Mambo matano ya kufanya na mtoto mgonjwa

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,870
155,829
MAMBO MATANO (5) YA KUFANYA NA MTOTO AKIWA AMEBAKI NYUMBANI ANAUMWA.

Kuna wakati inatokea mtoto anaumwa inambidi asiende shule angalau siku moja au mbili ili apone. Bila shaka mzazi atahakikisha mtoto anapata dawa, chakula kizuri na kupumzika vya kutosha lakini ngoja niongezee baadhi ya mambo mzazi unaweza kufanya mtoto awe "active" na kumuondolea mtoto upweke ingawa inategemeana na ugonjwa.

1. KUANGALIA ALBUM YA PICHA. Nina imani kila familia inatunza picha katika album kama kumbukumbu. Ni fursa nzuri kwa mtoto kujifunza historia ya familia kupitia picha.

2. KUCHORA NA KUPAKA RANGI. Inavutia pale mzazi na mtoto wakijumuika pamoja kuchora picha mbalimbali. Vile vile shughuri ya kupaka rangi kiti au meza itamletea furaha mtoto na kusahau kama anaumwa.

3. MSOMEE VITABU AU MSIKILIZE "AUDIOBOOKS"
Usomaji vitabu ni shughuri isiyomchosha mtoto. Tafuta vitabu kadhaa mtulie sehemu iliyotulia umsomee kitabu kwa sauti. Au tafuta "audiobooks" msikilize pamoja.

4. MCHEZO YA KUFICHA VITU. Mzazi una wajibu kumfariji mtoto ili kumfanya achangamke. Ficha baadhi ya vitu nyumbani na mshawishi mtoto avitafute. Ikiwezekana mpe ahadi ya zawadi akifanikiwa kuvipa.

5. NENDENI KUTEMBEA KIDOGO . Pia itapendeza kama mzazi na mtoto mkitoka kutembea kidogo mpate hewa. Nendeni sehemu yenye utulivu mkipiga stori. Mnunulie hata pipi au icecream.

Kumbuka: msamiati wa "kumdekeza" mtoto umepitwa na wakati pengine wazazi wengi wanashindwa kuonyesha mapenzi kwa watoto wao ati kwasababu wataonekana "wanadekeza mtoto". HAPANA. Wakati wa kuonyesha mapenzi yako ni sasa onyesha vitendo. Mambo mengine ya kufanya unaweza kuongezea kulingana na mazingira cha muhimu mtoto ajisikie amani na furaha.
 
Back
Top Bottom