Mambo nane kuhusu Whatsapp

Mambo nane kuhusu Whatsapp

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2016
Posts
20,746
Reaction score
25,638
Inawezekana ndio unaanza kutumia programu ya WhatsApp au hata pengine ulikua unatumia programu hiyo kwa miaka mingi sasa, lakini pia inawezekana ulikua unakosa kutumia programu hiyo vizuri kwa kutokujua mambo haya 10 yaliyopo kwenye programu hiyo maarufu ya WhatsApp.

1.KUBADILISHA MWANDIKO
KWENYE MESEJI.

WhatsApp imefanikiwa kuongeza sehemu maalum ambazo zinakufanya kutumia programu hiyo vizuri na kwa urahisi zaidi. Kwa kuandika *maneno* utaweza kukoleza maandishi ya maneno kwenye meseji, kwa kuandika
_maneno_ utaweza kuandika meseji kwenye staili ya mlazo na pia kwa kuandika ~maneno~ utaweza kuandika maneno na kuyawekea mkato.

2.Kurudia Meseji ya Mtu Kabla ya Kujibu (Quote)
Ili kuweza kurudia meseji ya mtu kabla ya kujibu shikilia meseji unayotaka kurudia kisha utaona imetokea menu yenye vitufe kazaa, kisha bofya kitufe cha nyota kisha utaona meseji ya mtu hyo imejiweka juu ya sehemu ya kujibu meseji, andika meseji yako kisha tuma.
Kujua Unachati na Nani Sana (iPhone)

3.Kujua Meseji Imefika na Kusomwa Saa Ngapi
Kama unataka kujua meseji uliyomtumia rafiki yako imefika na kusomwa saa ngapi, basi bofya kwenye meseji unayotaka kujua imefika sangapi kisha bofya kwenye sehemu iliyo na kitufe chenye alama ya (i) kisha utaona meseji yako imefika saa ngapi na kusomwa saa ngapi?

4.Kuzima Sauti ya Mlio Kwenye Meseji za Mtu Mmoja (Mute Conversation)
Inawezekana uko busy na unataka kuzima sauti ya group au mtu mmoja pekee unaweza kufanya hivyo kwa kushikilia meseji ya mtu unae taka kuzima sauti ya meseji zake kisha bofya kwenye kona kisha bofya Mute.

5.Kuzima Tick Mbili za Blue za Kuonyesha Meseji Imefika
Kuna wakati utaki mtu asione kama umesoma meseji yake hivyo kama unataka kufanya hivyo unaweza kubofya
Settings > Account > Privacy kisha ondoa tiki iliyoko kwenye maneno ya Read Receipts.

6.Kuzuia WhatsApp kuifadhi Picha na Video Kwenye Simu (iPhone)
Kama unatumia iphone na hutaki kujaza simu yako kwa picha na Video zinazotumwa kwenye magroup mbambali basi unaweza kufanya hivyo kwenye programu hiyo kwa kubofya Settings > Chats kisha zima kwa kuchagua off kwenye sehemu iliyoandikwa Media.

7.Hamisha Meseji Kwenda Kwenye Email.
Kama unataka kuamisha meseji kwenda kwenye email fanya hivi, wakati unachati na mtu bofya More > Email Chat kisha hamisha meseji zako. Kumbuka njia hii ni kama unatumia simu yenye mfumo wa Android, Kama unatumia iPhone unaweza kuchagua jina la mtu unaetaka kuhamisha meseji zake kisha nenda mpaka mwisho utaona sehemu iliyoandikwa Export Chat bofya hapo na utanza kuamisha moja kwa moja.
Kuficha Profile Picha Yako

8.Kama unataka kuficha profile picha yako kwenye programu ya whatsapp bofya Settings > Account > Privacy >
Status kisha chagua My contacts only
kisha hakikisha huja save namba ya mtu ambae hutaki aione profile picha yako.
Na hayo ndio baadhi ya mambo machache tu ambayo inawezakana kwa namna moja ama nyingine ulikua huyafahamu kwenye Programu ya WhatsApp

9. Kama Unataka Kuzima Last Seen
Kama unataka kuzima last seen kwenye programu ya WhatsApp fungua Settings > Account > Privacy > Last Seen . Kisha chagua unataka kuzima sehemu hiyo kwa watu gani, WhatsApp inakupa machaguo matatu ya kati ya : Everyone, My contacts, Nobody.

10. Kama unataka kujua unachati na nani sana na unatumia iphone njia hii ni rahisi sana. kwenye Whatsapp bofya Settings > Data and Storage Use > Storage Use hapo utaona majina yote ya watu uliochati nao sana bofya jina kuangalia idadi ya meseji picha au video ulizo chat na mwenzako. Kwa bahati mbaya kwa sasa bado hatuja weza kujua jinsi ya kufanya hivi kwenye simu za mfumo wa Android.
 
Unatumia whatsapp version gani mkuu

1. Unaweza ku mention jina la mtu kwenye magroup

2. Unaweza kuedit picha kabla hujaituma

3. Unaweza kuikata video kabla hujaituma

4. Unaweza weka shortcuts baadhi ya watu kwenye home screen ukawatext direct bila kuifungua whatsapp

5. Unaweza kuweka pop up notification ukasoma na kujibu text bila kufungua whatsapp app

6. Sio tu iphone, hata android unaweza kuzuia upakuaji wa sauti, video au picha

7. Ukiwa na iPhone una uwezo wa kuedit text uliyoituma kimakosa kabla haijasomwa

8. Unaweza kudukua chat za whatsapp za mtu mwingine kwa kutumia whatsapp web

9. Unaweza kuchat na mtu aliyekublok

10. Unaweza kubadilisha video kuwa GIF

hizo ni baadhi tuu yapo maujanja mengi, ningeweza kuongezea ingekuwa mnazungumzia GB whatsapp au GB whatsapp plus na Whatsapp plus au Whatsapp beta
 
Mbona yote hayo yawezekana kwa whatsapp ya kawaida tu(from playstore).
Ukiwa na rooted device, kisha ukiinstall xposed framework halafu una download na kuinstall xposed module yoyote ya whatsapp mfano whatsapp tweaks au whatsapp extension unakuwa ushamaliza kazi na unatumia whatsapp(from playstore) isiyokuwa na bugs wala virus.
 
Vipi kuhusu kuedit text uliyotuma, ukiroot simu unaweza?
 
Back
Top Bottom