Mambo ambayo kijana hutakiwi kufanya ili ujiwekee misingi ya maisha

Hajui tu akaangalie financial statements land huwa inawekwa wapi?kama sio upande wa Asset
Anaweza kuwa sawa kutokana na mtazamo wake au maana ya asset kwake. Maana wakati mwingine hasa maeneo ambayo yameenelea bila kujali mipaka, siyo lazima ardhi kupanda/kuongezeka thamani. Ila kwa mtazamo wako, ni sawa kuwa land ni asset.
 
===. KUCHAGUA KAZI.
Ni vigumu kupata Kazi ukiwa nje ya Kazi. Fanya Kazi uliyoipata upate Kazi unayoitaka.

===√. KUCHAGUA SEHEMU YA KUISHI /KUFANYIA Kazi.
Maisha ni safari ndefu, maisha ni popote, si lazima kukaa mjini. Hauwezi kujua ni sehemu gan iliyobeba mafanikio yako. Chagua sehemu yenye FURSA na si yenye MAGHOROFA.

===√. KUISHI BILA KUWA NA MALENGO.
Maisha si bahat mbaya au nzuri. Maisha ni mipango, Maisha yanaongozwa na malengo. Vile ulivyo leo ni matokeo ya jinsi ulivyopanga jana, na vile unavyoishi leo ndivyo kesho yako itakavyokuwa. PANGA KESHO YAKO SASA.

°===√. MAISHA YA KUIGA.
Maisha yako si ya mwenzako, na ya maisha ya mwenzako si ya kwako. Si kila ukionacho ni lazima ufanye, chagua kipi cha kufanya na kipi cha kuacha. Kupitwa na jambo wakat mwingine sio USHAMBA ni BUSARA.

===√ KUISHI JUU YA KIPATO CHAKO.
Ishi kulingana NA vile ulivyonavyo na si usivyonavyo. Kuwa na Busara katika MATUMIZI uepukane na MADENI yasiyo na ULAZIMA. RIDHIKA NA VILE ULIVYONAVYO.

===√.KUISHI BILA AKIBA.
kuweka akiba ni TABIA sio kiwango kikubwa cha Pesa. Jenga tabia ya kujiwekea akiba. Haujui ni kipi kitakupata muda USIOTEGEMEA.

===√. KUISHI KWA kutegemea MSHAHARA.
Mshahara haujawahi kutosha na hautatosha kama ukishindwa kuishi chini ya kipato chako na kuwa na njia mbadala za kuinua kipato chako. JARIBU NJIA ZINGINE MBALI NA MSHAHARA.

===√KUSHINDWA Kupangilia MATUMIZI YA PESA.
Maamuzi yako ya pesa ndiyo yatajayoamua hali yako ya kiuchumi baadaye. Ni muhimu kujua kipi cha kununua, kwa wakat gani na kwa sababu gani. Jifunze kutofautisha kati ya liability (dhima) mfano: gari ya kutembelea na assets (kitegauchumi) mfano:nyumba au kiwanja . TUMIA PESA YAKO KUNUNUA ASSETS KULIKO LIABILITY.

sent from toyota Allex
Exactly, İ like thic...!!
 
Mpk sasa hayo ndiyo ninayoyaishi nipo serikali nimeajiriwa ila nikitoka kazini naenda taasisi x napiga kazi mpk saa tano uck , sichagui kazi na sina marafiki wapuuzi wapuuzi wa kila mara bata

sent from toyota Allex
Hongera sana Mkuu natamani niwe kama wewe🤝💪
 
Msingi mzuri wa kufaidi maisha ni kuwa na roho ngumu hapo hela itakaa, halafu usisahau ukiendekeza ndugu utavuna magugu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom