Mambo usiyoyafahamu kuhusu Popo (Bat)

Wild Flower

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2023
Posts
969
Reaction score
1,939

Kila tarehe 17 Aprili huadhimishwa kama Siku ya Kimataifa ya Popo (International Bat Day).

Lakini wanyama hawa huchukuliwa vibaya, huogopwa na mara nyingi kuchukiwa na kudhaniwa kuwa ni viumbe wenye Bahati mbaya, mkosi na Hatari jambo linalofanya wauwawe kwa hofu.

Lakini sehemu nyingine kama vile Pemba wanyama hawa hutumika kama kitoweo na huwa wanawindwa.

Aidha inashauriwa kuwa nyama ya popo ni hatari kutumika kama kitoweo kwani hubeba virusi kama Kichaa cha mbwa (Rabies), Nipah na Hendra.

Facts kadhaa kuhusu Popo

Kuna aina zaidi ya 1,400 za popo duniani ispokuwa sehemu zenye jangwa na maeno ya barafu (polar regions).

Popo ndo mnyama pekee wa jamii ya mamali wanaoweza kuruka angani kutokana na kuwa na mabawa yenye ngozi laini na mifupa ya vidole kwa juu.

Popo wanaweza kulala muda mrefu hadi miezi 6 kulingana na hali ya hewa ya eneno husika na hula mbu 1,000 kwa saa moja.
 
is it serious wanakula mbu...🤣
 
Hao ni kama walivyo ccm
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…