Mambo ambayo Marekani na Uchina hawatakaa wakubaliane

Mambo ambayo Marekani na Uchina hawatakaa wakubaliane

Dr Count Capone

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2017
Posts
1,879
Reaction score
3,309
-Na, Jumaa Kilumbi

Baada ya vita ya pili ya Dunia mwaka 1945 Dunia ilipata kiranja mpya wa kuiongoza, kiranja huyo alijipa kazi ya kuchunguza na kutatua kwa maslahi yake Migogoro yote iliyokuwa inaibuka, kiranja hakuwa peke yake alikua na Mpinzani aliyetaka kufanya kazi kama ya kiranja, waliizeveza Dunia wakamuita kila mmoja kuwa upande wao huku wakiahidi Maendeleo na Uhuru.

Wapinzani hawa walivutana kwa takribani miaka Hamsini, ajabu hawakuwahi ‘kushikiana mtutu’ hata siku moja, kila mmoja alimhujumu mwenziwe kadri alivyoweza kwa nafasi zao lakini kama Waswahili wasemavyo ‘Mafahari wawili hawakai Zizi Moja’ hivyo Dunia haikuwatosha wakakimbilia mpaka angani kuoneshana Umwamba, wakavimbiana mpaka kwenye mbinu za kuua Wanaadamu wenzao kwa haraka kisha wakaita ati ‘ni Maendeleo makubwa’.

Wakawagombanisha ndugu na ndugu wakagombana, Wakawaacha watoto bila wazazi, na Wakaleta Magonjwa yaliyobuniwa Maabara ili tu kukomoana.

Waswahili husema ‘hakuna marefu yasiyo na ncha’ Hatimaye Mwaka 1990 Mmoja akaanguka na kuiacha Dunia ikiwa na Kiranja pekee asiye na Mpinzani. Akaiamrisha dunia kwenda uelekeo alioutaka, alimuita Gaidi asiyempenda, akamuita Rafiki aliyempenda, akawaacha huru waliomtii, akawaangamiza waliomkataa, akawakopesha na kuiongeza Riba mara dufu akawafanya Wadeni wakabaki watumwa wa Deni lisilolipika akawafanya Vibaraka wake wa kuaminika.

Hatimaye akachomoza Dragoni kutoka Mashariki, Dragon aliyemlea mwenyewe, aliyemfundisha Teknolojia, aliyewapa Elimu watoto wake, akampa Msaada uliomfaa na ndio Dragon huyu leo kakua na anambishia Kiranja nayeye anatoa Misaada kwa anaowaona hawajaendelea, anawanyonya wanaomlegezea, anatumia mbinu zilezile alizojifunza toka kwa Mlezi wake. Ama kweli Waswahili waliona mbali kwa kusema ‘Kikulacho kinguoni mwako’.

Hivi karibuni kulishuhudiwa kukua kwa kasi Kiuchumi na Kiushawishi kwa nchi ya China, kiasi cha kuchuana na Marekani, China si ya kuambiwa na kusikia atakachosema Marekani, siku hizi nae anafanya yanayomfaa, anajitanua anavyotaka ametapakaa kila kona kuanzia Pakistan, Sri lanka, Djibout mpaka Zambia ya kwetu akiwekeza, akijenga Barabara mpaka Bandari kila mahali. Siku hizi kila uendako huwezi kosa kuwaona watu wao wakifanya shughuli mbalimbali za kiuwekezaji karibu katika kila nchi hapa Afrika.

China ndio Taifa linaloangaziwa kushika Usukani baada ya kuanguka kwa Marekani. Kwa Mataifa haya mawili kuwa makubwa huku kila mmoja akijiona kuwa na uwezo wa kuuongoza Ulimwengu yapo mambo kadhaa ambayo hawatakaa wakubaliane na yote ni sababu ya kila mmoja kuwa na Jeuri. Kwa mara nyingine Waswahili walikuwa sahihi kusema ‘Mafahari wawili hawakai zizi moja’.

