Mambo matatu yanayofanywa na wanawake chumbani ambayo huchangia sana kuniondoa kwenye mood ya kuendelea nao

Bajeti ya kunguru

JF-Expert Member
Sep 21, 2014
1,371
1,041
Habari zenu humu wana jamvi.

Leo nimeamua kuweka wazi humu mambo ambayo wanawake huyafanya tinapokuwa ndani ya mahusiano ya kimapenzi ambayo kimsingi huwa yanachangia pakubwa sana kwa mimi kuamua kuyavunja mahusiano yetu. Kifupi yananikera huwa nina asilimia kama 2% tu ya kuweza kuvumulia. Mambo yenyewe ni haya;

a). Mwanamke nimemuingiza gheto kwangu kumpa muda tu mdogo labda wa siku nzima nakuja kubaini ameshanichunguza droo zangu zote (simaanishi kwa lengo la kuiba) yaani kaisha pekuapekua vitu vyangu na ku act amevirudishia vilivyopokuwa. Huu ni ujinga sana mimi ndiye mmiliki wa chumba/nyumba hiyo hivyo najua mara ya mwisho vitu vyangu niliviachaje.

So sad! Hata nisipokwambia ila nimeumia na umenikera sana ulikuwa unatafuta nini? Wewe ndio mmiliki wa vitu vyangu? Au unamamlaka na mambo yangu? Aaah kwenda huko kafie mbele.

b) Mwanamke kujenga tabia ya kuomba hela kila baada ya kukutana kimwili unaniondoa kwenye mood ya kukualika gheto mara kwa mara kama mshkaji wangu. Mimi ni mwanaume natambua natakiwa nikupe huduma ndogondogo kama mtu wangu tukikutana hata sokoni unashida niombe kama ninayo nitakupa sasa wewe unakuwa na staili ya kila ukija ghetto muda wa kuondoka ndio muda wa majanga matokeo yake najutia kufanyana na wewe badala ya kufurahi.

Jenga mfumo wa kuniomba hela nje ya huu nitakuwa na furaha sana ya kukuita au kukupokea gheto siku ukinimiss kwasababu najua pakikucha ni shwari hakuna ndoano. Kuliko kukaa nawaza hivi huyu mtu mahusiano yetu upande wake yeye anayachukulia kama mimi au ananioje mimi? Aaaah buushhiit sikuzaliwa nimtumikie yeye aachane na mimi kabisa.

c). Tabia ya kujifanya umeshapitiliza tarehe za sindano (majira) unakuta anaanza kujiulizisha mmh! Hivi tarehe hazijapitiliza kweli? Mara mmh!

Nashukuru majuzi niliziona siku zangu. Sasa unabaki unajiuliza hivi huyu mtu zimo kweli au ananiandalia headache? Kwanini asijisimamie yeye kwanza kabla ya kuja? Kama mambo hayapo sawa si anijulishe akiwa huko huko home kwake mie nitajua mshkaji wangu kweli ananipenda kulikoni umeshanipa mzigo ndo unaanza kuongea hivyo.

Swala la kuzaa ni la kukubaliana wote. Sasa hapo kinachofuata naanza kwenda naye ki machale. Kuna raha ya kufanya nae tena? Aaah pita kushoto nipite kulia tufanye it's over ndicho kitachofuata.

Mwenzenu haya mambo hata hatutadumu na mwanamke kwenye mahusiano. Kwani ukifanya kimya unapungukiwa nini? Kuna jambo umeliona au unataka kulifanya niulize! Mimi ndio nitakwambia kama nitajisikia hivyo. Kama sitaki ulifuatilie nitakwambia achana nalo.
 
Kuna fala alinikera sana,nilinunua saa nying za kke nkauza zngine chaçhe nkabaknazo nikawa nmezihifadh,sasa huyo pimbi nilpomleta gheto akakaa kama sku nne,sku ya kuondoka ikabid nmpe saa moja,akaniuliza na hzo zngne umebakza za nn,nkamtania kuwa ntakuwa navpatia vibint vizur,aisee cha kushangaza alivyorud siku nyingne akazchukua bila kunipa taarfa,baada ya muda mrefu nikaja gundua hazpo,nkahis labda madogo wamezchukua,kumuuliza yeye ndo akakubal baadae nakuja kuona nyingne kaigawa kwa rafik yake kirahis tu,wakat mim hzo saa nilizinunua kwa bei kubwa,
 
Ila hiyo kupekua tunafanya si kwa lengo baya ila tu ni kujihakikishia kama kweli hakuna mwanamke mwingine?, mimi ntakua napekua tu kwakweli 🤔
Yaani hawa watu hawa naona kama maradhi yanawakomaa,mbona mimi sipekui mkoba wako? Unajua siku hizi mwanamke anataka amiliki mwanaume peke yake ila yeye ndio awe na wanaume wengi hivi,hivi vichwa vyenu hivi mnajiona mpo sawasawa kweli!? Yaani umbane mwanaume asiwe na mwingine halafu wewe unao kama watano .
 
Yaani hawa watu hawa naona kama maradhi yanawakomaa,mbona mimi sipekui mkoba wako? Unajua siku hizi mwanamke anataka amiliki mwanaume peke yake ila yeye ndio awe na wanaume wengi hivi,hivi vichwa vyenu hivi mnajiona mpo sawasawa kweli!? Yaani umbane mwanaume asiwe na mwingine halafu wewe unao kama watano .
Mi naona mtu hadi anaamua kuwa na wivu hivo ni sababu ana future na wewe so anajiridhisha ili azidi kuwa committed kwako, sasa kama ana wanaume 5 huo wivu kwako utatokea wapi? Kama nilivosema si kwa lengo baya, wivu kidogo unahitajika mkuu.
 
Mi naona mtu hadi anaamua kuwa na wivu hivo ni sababu ana future na wewe so anajiridhisha ili azidi kuwa committed kwako, sasa kama ana wanaume 5 huo wivu kwako utatokea wapi? Kama nilivosema si kwa lengo baya, wivu kidogo unahitajika mkuu.
Kwani kwa kupanga maneno kuna mtu wakuwafikia? Ila huku field sasa mwanamke mwenye wanaume wachache anao wawili
 
Back
Top Bottom