Mambo ya kuyaepuka kwenye gear box ya Automatic

Ila kutumia O/D Off hapo vipi? Maana mie nikitaka overatake on highway speeds lazma nifanye O/D Off kisha narudisha ON!

Gari inavuma ikirudi gear ya 3, ila nikiiwasha gear zinaenda 4-5 chap na wepesi unaongezeka maradufu sambamba na speed naikata gari kama imesimama.
 
Nichangie na mimi Pointi namba 3.... Nimewahi kuona spear tire imeandikwa kuwa isitumike zaidi ya umbali wa 60km, aina ya gari ilikuwa ni hizi minicars zenye 660cc.
 
Mwaka 2013 brake pads za mbele zilishawahi kunichomokea hapo kitonga sema nlikua nalamilia mteremko, nikichofuata ni kuzama shambani kwa mtu ndio ilika pona yangu na abiria wangu
Pole sana mkuu, hahaha najaribu ku imagine unatia mguu kati halafu hamna kitu! Hahahah kuingia shamba haikwepeki πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ breki mgomba!
 
Pole sana mkuu, hahaha najaribu ku imagine unatia mguu kati halafu hamna kitu! Hahahah kuingia shamba haikwepeki πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ breki mgomba!
natia mguu kati naona moshi unatoka mbele kube mafuta ya brake yanaingia kwenye brake disc ya moto ilikua kimbembe nliwasha hazard na full light na natembea na honi hadi naingia shambani πŸ˜€ πŸ˜€
 
Unamaanisha aondoe mguu kwenye accelerator ?Unamaanisha nini wakati gari inatembea. Husisha jibu lako na pedals ndo utaeleweka zaidi.

Mimi hunitokea sana wakati nageuza gari...ninakuwa kwenye D nanyunyiza break kwa mbali na R gear inaingia vizuri tu ingawa kuna mlio fulani usiokuwa wa kawaida husikika na gari hustuka na kuanza kurudi nyuma as if hakuna uharibifu lakini baada ya kujisomea tabia hiyo nimekoma
 
Unamaanisha aondoe mguu kwenye accelerator ?Unamaanisha nini wakati gari inatembea. Husisha jibu lako na pedals ndo utaeleweka zaidi.

Siyo tu uondoe mguu kwenye accelerator. Unatakiwa ukanyage brake kabisa. Kwa sababu kuna gari hata ukiondoa mguu kwenye accelerator bado inatembea...
 
Ni bora uache mapema... kwa maana utakuja kuingia gharama kwenye gearbox wakati gearbox yako labda ingekaa muda mrefu...
 
O/D iache tu ON mkuu wala hakuna ulazima wowote wa kuizima. Na wala haina athari yoyote...
 
Nichangie na mimi Pointi namba 3.... Nimewahi kuona spear tire imeandikwa kuwa isitumike zaidi ya umbali wa 60km, aina ya gari ilikuwa ni hizi minicars zenye 660cc.

Unajua kikawaida kila unapobadili tairi za gari yako inatakiwa ufanye wheel alignment.

Ndio maana hiyo spea tairi wameandika usiendeshe zaidi ya 60km sababu wengi hufunga tu na kuanza kuendesha.
 
Mwaka 2013 brake pads za mbele zilishawahi kunichomokea hapo kitonga sema nlikua namamizia mteremko, nikichofuata ni kuzama shambani kwa mtu ndio ilikua pona pona yangu na abiria wangu

Aiseee pole sana mkuu....
 
natia mguu kati naona moshi unatoka mbele kube mafuta ya brake yanaingia kwenye brake disc ya moto ilikua kimbembe nliwasha hazard na full light na natembea na honi hadi naingia shambani πŸ˜€ πŸ˜€

Aiseeeee noma sana.
 
Siyo tu uondoe mguu kwenye accelerator. Unatakiwa ukanyage brake kabisa. Kwa sababu kuna gari hata ukiondoa mguu kwenye accelerator bado inatembea...
Ndiyo hivyo,Gari zote ukitowa mguu kwenye accelerator hazisimami bali kasi inapungua tu maana kunakuwa bado na Kinetic Energy. Ili gari isimame lazima ukanyage break.ila unapokuwausikanyage unashuka galope kali usikanyage break continousily.
 
kwanini usikanyage breki continuiusly?
 
Kuna gari nyingne zina herufi B .. nayo ina kazi gani? Ni kama L au?

B ina maana ya Brake. Yaani itatumika kama engine brake wakati unashuka mteremkoni, itaongeza drag kwenye engine hivyo engine haitakuwa kama ipo free...

Pia itakusaidia kwenye kupunguza matumizi ya brake. Hivyo brake zako hazitaisha haraka. Japo nayo ni gear ndogo kama tu ilivo L
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…