SUALA LA TAIWAN
Taiwan ni nchi ambayo China inaamini ni sehemu ya mamlaka yake yaliyoporwa kutoka Mikononi mwake na ni ndoto yao kuona siku moja inawaunganisha watu wote wa China chini ya utawala mmoja, Suala la Taiwan linaanzia miaka ya nyuma katika kipindi ambacho China tuionayo hivi sasa haikuwepo.
Wakati Mweneykiti Mao akiwa katika harakati zake za ukombozi wa China nchi hiyo ilikuwa chini ya kibaraka wa Mataifa ya Magharibi ambaye alikuwa Madarakani kuhakikisha maslahi ya Mabeberu yanatimizwa kikamilifu.

Mao Zedong akiwa ameiva na sera zake za kijamaa alishirikisha watu watu wakamuamini wakamuunga mkono na wote wakakubaliana kutekeleza mpango wa kuwakomboa watu wa China kutoka katika Uongozi wa Kibabe.

Walipishana itikadi na waliokuwa washirika wao wakati wa vita dhidi ya japan watu kutoka Chama cha Kuomitang wakaishia kupigana mwishowe Mwenyekiti Mao akashinda vita akatawala China yote huku Mwenzake kutoka chama cha Kuomitang Bwana Chiang Kai-shek akatokomea visiwani huko Taiwan, Hainan na visiwa jirani, akiwa huko akatengeneza Serikali na akawa kiongozi wa Taiwan. Hali mbaya ya kiuchumi iliyosababishwa na vita ikamfanya Mwenyekiti Mao kusimamisha vita na kuelekeza Jitihada zote kwenye kuijenga China huku mpango wa kuiunganisha na Taiwan akatizamia kuufanya baadae.

Wakati huu Marekani ilifuatilia kwa karibu mwenendo wa China wakaunga mkono Harakati za Chiang kai-shek aliyekuwa na Itikadi za Kibepari ambaye hakuridhika aliendelea na madai ya kuiunganisha China chini ya Utawala wa Taiwan na madai hayo yapo mpaka hii leo. Marekani Wakawapa misaada ya Kijeshi ikiwemo Mafunzo, Wakashiriki mazoezi ya pamoja ya Kijeshi na Wakaingia Mkataba wa kuweka kambi yao ya Kijeshi ndani ya Taiwan huku lengo kuu ni ‘kuiambia’ China kuwa kama watataka kuivamia Taiwan basi wajue watakuwa wameingia Matatani na Marekani.

Uvamizi wa Taiwan haukuwa na Faida kwa China ile iliyoharibika Kiuchumi.
Hivi karibuni Vikosi vya China vimekuwa vikipiga ‘doria za kichokozi’ maeneo ya karibu kabisa na Taiwan jambo ambalo linalalamikiwa na viongozi toka kwa Taiwan na Marekani imekuwa ikiingilia kati kuitaka China kuheshimu sheria za kimataifa. Lakini China bado inaamini kuwa Taiwan inatakiwa kukombolewa na kuunganishwa na China kwa nguvu zote. Katika hili mabwana wakubwa hawataelewana kamwe.


CHINA KUJENGA ‘VISIWA FEKI’ KATIKA BAHARI YA CHINA KUSINI (SOUTH CHINA SEA)
China haijakurupuka katika hili, kwa mujibu wa sheria za kimataifa kuwa na kisiwa baharini kunakupa haki ya kuvuna Rasilimali bahari kwa upana wa zaidi ya maili 200 toka kisiwa kilipo, Tangu mwaka 2013 China imejenga visiwa vitano. Ujenzi wake huu pia unafanyika katika eneo ambalo ni la kimkakati kwani Bidhaa zenye Thamani ya zaidi ya Dola Trilioni tatu za Kimarekani hupitia Bahari hii kwa mwaka.

Viumbe bahari kama Samaki ambavyo hutumiwa kama Chakula hupatikana kwa wingi kwenye eneo hili, Rasimali kama Gesi asilia na Mafuta vinaaminika kuwepo kwa wingi sana. Ujenzi wa visiwa hivi unaipa China nguvu kubwa ya kuamua Sera za Kiuchumi barani Asia.

Marekani na Mataifa mengine wamekuwa wakipigania madai yao katika Bahari hii na imekuwa mpingaji mkubwa wa hatua hii ya China imeionya China kwa hatua hii huku ikiishia kusema kuwa haitakubali kuona China inajenga kambi za jeshi ndani ya visiwa hivyo kwani hali hii inatishia Usalama wa Dunia, na kuongeza kuwa italinda maslahi yake kwa nguvu zote katika Bahari ya kusini ya China.

