Mambo ya kustaajabisha msibani

Mambo ya kustaajabisha msibani

PRINCE VELLA

New Member
Joined
Oct 2, 2014
Posts
1
Reaction score
3
Wakuu habari,

Miongoni mwa mambo yanayonitafakarisha ni haya hapa:

1. Watu kula na kunywa msibani

2. Watu kupigania chakula msibani

3. Watu kuwashangaa na kuwachukukia wasiokula msibani.

Najiuliza kuna sababu gani ya msingi, mtu anayetokea nyumbani kwake mwendo wa hatua 10, 40, 100 au hata ndani ya 5km kwenda kula chakula msibani? Kwanini asile kwake?

Kwanini Wafiwa wateseke kufikiria gharama ya kuwapikia waombolezaji? Hii tabia hailengi kuwatweza na kuwaimiza Wafiwa?

Kuhusu kupigania na kuiba chakula msibani nalo ni gumzo maeneo mengi sana. Tatizo hilo linasababishwa na kupika msibani.

Kwanini pia watu wenye tabia ya kula msibani wanakerwa na yule asiyekula?

Mimi najua chakula kinapikwa kwaajili ya Wanafamilia, ndugu na watu wachache wanaohudumu katika msiba husika au wageni wanaotokea mbali.

Naombeni kuelimishwa!
 
Shida Nini kula msibani,ni maombolezo,kufarijiana,kujitafakari juu ya kifo na ndio mwisho wetu,huyo aliyekufa kagoma kula milele!
 
Back
Top Bottom