Mambo matatu ya kurekebisha ndani ya CHADEMA

Salary Slip

Platinum Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
52,162
Reaction score
162,591
Napenda kuwashauri CHADEMA watekeleze mambo matatu yafuatayo ili kuondoa propaganda chafu zinazosambazwa na CCM na ambazo zinaweza kuwa na athari mbaya kwa chama chetu.

Wana-CHADEMA,tunapaswa kutambua kuwa watu tunatofautiana katika uelewa wa mambo na katika mapokeo ya taarifa tunazoletewa au kuzisoma.

Kwa maana hiyo basi,mambo haya nashauri yatazamwe upya.
1.Ukomo wa kugombe uongozi urudishwe katika katiba ya chama na ikiwezekano ukomo uwe ni vipindi vitatu vya miaka mitano mitano.

2.Wanachama waruhusiwe kwenda mahakamni na mtu akishindwa kesi aruhusiwe kuendelea na uanachama wake.

3.Mh.Mbowe,kipindi chako cha sasa kikiisha,nakushauri usigombee tena na utoe fursa kwa wengine kugombea na wewe kama kiongozi, ujikite katika kuhakikisha chama kinapata mrithi bora,wa kuamimika na mwenye viwango.

Mchango ndani wako ndani ya chama ni mkubwa na wa kuthaminiwa sana ila ni vizuri sasa ukatoa nafasi kwa wengine ili kukinusuru chama na propaganda hizi.

4.Japo hatuchagu kiongozi kwa kuangalia kabila lake, lakini ikiwezekana katika uchaguzi wa mwenyekiti ajae jambo hili likaangaliwa kwa mapana na marefu yake.

Wenye akili na upeo wa kuona mbali watanielewa, ila wenye kukariri kuwa chama hakihitaji ushauri wa aina hii, watakuja hapa na vijembe na kejeli.

Niwaambie tu,hata kiburi na kujiamini kwa Zitto msingi wake ni uwepo wa hizi propaganda na ndio maana hata anapata public sympathy kutoka kwa baadhi ya watu na watu hao ni wengi tu huku mitaani tunakoishi.Fanya utafiti mdogo uone.

Propaganda zingine ni za msimu tu lakini sio hizi nilizoziongelea hapa.

Yangu ni hayo tu.
 
Last edited by a moderator:
Kubadilisha hicho kipengele cha katiba ni vizuri zaidi ili wanachama wawe na uhuru zaidi kisheria na kikatiba ndani ya chama.
La kipindi cha uongozi ni muhimu pia tuwe na kikomo japo si lazima ifanane na ya ccm,tunaweza kuwa na kipindi cha miaka sita cha uongozi wa mihula miwili miwili.
Nasema sita ili ikitokea mgombea mwingine ambaye si mwenyekiti akachaguliwa kuwa rais basi mwenyekiti aliyepo madarakani amwachie mwaka mmoja wa mpito yule rais wa nchi.
Ishu ya mgombea uenyekiti asiwe mchaga wala siliungi mkono hata kidogo,kama mtu anakubalika basi atashinda kwa kukubalika kwake na si kwa uchaga wake kwani siamini watakaomchagua watakuwa ni wachaga.
Kanda zote zifanye vizuri ili tuwapate watu wenye ushindani mkubwa na wanaouzika kwa wananchi na watakaokuwa wazuri zaidi ya wapinzani nje ya chama.
 
Nakubaliana na hoja zote isipokuwa moja ya uchaga. Udini, ukabila siyo sifa inayohitajika ili kupata kiongozi wa chama au serikali bali uwezo wa kuongoza na kukifikisha chama kwenye malengo yake. Hivyo afuataye awe mchaga, na afuataye awe mchaga hilo siyo swala, swala ni uwezo wa kuongoza.
 
