Mambo haya ni kinga usikamatwe kwa makosa ya Mtandao

Sodoku

JF-Expert Member
Feb 3, 2016
1,271
2,903
Najua kuna kipindi kama binadamu unakuwa na hasira, jazba, ghadabu, taharuki, tashtiti, mhemko, kiroho pasu, mshtuko na yooote mengi mengi. lakini mambo haya yote yanahitaj lugha sahihi kuyakabiri. wazungu wanaita satire,sarcasim au irony.

Ukisoma vitabu kama "MASHETANI, KAPTULA LA MAX, ROSA MISTIKA, ANIMAL FARM, na kile cha EMMANUEL MAKAID( nimekisahau jina) n.k ni vitabu ambavyo viliwasema wakubwa wa nchi. Lakini namna ambavyo lugha ilitumika haikuwa rahisi moja kwa moja mtu akasema kuwa amesemwa yeye kwa kuwa ilitumika lugha ya sanaa,fasihi nzuri kufikisha ujumbe wake. ingawa wakubw wenye akili walijua kuwa wanasemwa wao.

Hivyo nawasihi vijana wenzangu pamoja na kuwa na ghadhabu kubwa sana kwa yoooote mabyo mnadhan hayakuwa stahili kwenu kuyapitia basi mkumbuke kuwa mdomo uliponza kichwa.

Na kama mambo yamezidi sana tumia lugha ambayo haitakuingiza matatani. tumia fasihi, tumia tashdadi, kejeri n.k ambazo hizo wala hakuna atakayesema kwa ushahidi kuwa umemsema yeye.

Inawezekana kabisa kuna watu ambao wao wamekaa standby kutafuta wapi pa kupatia kazi. hivyo kosa lako dogo tu likasababisha ufungwe au ndugu zako wakuchangie pesa ya faini ambayo hiyo pesa mngeenda kufanyia mambo mengine ya maana zaidi.

Narudia MDOMO ULIPONZA KICHWA, wabunge hawa mnaowachagua ndio waliosimamia sheria hiyo ipite na ikapita kwa kura nyingi. Sasa wacha itumike la msingi sasa ni kuwa unaandika kwa akili.

Ukishindwa sana omba wataalmu wa lugha waedit kabla hujatuma na hili labda modulators wangeweza kuniajiri niwasaidie ku edit maneno yenye ukakasi ambayo yanaweza leta mushkeri kwenye uso wa wakubwa.

Usitake uone mkubwa akikunja sura, makunyanzi yake si mazuri kwako. Hivyo ili kuhakikisha kuwa JamiiForums inadumu na members wake wote hawafungwi nashauri Mods muanzishe kitengo hicho nami najitolea kuwa mhusika pia.
 
hatari sana!mtoa mada somo halijaeleweka..hahahaaa... kazi kwelkwel!(vtabu ametoa kama mf namna ya ktumia lugha bila kumgusa mtu direct kw matusi ila kaujumbe kanamfikia kunako moyo ili ajirekebishe)
 
The most certain test by which we judge whether a country is really free is the amount of security enjoyed by minorities.
 
kwa mfano kusema "mkuu wa kaya kachanganyikiwa"
Nani atakushtaki hapo. Ni rahisi kucheza na fasihi sema ushabiki ukizidi watu hujisahau
 
Mtoa maada umekuwa mkweli sana. Huwezi kutukana kiongozi Wa nchi harafu uachwe Salama tu. Rais Wa nchi ndo image ya Taifa letu. Tatizo watu bado wanaviongozi wao ambao hawakuchaguliwa na wananchi. Ukitukana utakamatwa tu maana hakuna namna nyingine
 
Back
Top Bottom