Lakini China inatenda zaidi kuliko kuongea, inaendelea na Mipango yake ya kuviendeleza Visiwa vyake kila leo huku Picha za Satelaiti zikionesha Ujenzi wa Kambi za Kijeshi. Jambo hili halijapata jawabu bado na mvutano unaendelea.


VIRUSI VYA COVID-19
Virusi vya homa kali ya mapafu COVID-19 vilianzia katika jimbo la Wuhan huko China mwishoni mwa mwaka jana baadae kusambaa kufika Duniani kote, Marekani ni moja ya nchi iliyoathirika zaidi wakati China mambo yanarudi kama awali na Visa vipya vikipungua.

Kutokana mambo kuzidi kuwa magumu kila siku, Serikali ya Marekani inailumu China kwa kuficha taarifa za ugonjwa huu na kuviita ni Virusi vya Wuhan, jambo hili linaighadhibisha China.

Marekani inahamishia lawama zake kwa Shirika la Afya Duniani kwa kulituhumu kuwa kibaraka wa China, na kuamua kujiondoa katika kufadhili Shirika hilo jambo linalotishia Mustakabali wake, Lakini China haipo nyuma imejitokeza kifua mbele na kuongeza kiwango chake cha kuchangia. Kila mmoja anatumia Ugonjwa huu kuonesha ‘Makali yake’, Marekani yaonekana kurudi nyuma huku China ikionekana kupiga hatua zaidi.


MGOGORO WA HONG KONG
Hong kong imekuwa moja ya maeneo muhimu sana ya kiuchumi huko Asia, ilikabidhiwa mikononi mwa China miaka ya 1990 kutoka kwa Uingereza kwa sharti la kuwa Huru lakini ndani ya China. Hong kong walipaswa kuwa na Katiba yao, Kiongozi wao, Bunge lao, na Itikadi yao ya Kibepari ila ingebaki chini ya Utawala wa China ambao ni Wajamaa.

Uingereza iliikabidhi Hong Kong kwa China kwa masharti haya lakini hivi karibuni China imebadili sera zake juu ya Hong Kong china imedhamiria kuifanya Hong Kong kuwa ni sehemu kamili chini ya China kwa kuitangazia sheria mpya ya Usalama wa Taifa, Sheria ambayo imeonekana kulenga kuudhoofisha Uhuru walionao wana Hong Kong juu ya kujiamulia mambo yao.

Moja ya athari ya Sheria hii ni kuwa itavipa vyombo vya Usalama vya China nguvu zaidi ya kufanya Opersheni zake ndani ya Hong Kong ikiwa ni pamoja na ile ya kuwahukumu watu waliofanya makosa ndani ya Hong Kong nchini China.
Wananchi wengi wa Hong Kong wamepinga sheria hii na Marekani imejitokeza kuwaunga mkono na kuona kuwa sheria hiyo ina lengo la kuikandamiza na kuharibu mfumo mzima wa Maslahi yao ndani ya Hong Kong.

Haya ni mambo makuu matatu ambayo si China wala Marekani anaweza kumsikiliza mwenzake juu yake. Na ni mambo hayohayo yanayopelekea muendelezo wa visa mbalimbali baina ya nchi hizi ikiwemo Vikwazo inavyoweka Marekani kwa Makampuni ya China na visa vya kufungiana Ofisi ndogo za Kibalozi. Nimalize kwa kurejelea msemo wa Waswahili kuwa ‘Mafahari wawili hawakai Zizi Moja’.

NINI MAONI YAKO JUU YA HILI? CHINA NDIYE KIRANJA MKUU WA DUNIA KWA SASA AU ANAJARIBU JAMBO AMBALO HALIWEZEKANI?
KWA MAANDIKO MENGI KAMA HILI USIACHE KULIKE PAGE YETU YA FACEBOOK IFAHAMIKAYO KAMA ‘The FocuX’ fb.com/thefocux SASA.
FB_IMG_1597147810042.jpeg
FB_IMG_1597147799007.jpeg
FB_IMG_1597147804613.jpeg
FB_IMG_1597147793976.jpeg
 