Mkuu propaganda ni propaganda tu yatakuja mwengine cha msingi chadema ifocus kwenye mambo yanayohusu wananchi
 
Kubadilisha hicho kipengele cha katiba ni vizuri zaidi ili wanachama wawe na uhuru zaidi kisheria na kikatiba ndani ya chama.
La kipindi cha uongozi ni muhimu pia tuwe na kikomo japo si lazima ifanane na ya ccm,tunaweza kuwa na kipindi cha miaka sita cha uongozi wa mihula miwili miwili.
Nasema sita ili ikitokea mgombea mwingine ambaye si mwenyekiti akachaguliwa kuwa rais basi mwenyekiti aliyepo madarakani amwachie mwaka mmoja wa mpito yule rais wa nchi.
Ishu ya mgombea uenyekiti asiwe mchaga wala siliungi mkono hata kidogo,kama mtu anakubalika basi atashinda kwa kukubalika kwake na si kwa uchaga wake kwani siamini watakaomchagua watakuwa ni wachaga.
Kanda zote zifanye vizuri ili tuwapate watu wenye ushindani mkubwa na wanaouzika kwa wananchi na watakaokuwa wazuri zaidi ya wapinzani nje ya chama.
Umejiuliza ni watanzania wangapi wenye uelewa kama wako?

Ni wangapi wenye uwezo wa kuchambua pumba na mchele?

Mtu asie na uwezo wa ku-reason akitajiwa alianza Mtei akafuaya Bob Makani na sasa Mbowe wote wakiwa ni wachaga ni rahisi sana kuamini hizo propaganda.

Tusiotoe mwanya wa watu kutengeneza propaganda.
 
Nakubaliana na hoja zote isipokuwa moja ya uchaga. Udini, ukabila siyo sifa inayohitajika ili kupata kiongozi wa chama au serikali bali uwezo wa kuongoza na kukifikisha chama kwenye malengo yake. Hivyo afuataye awe mchaga, na afuataye awe mchaga hilo siyo swala, swala ni uwezo wa kuongoza.
Inaonesha mmegundua makosa yenu....kali kuliko yote ni chama cha kidemokrasia kukataza kesi kupelekwa mahakamani.nawaza chadema wakipewa dola watafanya kazi vipi na mahakama? Ndipo mambo ya kunyongana na kutupana kwenye makorongo kwa maagizo ya kamati kuu yatakapo anza
 
Don't allow others to set the agenda for you. We must continue to put them on the defense. We must not take instructions from them. Yaani unashauri tumwachishe Mbowe kugombea tena uenyekiti kwa sababu tu za kikabila?

It is not possible to be a little bit pregnant. Aidha CDM ina principles always au haina at all.
 
Napenda kuwashauri CHADEMA watekeleze mambo matatu yafuatayo ili kuondoa propaganda chafu zinazosambazwa na CCM na ambazo zinaweza kuwa na athari mbaya kwa chama chetu.

Wana-CHADEMA,tunapaswa kutambua kuwa watu tunatofautiana katika uelewa wa mambo na katika mapokeo ya taarifa tunazoletewa au kuzisoma.

Kwa maana hiyo basi,mambo haya nashauri yatazamwe upya.
1.Ukomo wa kugombe uongozi urudishwe katika katiba ya chama na ikiwezekano ukomo uwe ni vipindi vitatu vya miaka mitano mitano.

2.Wanachama waruhusiwe kwenda mahakamni na mtu akishindwa kesi aruhusiwe kuendelea na uanachama wake.

3.Mh.Mbowe,kipindi chako cha sasa kikiisha,nakushauri usigombee tena na utoe fursa kwa wengine kugombea na wewe kama kiongozi, ujikite katika kuhakikisha chama kinapata mrithi bora,wa kuamimika na mwenye viwango.

Mchango ndani wako ndani ya chama ni mkubwa na wa kuthaminiwa sana ila ni vizuri sasa ukatoa nafasi kwa wengine ili kukinusuru chama na propaganda hizi.

