maramia
JF-Expert Member
- Jul 17, 2015
- 2,029
- 1,345
Mambo mawili makubwa ambayo bila ubishi wowote lazima yatakitokea Chama cha Demokrasia na Maendeleo, kiwe kimeshinda ama kimeshindwa katika uchaguzi mkuu wa 25 Oktoba 2015 kwa mujibu wa mtazamo na mwonekano wa mwenendo wa chama hicho ni kama ifuatavyo:
1. Kama Chadema itashinda ktk uchaguzi mkuu wa mwaka huu utakaofanyika 25 Oktoba, kutaibuka mgogoro mkubwa wa kiuongozi wa siasa za kimakundi utakaotokana na mgawanyo wa madaraka ndani ya serikali. Hali hiyo itatokana na wakubwa wa chama na serikali kuwa na makengeza na ubabe ktk kuteua viongozi wa kuongoza wizara, idara, taasisi na mashirika mbali mbali.
Kutakuwa na makundi mawili makubwa yatakayotaka kulazimisha watu wao wateuliwe, kundi la Lowassa na wahamiaji wake na kundi la Chadema asili. Makundi haya yatakivuruga sana chama hicho na Lowassa na kundi lake litataka kuwaacha makada wa Chadema nje halitakubali kutii amri ya yeyote na kama mkuu wa nchi Lowassa atakuwa na maamuzi yake na hii itapelekea atimliwe ktk chama na serikali ya Chadema itaishia hapo.
2. Jambo la pili ambalo ni la hatari kubwa kama litatokea ni pale Chadema itakaposhindwa kuchukua dola tarehe 25 Oktoba. Hali hii ikitokea, Chadema itakuwa historia masikioni mwa watanzania, hakutakuwa na Mbowe wala Lowassa katika siasa za nchi hii, huo utakuwa mwisho wao kisiasa na haitakuja itokee Chadema ishike dola ktk miaka ya karibuni labda kwa uchache iwe baada ya miaka 50 mbeleni.
Anayebisha asubiri na atenge miaka yake mitano mbele atayakubali maneno yangu.
Na wakati tukisubiri kuyaona haya tumwombee Dk Slaa awe na afya yake naye ayashuhudie.