Ishu ya hong Kong iko tofauti kidogo,
Ile sheria mchina kaiweka kwa sababu kuu mbili.
1,watu wengi walikuwa wanafanya makosa na wanakimbilia kule, so sheria ilikuwa inambana kuwakamata
2, ni security reason, hong Kong ilikuwa spy hub, kitu ambacho kilikuwa kinahatarisha usalama wake
 
Ishu ya hong Kong iko tofauti kidogo,
Ile sheria mchina kaiweka kwa sababu kuu mbili.
1,watu wengi walikuwa wanafanya makosa na wanakimbilia kule, so sheria ilikuwa inambana kuwakamata
2, ni security reason, hong Kong ilikuwa spy hub, kitu ambacho kilikuwa kinahatarisha usalama wake
Naam ni kweli, ameamua kujihakikishis usalama. Ni mjanja sana
 
Mh mkuu ni sahihi kusema hivi?
Ni sahihi sababu tunaelewa Marekani tuliyoizoea ilikuwa ni maneno na vitendo, ila kwa sasa Marekani imebaki maneno tu.
Mataifa yanayoinukia sasa kama Iran, Korea Kaskazini na hata ubabe wa Magu ni baada ya kujua kuna wababe wengine wenye kukidhi vigezo wameibuka kwa nguvu ambao ni kina Uchina na Urusi. Ingekuwa sio hawa mabwana Marekani angeshatia timu hapo Iran kwa gharama yoyote ile.

Marekani hana tena options yoyote ya kuendelea kuwa juu zaidi ya kukubali kushindwa ili atengeneze uchumi wa nyumbani kwake kwa aibu.
 
Ni sahihi sababu tunaelewa Marekani tuliyoizoea ilikuwa ni maneno na vitendo, ila kwa sasa Marekani imebaki maneno tu.
Mataifa yanayoinukia sasa kama Iran, Korea Kaskazini na hata ubabe wa Magu ni baada ya kujua kuna wababe wengine wenye kukidhi vigezo wameibuka kwa nguvu ambao ni kina Uchina na Urusi. Ingekuwa sio hawa mabwana Marekani angeshatia timu hapo Iran kwa gharama yoyote ile.

Marekani hana tena options yoyote ya kuendelea kuwa juu zaidi ya kukubali kushindwa ili atengeneze uchumi wa nyumbani kwake kwa aibu.
Aje kwenye meza ya win win situation ya makinikia!
 
Ni sahihi sababu tunaelewa Marekani tuliyoizoea ilikuwa ni maneno na vitendo, ila kwa sasa Marekani imebaki maneno tu.
Mataifa yanayoinukia sasa kama Iran, Korea Kaskazini na hata ubabe wa Magu ni baada ya kujua kuna wababe wengine wenye kukidhi vigezo wameibuka kwa nguvu ambao ni kina Uchina na Urusi. Ingekuwa sio hawa mabwana Marekani angeshatia timu hapo Iran kwa gharama yoyote ile.

Marekani hana tena options yoyote ya kuendelea kuwa juu zaidi ya kukubali kushindwa ili atengeneze uchumi wa nyumbani kwake kwa aibu.
nyie kaeni mkiota na kujifariji.

kwani kuna siku yoyote marekani aliishawahi kukabana live live na mkubwa mwenzie kiuchumi?? Si USSR wala CHINA ya sasa.

tuweke akiba ya maneno kwanza.
 
Kwa misingi hii mkuu naungana na wewe
Ni sahihi sababu tunaelewa Marekani tuliyoizoea ilikuwa ni maneno na vitendo, ila kwa sasa Marekani imebaki maneno tu.
Mataifa yanayoinukia sasa kama Iran, Korea Kaskazini na hata ubabe wa Magu ni baada ya kujua kuna wababe wengine wenye kukidhi vigezo wameibuka kwa nguvu ambao ni kina Uchina na Urusi. Ingekuwa sio hawa mabwana Marekani angeshatia timu hapo Iran kwa gharama yoyote ile.

Marekani hana tena options yoyote ya kuendelea kuwa juu zaidi ya kukubali kushindwa ili atengeneze uchumi wa nyumbani kwake kwa aibu.
 
The drogon without wings is a lizard.
the CCP is not really political party anyway, they are gangsters holding the people hostage.
china already failed
Screenshot_20200803-214826.jpg
 
Back
Top Bottom