4.Japo hatuchagu kiongozi kwa kuangalia kabila lake, lakini ikiwezekana katika uchaguzi wa mwenyekiti ajae jambo hili likaangaliwa kwa mapana na marefu yake.

Wenye akili na upeo wa kuona mbali watanielewa, ila wenye kukariri kuwa chama hakihitaji ushauri wa aina hii, watakuja hapa na vijembe na kejeli.

Yangu ni hayo tu.
Kwa hapa Tanzania makabila yenye uwezo wa kuendesha vyama vya upinzani na kupata mafanikio ni haya Chagga,Meru,Iraq/Mbulu,Kyusa,Kurya basi.Wengine wote maneno tu.Chadema bado inajengwa sasa unataka wasaliti waje kuongoza Chadema?
 
Umejiuliza ni watanzania wangapi wenye uelewa kama wako?

Ni wangapi wenye uwezo wa kuchambua pumba na mchele?

Mtu asie na uwezo wa ku-reason akitajiwa alianza Mtei akafuaya Bob Makani na sasa Mbowe wote wakiwa ni wachaga ni rahisi sana kuamini hizo propaganda.

Tusiotoe mwanya wa watu kutengeneza propaganda.

Nakubaliana na wewe unaposema CDM wasitoe nafasi ya propaganda lakini ukweli utabaki kusemwa.
Wanaomchagua mwenyekiti ni kina nani?
Inawezekanaje watu wa mikoa yote wamchague mchaga ikiwa hana sifa?
Haiwezekani na haiingii akilini hata kwa yule ambaye ameishia vidudu.
La pili, Bob Makani hakuwa Mchaga.
Tatu, nitakuelewa zaidi ukisema asitokee mtu yeyote akawekewa zengwe kugombea uenyekiti ikiwa kama ana sifa stahiki.
 
Napenda kuwashauri CHADEMA watekeleze mambo matatu yafuatayo ili kuondoa propaganda chafu zinazosambazwa na CCM na ambazo zinaweza kuwa na athari mbaya kwa chama chetu.

Wana-CHADEMA,tunapaswa kutambua kuwa watu tunatofautiana katika uelewa wa mambo na katika mapokeo ya taarifa tunazoletewa au kuzisoma.

Kwa maana hiyo basi,mambo haya nashauri yatazamwe upya.
1.Ukomo wa kugombe uongozi urudishwe katika katiba ya chama na ikiwezekano ukomo uwe ni vipindi vitatu vya miaka mitano mitano.

2.Wanachama waruhusiwe kwenda mahakamni na mtu akishindwa kesi aruhusiwe kuendelea na uanachama wake.

3.Mh.Mbowe,kipindi chako cha sasa kikiisha,nakushauri usigombee tena na utoe fursa kwa wengine kugombea na wewe kama kiongozi, ujikite katika kuhakikisha chama kinapata mrithi bora,wa kuamimika na mwenye viwango.

Mchango ndani wako ndani ya chama ni mkubwa na wa kuthaminiwa sana ila ni vizuri sasa ukatoa nafasi kwa wengine ili kukinusuru chama na propaganda hizi.

4.Japo hatuchagu kiongozi kwa kuangalia kabila lake, lakini ikiwezekana katika uchaguzi wa mwenyekiti ajae jambo hili likaangaliwa kwa mapana na marefu yake.

Wenye akili na upeo wa kuona mbali watanielewa, ila wenye kukariri kuwa chama hakihitaji ushauri wa aina hii, watakuja hapa na vijembe na kejeli.

Yangu ni hayo tu.
Naona umejivua mahaba na kuamua kutumia kipaji ulichojaliwa na Mungu ili kuwakumbusha wenzako mambo muhimu yanayotakiwa kuzingatiwa.

Watu hawataki lakini suala la uchagga/ukasikazini, iwe propaganda ama kweli, linakiumiza CHADEMA.
 
Da adui anakupa war tactic
 
Sikuwahi kufikiri mwanachadema anaweza kuathirika kwa propaganda zinazotengezwa mtaa wa Lumumba.

