweza vamiwa.

CHA KUZINGATIA:
1. Kama una wazazi mtu pekee anaeweza stiri aibu yako ni mzazi pekee kwani ukiaibika wewe ni sawa ameaibika yeye.

2. Ni vyema kumshirikisha Mungu, kwani yeye ndio muweza wa kila kitu chini ya jua.

3. Ni heri ukamfwata mtu yoyote mwenye busura na ambae hamfahamiani akakupa ushauri juu ya tatizo lako kwani huyo hawezi ona umuhimu wa kufanya yote hayo kwa kuwa hakujui.

4. Si kila jambo au tatizo, unahitaji msaada kutoka kwa mwingine mengine ni ya kupambana mwenyewe na kumuomba Mungu wako.

5. Kila unaemuona mbele ya macho yako ana matatizo kama yako au hata kuzidi yako lakini swali moja la kujiuliza kwanini yeye hakwambii ya kwake ni kwa sababu anatambua thamani yake.

****TUJIFUNZE HAYA DUNIA YA SASA***
SIO KAMA ILE YA ZAMA ZILE
 
Sio kila mtu wa karibu kuitwa rafiki, kwani kikulacho kinguoni mwako. Baadhi ya marafiki kama mbuzi ukilia beee(ukimhadithia) na yeye analia beee(nae humtafuta mwengine na kumwambia mambo yako).

Ndukiiiii
 
Haha ndo unajua leoo..binadamu wengi hasa ndugu ongea nao general topics tu kama siasa,weather nk..ishu zako binafsi don't say shit..wanajali kwani...
 
Habari wana JamiiForums,

Leo nina kitu kidogo cha kuwashirikisha kutokana na utafiti wangu mdogo nilioufanya wa kutembelea ndugu, jamaa na marafiki ambao hatukuonana kwa muda kidogo. Nilichobaini ndugu zangu tujifunze kuficha siri zetu za kimaisha ikiwemo changamoto mbalimbali kwani si kila utakaemuelezea ukiamini ni ndugu na rafiki wa karibu anaweza kuwa msaada kwako lahasha bali yanayoweza kutokea ni kama yafuatayo-:

1. Wengi hupokea kama taarifa tu ya umbea, hivyo ni mwanzo wa kujua undani wa maisha yako na hupata nafasi ya kwenda kuwaeleza wengine. Kwani kwa kufanya hivyo ni sawa na kuanika matatizo yako mbele ya jamii nzima.

2. Hufurahia miyoyoni mwao, kwani binadamu tunapenda kumuona mtu akianguka zaidi kuliko kufanikiwa.

3. Ni mwanzo wa kupata maswali ya kebehi yatakayokufanya kuvunjika moyo zaidi kuliko ya ulivyokuwa awali. Hivyo basi wanakuwa ni chanzo wa kuongeza tatizo na sio kulitatua.

4. Utawapa ujasiri wa kukuuliza mambo mengi ya undani ambayo walitamani kukuuliza mwanzo wakashindwa, hivyo kuwafanya kujua vingi kukuhusu wewe, na ukishawaeleza huguna na kukucheka kimoyomoyo. Mpaka hapo jua heshima yako ipo mikononi mwao.

5. Utawafanya wakudharau kwani kile walichokuwa wanahisi unaweza kuwa nacho watakuwa wamepata uhakika kwamba huna, hivyo hata kukusema na kukunyanyasa ni rahisi kwani watajua huna lolote hivyo huna cha kuwafanya. Hivyo ni sawa na jeshi lililogunduliwa ni aina gani ya silaha za kivita linamiliki kwani ulinzi wake ni hafifu hivyo wakati wowote laweza vamiwa.

CHA KUZINGATIA:
1. Kama una wazazi mtu pekee anaeweza stiri aibu yako ni mzazi pekee kwani ukiaibika wewe ni sawa ameaibika yeye.

2. Ni vyema kumshirikisha Mungu, kwani yeye ndio muweza wa kila kitu chini ya jua.

3. Ni heri ukamfwata mtu yoyote mwenye busura na ambae hamfahamiani akakupa ushauri juu ya tatizo lako kwani huyo hawezi ona umuhimu wa kufanya yote hayo kwa kuwa hakujui.

4. Si kila jambo au tatizo, unahitaji msaada kutoka kwa mwingine mengine ni ya kupambana mwenyewe na kumuomba Mungu wako.

5. Kila unaemuona mbele ya macho yako ana matatizo kama yako au hata kuzidi yako lakini swali moja la kujiuliza kwanini yeye hakwambii ya kwake ni kwa sababu anatambua thamani yake.

****TUJIFUNZE HAYA DUNIA YA SASA***
SIO KAMA ILE YA ZAMA ZILE
FACT
Ubarikiwe
 
Ujumbe mzuri sana ila heshima yangu ipo mikononi mwangu. Siwaogopi sana binadamu, hauwezi kuwaridhisha wote hata ufanyaje. Unaweza kukaa kimya napo watakusema tu.

Fanya linalokufurahisha na lisiloathiri wengine, kuhusu watasema nini, waachie wenyewe kwa sababu hauwezi kuwazuia.
 
Back
Top Bottom