Umeona na wewe kaka,
Yaani kwanza ni jukumu lako kumtunza mtoto wa watu...na halafu sheria inampa mamlaka ya kuuza phoenix yako ili eti akalipie matumizi yake na mtoto.
Hii sheria inahitaji marekebisho ya haraka sana.
Ndio maana mimi napendekeza kwamba ndoa ziwe katika mfumo wa corporate union. Kila mtu awe na shea zake ili mambo yakienda mrama ajue anachoambulia!!
Corporate union??? Dah umefika mbali! Kimsingi sheria hii iliandikwa wakati wanawake wamekandamizwa sana. Ila kwa sasa Law Reform
commission imependekeza mabadiliko yake. Ikiwa wataileta hadharani tusikawie kutoa maoni yetu!
Seriously, inabidi tuanze kuziangalia ndoa kiuchumi pia.
Niliwahi kutoa mawazo yangu kuhusu hili suala hapa JF na bado naamini ndoa za kisasa zinatakiwa kuangalia mchango wa mwanandoa ili kuamua nini anamiliki na anastahili kupata ndoa inapoparaganyika!!
Kuna concept mpya inaitwa economic refugees. Hawa ni watu wenye shida za kiuchumi, wamepigika! Sasa wanatafuta mtu mwenye pesa
wamuoe au waolewe nae ili kuepukana na shida zake. Nadhani suggestion yako itafaa kuondokana na matatizo haya
Ieleweke tuu kwamba mali mnazopata nkiwa ndani ya ndoa zinakuwa ni za wote labda pale ambapo itathibitika bila shaka kuwa ilikusudiwa mali iwe ni
ya mmoja wao. Kitendo cha kuongeza thamani katika mali hiyo, mfano kurekebisha nyumba, kujenga fensi nk inatosha kumpa mwenzi wako haki
katika mali hiyo na itachukuliwa kuwa wote mna share sawa katika mali hiyo. Ieleweke kwamba kwa mujibu wa kesi ya Bihawa Mohammed v Ali Sefu (moja ya kesi chache ambazo court of appeal imeamua kwa haki) hata kitendo cha mkeo kuwa mama wa nyumbani kinachangia yeye
kupata haki katika mali zenu
Katika hii kesi sina ugomvi na mwanamke kupewa mali walizochuma na mume wake. Ugomvi wangu ni kutoa 50% kwa 50%. Binafsi naamini kwamba haiwezekani watu wawili wakazalisha kwa usawa wa kiasi hicho.
Katika mazingira ya sasa...Ni muhimu kuweka kanuni zinazoweza kukutoa mchango wa kila mwanandoa kwenye mali walizochuma pamoja (matrimonial property)
Kuna ugumu katika kupima hasa pale ambapo mwanamke anachangia 'invisibly' ! Labda concept hii intokana na philosphy kwamba mkioana
mnakuwa mwili mmoja na mnapotengana mnapata nusu mbili zilizo sawa