Mkuu Salary Slip hatuendi hivyo hata siku moja, Huwezi kucheza ngoma inayopigwa na mpizani wako na kufuatisha midundo yake na mirindimo yake huku ukipiga mruzi na macho umeyafumba huku ukidhani eti unapambana naye... Hakika utatumbukia shimoni..!!!

Hiyo unayodai tuifuate ni Demokrasia ya woga na ni ubaguzi wa waziwazi usio na kificho ambao katu sikudhani unaweza kukukumba mtu kama wewe.. Inashangaza kwa kweli..!!!!

Tambua mwisho wa Propaganda hii ndio mwanzo wa Propaganda nyingine.. Kamwe kwenye siasa propaganda si kitu cha kukikwepa kwa kufuata namna mpiga propaganda anavyoieneza (Umeamkia wapi leo mkuu?) Hapa ilipo Chadema imepigwa propaganda kadha wa kadha na za hatari kuliko hizo unazodai eti tuzitende ili kuepukana nazo...!!! Mpaka wapiga propaganda wenyewe ilifikia kipindi wakajiaminisha sasa Chadema INAKUFA..!! Naam walijiaminisha kwamba itakufa kabla ya mwaka 2013 lakini je iko wapi??

Chadema ilidaiwa ni chama cha kikristo (Propaganda hii imewaathiri sana cuf mpaka leo kuhusu Uislam) IKAPITA SALAMA..
Chadema ilidaiwa ni chama cha Ukanda wa kaskazini... IKAPITA. SALAMA...
Kama vile haitoshi Chadema ilidaiwa ni chama cha Kigaidi...IKAPITA SALAMA.....!!!!!

Kumbuka propaganda zote hizo kila zinapoibuliwa na wapigaji zinakuwa na matukio kadha wa kadha ya kuisindikiza ili iweze kukubaliwa na wasikilizaji (wananchi) kamwe haivumishwi hivi hivi. Watakudanganyaje kwamba hiki ni chama cha Kigaidi?? Naam hapo watawakamata viongozi kadahaa wa chama na kuwahusisha na matukio hayo... Hapa wenye akili fupi watakubaliana na wapigaji..!!

Kuna watu huwa wanadai chama hiki ni Mpango wa Mungu..... Naam si bure ni kutokana na kuluka vihunzi,Mashimo,Makorongo na kila aina ya Mitego. Na mpaka tunavyoongea hapa mimi na wewe na wewe kuja na Mada yako hii ni kwamba Chadema ndicho chama kinachoshika nafasi ya pili kwa kuwa na wenyeviti wengi wa Mitaa kuliko chama chochote hapa Tanzina...!!! (Na hii ni baada ya kuungana na vyama vingine vinavyounda UKAWA pamoja na uchakachuaji mkubwa tuliouona ktk uchaguzi huo)

Kwa maoni yangu mimi ningesema.....

HAPO ILIPOSHIKA (CHADEMA) KATU ISIACHIE IENDELEE KUKAZA ZAIDI.

BACK TANGANYIKA
 
Last edited by a moderator:
Salary Slip

Una Mawazo Mgando sana Ndugu.
Kama vp na wewe nenda ACT kama unaona Chama hakina makazi bora kwako

Haya mambo tunayapuuza lakini ukweli ni kuwa yanatuathiri katika harakati za kuleta mageuzi nchi hii.

Hakuna propaganda nyingine zinazoweza kutusumbua zaidi ya hizi nilizotaja.

Tusiwe rigid badala yake tuwe flexible kama kweli tunataka kushika dola.

Kufanya mabadiliko hayo kuna ugumu gani?

Tambua kuwa wewe unaona hizi propaganda ni upuuzi kwasababu tu wewe ni muelewa ila u anasahau kuwa watu wote sio waelewa.
 
