Mambo ya kuepuka kama wewe ni dereva wa Automatic Transmission Car

Joseverest

JF-Expert Member
Sep 25, 2013
52,480
70,593
Teknolojia ya vyombo vya usafirishaji inabadilika kwa kasi sana kadri miaka inavyokwenda. Leo hii makampuni mengi yanayotengeneza magari yanazalisha magari mengi yenye uwezo wa kujibadilisha gia yenyewe (Automatic Transimission Cars) tofauti na hapo zamani.



Kuna tofauti kubwa sana ya kiutendaji kati ya magari haya ya automatic na yale ya manual. Magari haya ya automatic ni rahisi sana kuyaendesha kwa kuwa sehemu kubwa ya mfumo wa utendaji wake ni wa kisasa kabisa. Ila kuna vitu vya msingi usivyotakiwa kufanya wakati unaendesha magari haya ili kuongeza maisha ya gear box (Transmission Box).

1. Usipaki gari lako bila kubana Parking Brake

Mara nyingi madereva wamekuwa wakipaki magari yao kwa kuweka transmission handle kwenye herufi P, bila ya kuengege Parking Brake. Kama wewe ni mmoja wao tafadhali acha kufanya hivyo kwa sababu Parking Pawl, kichuma kinachoizuia gari kuondoka wakati imewekwa kwenye Park ni kidogo sana na hakijatengenezwa kwa kazi hiyo. Hivyo ikitokea mtu akaligonga gari lako kidogo kuna uwezekano mkubwa wa gari lako likaanza kutembea kama ulikuwa hujalizima. Pia kipande cha Parking Pawl kilichovunjika kinaweza kikaleta matatizo makubwa katika gear box yako.

2. Epuka kutumia Gear kubwa kama brake

Mara nyingi wakati unashuka milima mkali na gari ya manual huwa tunashusha gari katika gear kubwa kama namba 2 au 1 ili kupunguza kasi ya mwendo. Usijaribu kufanya hivyo kwa gari ya automatic transmission, kwa sababu itasababisha kuchubuka na kulika kwa vyuma vya ndani ya transmission box na kuleta usumbufu hapo baadae.

3. Usibadili Gear wakati mzunguko wa engine wa gari ni mkubwa

Kubadili gear wakati mzunguko wa engine wa gari lako ni mkali ni kitu kibaya kwa sababu itasababisha kulika kwa clutch plates za ndani ya gear box yako na kukuletea matatizo hapo baadae.

4. Usibadili Gear ya mbele kwenda ya nyuma moja kwa moja au ya nyuma kwenda ya mbele moja kwa moja bila ya kusimamisha gari kwanza

Simamisha gari lako kabisa kabla ya kuamua kubadili gear ya kutoka mbele na kurudi nyuma au vinginevyo. Kufanya hivyo bila kusimamisha gari lako kutapelekea uharibifu mkubwa katika gear box yako.

5. Hakikisha engine inapata joto la kutosha kabla ya kuanza kuendesha gari lako

Kama ulilipaki gari lako muda mrefu sana no bora ukaliacha kwa muda baada ya kuliwasha ili engine ipate joto la kutosha na kufanya vimiminika vyote vya katika gari kutawanyika na kufika katika maeneo husika katika kiwango stahiki.

6. Usipitishe muda wa kufanya service mara kwa mara

Wengi tumekuwa na tabia ya kupitisha muda wa kuyafanyia service magari yetu mara kwa mara. Maisha na ubora wa gari lako hutegemea sana muda wa service hasa kubadili oil za engine na transmission box, brake pads, air filter na vingine vingi.



Karibuni kwa nyongeza na hoja nyingine kama zipo tujifunze


Credits: Swahilitech
 
Sijaelewa unaposema usibadili gear wakati mzunguko wa engine ni mkubwa wakati ni automatiki.Na uliposema tusibadili gear ya mbele kwenda ya nyuma moja kwa moja wakati ni auto.
Hebu nifanulie hapo mkuu.
Ilo la kwanza hata mi sijamsoma, ila kuhusu gear ya mbele kwenda nyuma ni kwamba, usihamishe ile knob kutoka kwenye D (drive) kwenda R (reverse) wakati gari ikiwa inatembea...
 
