Wadau nimepata haya ndani ya Biblia nikasema kumbe kwenye Biblia kuna mambo ambayo hata Sayansi inakiri kuwa, ndivyo yalivyo. Nikasema tushirikishane.
1. JUA, MWEZI KUWA ANGANI.
Biblia. Mwanzo 1: 16-17. Mungu akafanya mianga miwili mikubwa, ule mkubwa utawale mchana, na ule mdogo utawale usiku. Akafanya na nyota pia. Mungu AKAIWEKA (mianga) KATIKA ANGA LA MBINGU ITIE NURU JUU YA NCHI.
*Sayansi pia inakiri Jua na Mwezi vipo angani na vinatoa mianga.
2. BAHARI KUPWA NA KUJAA.
Biblia. Ayubu 38: 8-11. Au ni nani aliyeifunga bahari kwa milango, Hapo ilipofurika kana kwamba imetoka tumboni.
Nilipolifanya wingu kuwa vazi lake, Na giza zito kuwa nguo ya kuifungia, Nikaiagiza amri yangu; Nikaiwekea makomeo na milango. Nikasema, UTAFIKA MPAKA HAPA, LAKINI HUTAPITA, Na hapa mawimbi yako yanyetayo YATAZUILIWA?
Biblia. Ayubu 14: 10-11. Lakini mwanadamu hufa, huifariki dunia; Naam, mwanadamu hutoa roho, naye yupo wapi? Kama vile MAJI KUPWA KATIKA BAHARI...
*Sayansi pia inakiri Bahari kupwa na kujaa. Maji ya bahari kwenda kule na kurudi huku.
3. SAYARI ZIPO ZAIDI YA MOJA.
Biblia. Ayubu 38: 32. Je! Waweza KUZIONGOZA (nyingi) Sayari kwa wakati wake? Au waweza kuongoza Dubu na watoto wake?
*Sayansi pia inakiri kuna sayari nane.
4. SAYARI ZINATEMBEA (MJENGEO).
Biblia. Ayubu 38: 32. Je! Waweza KUZIONGOZA (kitu kinachotembea) Sayari...
* Sayansi pia inakiri Sayari zinatembea (mjengeo).
4. DUNIA NI DUARA.
Biblia. Mithali 8: 26-27. Alipokuwa hajaiumba dunia, wala makonde wala chanzo cha mavumbi ya dunia; Alipozithibitisha mbingu nalikuwako. Alipopiga duara katika uso wa bahari...
*Sayansi pia inakiri dunia ni duara.
5. UPINDE WA MVUA (RAINBOW).
Biblia. Mwanzo 9:12-16. Mungu akasema, Hii ndiyo ishara ya agano nifanyalo kati yangu na ninyi, na kila kiumbe hai kilichoko pamoja nanyi, kwa vizazi vyote hata milele; Mimi nauweka UPINDE wangu WINGUNI, nao utakuwa ni ishara ya agano kati yangu na nchi. Hata itakuwa nikitanda mawingu juu ya nchi, UPINDE utaonekana WINGUNI, nami nitalikumbuka agano langu, lililoko kati yangu na ninyi, na kila kiumbe hai katika wote wenye mwili, wala maji hayatakuwa gharika tena kuwaharibu wote wenye mwili. Basi huo UPINDE utakuwa WINGUNI; nami nitauangalia nipate kulikumbuka agano la milele lililoko kati ya Mungu na kila kiumbe hai katika wote wenye mwili kilichoko katika nchi.
*Sayansi pia inakiri uwepo wa Upinde wa Mvua (rainbow) angani.
6. NYOTA ZIKO MBALI KUTOKA DUNIANI.
Biblia. Ayubu 22: 12. Je! Mungu hayuko mbinguni juu? Tena tazama UMBALI wa NYOTA, jinsi zilivyo JUU!
*Sayansi pia inakiri Nyota zipo mbali sana na dunia kuliko ulivyo Mwezi.
7. WATU KUISHI JUU YA DUNIA.
Biblia. Ayubu 37: 11-12. Naam, huyatweka mawingu mazito mzigo wa maji; Hulitandika wingu la umeme wake; Nalo hugeuzwa huku na huku kwa uongozi wake, Ili yafanye yote atakayoyaagiza JUU YA USO WA DUNIA HII IKAAYO WATU...
*Sayansi pia inakiri binadamu wanakaa juu ya uso wa dunia na siyo ndani.
8. RADI, MWANGA NA SAUTI.
Biblia. Zaburi 77: 17-18. Mawingu yakamwaga maji. Mbingu nazo zikatoa sauti, Mishale yako nayo ikatapakaa. SAUTI YA RADI yako ikawa katika kisulisuli; UMEME ULIUANGAZA ulimwengu. Nchi ilitetemeka na kutikisika.
*Sayansi pia inakiri uwepo wa Radi; sauti (mngurumo) na mwanga.
9. MASHARIKI, MAGHARIBI, KASKAZINI, KUSINI.
Mwanzo 13: 14-15. Bwana akamwambia Abramu, alipokwisha kutengana na Lutu, Inua sasa macho yako, ukatazame kutoka hapo ulipo, upande wa KASKAZINI na wa KUSINI na wa MASHARIKI na wa MAGHARIBI; maana nchi hii yote uionayo, nitakupa wewe na uzao wako hata milele.
*Sayari pia inakiri Dunia ina pande nne.
10. Binadamu kuumbwa kwa ngozi, nyama, mifupa na mishipa.
Biblia. Ayubu 10: 11-12. Umenivika NGOZI na NYAMA, Na kuniunga pamoja kwa MIFUPA na MISHIPA. Umenijazi uhai na upendeleo, Na maangalizi yako yameilinda roho yangu.
*Sayansi pia inakiri kibailojia kuwa, mtu aliumbwa kwa ngozi, nyama, mifupa na mishipa.
11. DUNIA HUKU KUKIWA USIKU, KWINGINE.
Biblia. Luka 17: 34-36. Nawaambia, USIKU huo watu wawili watakuwa katika kitanda kimoja (wamelala); mmoja atatwaliwa, mmoja ataachwa....
Watu wawili watakuwa SHAMBANI (kazi ya kulima hufanyika mchana), mmoja atatwaliwa, mmoja ataachwa.
Nyongeza: Yesu aliisema hii akimaanisha mzunguko wa dunia ulivyo. Ndiyo maana alisema siku ya mwisho itakuwa sehemu nyingine MCHANA, sehemu nyingine USIKU.