Last edited by a moderator:
Napenda kuwashauri CHADEMA watekeleze mambo matatu yafuatayo ili kuondoa propaganda chafu zinazosambazwa na CCM na ambazo zinaweza kuwa na athari mbaya kwa chama chetu.

Wana-CHADEMA,tunapaswa kutambua kuwa watu tunatofautiana katika uelewa wa mambo na katika mapokeo ya taarifa tunazoletewa au kuzisoma.

Kwa maana hiyo basi,mambo haya nashauri yatazamwe upya.
1.Ukomo wa kugombe uongozi urudishwe katika katiba ya chama na ikiwezekano ukomo uwe ni vipindi vitatu vya miaka mitano mitano.

2.Wanachama waruhusiwe kwenda mahakamni na mtu akishindwa kesi aruhusiwe kuendelea na uanachama wake.

3.Mh.Mbowe,kipindi chako cha sasa kikiisha,nakushauri usigombee tena na utoe fursa kwa wengine kugombea na wewe kama kiongozi, ujikite katika kuhakikisha chama kinapata mrithi bora,wa kuamimika na mwenye viwango.

Mchango ndani wako ndani ya chama ni mkubwa na wa kuthaminiwa sana ila ni vizuri sasa ukatoa nafasi kwa wengine ili kukinusuru chama na propaganda hizi.

4.Japo hatuchagu kiongozi kwa kuangalia kabila lake, lakini ikiwezekana katika uchaguzi wa mwenyekiti ajae jambo hili likaangaliwa kwa mapana na marefu yake.

Wenye akili na upeo wa kuona mbali watanielewa, ila wenye kukariri kuwa chama hakihitaji ushauri wa aina hii, watakuja hapa na vijembe na kejeli.

Yangu ni hayo tu.

Mapendekezo yako ni mazuri lakini mimi nakushauri yapeleke kwenye vikao vya chama, anzia ngazi ya chini kabisa, watakusikiliza tu usiwe na hofu, hapa JF ni kama umbeya tu wa akina Zitto et al.
 
Napenda kuwashauri CHADEMA watekeleze mambo matatu yafuatayo ili kuondoa propaganda chafu zinazosambazwa na CCM na ambazo zinaweza kuwa na athari mbaya kwa chama chetu.

Wana-CHADEMA,tunapaswa kutambua kuwa watu tunatofautiana katika uelewa wa mambo na katika mapokeo ya taarifa tunazoletewa au kuzisoma.

Kwa maana hiyo basi,mambo haya nashauri yatazamwe upya.
1.Ukomo wa kugombe uongozi urudishwe katika katiba ya chama na ikiwezekano ukomo uwe ni vipindi vitatu vya miaka mitano mitano.

2.Wanachama waruhusiwe kwenda mahakamni na mtu akishindwa kesi aruhusiwe kuendelea na uanachama wake.

3.Mh.Mbowe,kipindi chako cha sasa kikiisha,nakushauri usigombee tena na utoe fursa kwa wengine kugombea na wewe kama kiongozi, ujikite katika kuhakikisha chama kinapata mrithi bora,wa kuamimika na mwenye viwango.

Mchango ndani wako ndani ya chama ni mkubwa na wa kuthaminiwa sana ila ni vizuri sasa ukatoa nafasi kwa wengine ili kukinusuru chama na propaganda hizi.

4.Japo hatuchagu kiongozi kwa kuangalia kabila lake, lakini ikiwezekana katika uchaguzi wa mwenyekiti ajae jambo hili likaangaliwa kwa mapana na marefu yake.

Wenye akili na upeo wa kuona mbali watanielewa, ila wenye kukariri kuwa chama hakihitaji ushauri wa aina hii, watakuja hapa na vijembe na kejeli.

Yangu ni hayo tu.
Japokua umejita wewe nimwanachadema na nilikua nakuona humu ndani ukipambania chama lakini nimeanza kukutazama kwa jicho la tato jitafakari kama hayo uliyoyandika yana Afya kwa chama?
 
Back
Top Bottom