Mambo ya kufanya ili Simba itishe katika kombe la shirikisho

thechosenone

Member
Jan 10, 2016
17
5
Simba inahitaji kujiimarisha zaidi kwani msimu ujao wanajukumu la Ligi Kuu na michuano ya Kombe la Shirikisho ambyo wanahitaji kufanya vizuri.

Klabu ya Simba imemaliza nafasi ya pili nyuma ya mabingwa wa Ligi Kuu msimu huu klabu ya Yanga kwa tofauti ya magoli ya kufunga na kufungwa.

Simba ilikuwa na asilimia zaidi ya 60 kunyakuwa ubingwa msimu uliopita kabla ya kuanguka dakika za mwishoni na kuwaruhusu Yanga kutetea taji lao.

Msimu ujao Simba watashiriki michuano ya shirikisho Afrika hivyo wanahitaji marekebisho makubwa kwenye timu yao ili kuendana na kasi ya shirikisho Afrika na Ligi kuu Bara.

Ili kunyakuwa taji la Ligi Kuu msimu ujao na kufanya vyema michuano ya kimataifa, klabu ya Simba wanaitaji kufanyia mabadiliko baadhi ya maeneo yaliyokuwa na mapungufu msimu uliopita.

Haya ni mambo ambao Klabu ya Simba inaitaji kuyaongezea nguvu kwa ajili ya msimu ujao.

NAFASI YA BEKI WA KATI
Mlinzi wa kati ni nafasi iliokuwa na changamoto kubwa sana Simba msimu uliopita hasa baada ya kuumia Method Mwanjale, Simba wanaitaji mlinzi mwenye uwezo mkubwa kuliko mabeki waliopo sasa, mwenye uwezo mzuri wa kucheza mipira yote ya juu na ile ya chini ili kuweza kupambana na washambuliaji wajanja kwenye michuano ya Afrika.

KIUNGO MKABAJI
Simba ina utajiri wa viungo washambuliaji wengi wenye ubora, kiungo mkabaji bado ni sehemu yenye mapungufu makubwa, James Kotei na Jonas Mkude bado wanaitaji mtu wa kuwapa changamoto, anaitajika mkabaji mwenye uwezo mkubwa wa kuusoma mchezo na kuilinda safu yake ya ulinzi kwa umakini.

MSHAMBULIAJI WA KATI
Ni moja ya idara iliyo iangusha klabu ya Simba msimu uliopita kwenye Ligi Kuu, Mavugo na wenzake kwenye safu ya ushambuliaji hawawezi kuifanya Simba ikatisha msimu ujao kwani uwezo wao wa kufumania nyavu ni mdogo.

Msimu ujao Simba wanaitaji mshambuliaji mwenye jicho la goli, ambaye kufunga magoli 15 na kuendelea siyo tatizo kwake, mwenye nguvu, kasi, mzuri kwenye mipira ya juu na ya chini.

CHANZO: MAMBO YA KUFANYA SIMBA ILI ITISHE KATIKA KOMBE LA SHIRIKISHO
 
Wenzio wanawaza namna ya kupiga pesa wewe unawaza namna ya kuifanya timu imara, kwa uongozi uliopo sahau hayo kbsa jiandae kudanganywa kama ulivyohadaiwa rufaa FIFA..mashabiki , wapenzi na wanachama wa mbumbumbu fc mnasumbuliwa na tatizo la umbumbumbu ndiyo maana viongozi wenu wanafanya watakavyo
 
fukuza omog, bukungu, mavugo, blagon, sajili ngoma, niyozima, msuva ...,..,,,,,, etc
 
Kwa mashabiki tuchange twende wenyewe FIFA tukachukue point zetu 3 ndo kieleweke.
 
Back
Top Bottom