Ule msemop wa Mwaka mpya na mambo umekuwa kivitendo zaidi kwangu kwa huu mwaka, Namshukuru mwenyezi mungu kwa kubariki juhudi zangu na sasa nimefanikiwa kununua gari langu na sina budi kumshukuru Mungu, Nina takribani miezi mitatu tangu ninunue gari langu na haya ndio mambo niliyoyashuhudia na kuyaexperience.
1. Hadhi yangu(status) Imepanda - Simanishi kusema nlikuwa nadharaulika pindi sina gari, Hapana ila nachomaanisha ni kwamba status yangu imeongezeka, Majina kama Brother, Uncle, Tajiri(japo sio kweli), nshayazoea maana haipiti siku bila kuitwa hayo majina.
2. Gharama za matumizi zimepanda - Gharama zangu za matumizi zimepanda maana Gari linahitaji mafuta na ya elfu 5 kwa siku (mizunguko michache na mji ni mdogo), Gari inahitaji service kwenye gereji na hayo ni matumizi mapya kwangu, Gari inahitaji kushwa, n.k
3. Usafir wa usiku sio wa mawazo tena - Sina tabia za kutoka toka nje usiku ila ikija kutokea mfano nimeenda kwenye sherehe zile za kutoka usiku wa manane sitakuwa na hofu juu ya upatikanaji wa usafiri au gharama za juu za usafiri, Nina usafiri wangu.
4. mwili umekosa mazoezi - zamani kutembea, kukimbilia dala dala, na kugombaniana siti yalikuwa mazoezi tosha, ila kwa sasa k\sitembei umbali mrefu wala kukimbia ili kuwahi sehem nayotaka kufiaka, however naconsider kuanza kwenda gym
5. Watoto wa kike sio tatizo tena - Bado mimi ni kijana and off course napenda totoz, Gari langu limekuwa likinisaidia sana kunipandishia status na wanawake wanapenda wanaume wenye status,