Sijaelewa unaposema usibadili gear wakati mzunguko wa engine ni mkubwa wakati ni automatiki.Na uliposema tusibadili gear ya mbele kwenda ya nyuma moja kwa moja wakati ni auto.
Hebu nifanulie hapo mkuu.
Anamaanisha usitoe gear no 2 ukaweka D ( na vice versa ) wakati gari iko kwenye motion japokuwa sioni kama ni tatizo ..Mimi huwa ndo ninavyoendesha hivyo miaka yote lakini sijawahi pata tatizo lolote na geabox.. Huwa napenda kuondoka na gear no 2 then ikichanganya natupia D hapo ni murua kabisa..
 
Anamaanisha usitoe gear no 2 ukaweka D ( na vice versa ) wakati gari iko kwenye motion japokuwa sioni kama ni tatizo ..Mimi huwa ndo ninavyoendesha hivyo miaka yote lakini sijawahi pata tatizo lolote na geabox.. Huwa napenda kuondoka na gear no 2 then ikichanganya natupia D hapo ni murua kabisa..
Kuna "L", "2" na "D"(D1,D2,D3) kwa gear za kwenda mbele, alichomaanisha ni rpm kuwa juu sana (kisadifu cha mzunguko wa engine)...madereva wengine hupendelea kuendeshea katika mizunguko ya juu. Mfano gari nyingi za automatic za kisasa kuna option ya kuendesha kama manual, yaani unabadili gear kwa button au shifting paddles zilizopo kwenye sterring. Binafsi nimemwelewa hivyo
 
Sijaelewa unaposema usibadili gear wakati mzunguko wa engine ni mkubwa wakati ni automatiki.Na uliposema tusibadili gear ya mbele kwenda ya nyuma moja kwa moja wakati ni auto.
Hebu nifanulie hapo mkuu.
Namaanisha gari likiwa linatumika kwenye spidi kali..yaani kubadili gia chapchap..kama hivo D UENDE R HAPO KWA PAPO
 
Sina maana nyingine mkuu..ni kama mwanajamii mpya alivosema
may be ana maana nyingine maana kutoka D then R wakati gari inatembea ni ukichaa mwingine. Tumsubili atoe ufafanuzi
 
Mada nzuri na inatoa shule haswa ila nina uhakika wakiamka wauliza maswali na waomba miongozo mtoa mada lazima atakimbia
 
Mada nzuri na inatoa shule haswa ila nina uhakika wakiamka wauliza maswali na waomba miongozo mtoa mada lazima atakimbia
Uko sawa Mtoa mada mwenyewe nime C&P ili nijifunze zaidi ili niongeze ufaham kidogo nilio nao...Lakini siwezi kukimbia kwa sababu naamini wataalamu wapo watatujuza hapa sawa hapa sio sawa
 
by the way gari za kisasa likiwa linatembea kwenda mbele mara kwa bahat mbaya ukataka weka R huwa haikubali had lisimame hivo linakusaidia kutoharibu vitu
 
Sidhani kama kweli wewe ni dereva.
Achilia mbali ufundi.
Sasa mkuu kwenye automatic ukiwa uko kwenye D halafu unaraka urudi nyuma si utasimama kwanza ndio upeleke Gear Lever kwenye R?? au ni automatic ipi wewe unayodhani
 
Sidhani kama kweli wewe ni dereva.
Achilia mbali ufundi.
Kuhusu ufundi mimi sio fundi Gari...nina idea kidogo ya kuendesha gari na nipo katika kujifunza

Hii taarifa source yake ni swahilitech.com kwa hiyo usifikiri labda vyoote ni mimi nimeandika
 
Back
Top Bottom