Mimi kama mdau wa kilimo na ufugaji. Napenda kuwashirikisha jambo moja muhimu sana, pale unapoingia kwenye Tasnia ya ufugaji na kilimo jua kama biashara yoyote ile ina changamoto zake kama biashara nyingine. Hizi ni baadhi ya picha ambazo siyo rahisi kukutana nazo hasa kwenye mitandao ya kijamii. Mitandao hii imekuwa ikiaminisha kilimo na ufugaji ni rahisi hasa kwa wadau kupenda kutuonyesha mafanikio tu ili hali kwenye uhalisia wake sivyo.
Mara nyingi mitandaoni huonyeshwa mafanikio tu na si upande wa changamoto.
Pamoja na hayo yote Usikate Tamaa. Unaweza wekeza fedha na muda ukaishia kujifunza tu. Hivyo Jifunze Songa mbele. Picha hizi ni baadhi ambazo tulishare baadhi ya vijana kutoka ukanda huu wa Africa haswa kusini mwa jangwa la Sahara.
Challenge: Unaweza share picha ambazo ni nadra kutoka kwenye hii sekta kwa lengo la kujifunza.
Kilimo Kama uwekezaji mwingine unahitaji uhakikishe una rasilimali zote zinazohitajika wakati wote wa mradi.
Mkulima anatakiwa kuwa na mpango mkakati wa uzalishaji na wa masoko inayorandana.
Tukirudi kwenye kiambatanisho Cha picha hapo juu;
Mkulima hakujiwekeza kwenye elimu ya ya uzalishaji vyakutosha....
Mfano:
1. Magonjwa ya nyanya: Majani yanakauka kutoka chini kwenda juu; probably Ni late bright.
2. Jinsi ya kulima: angepunguza ukubwa wa eneo lakulima Kisha akainulia Miche kwa kuishikilia na fito.
3. Umwagiliaji: inawezekana kilimo hiki kilifanyika kipindi Bado Kuna mvua au umwagiliaji ulikuwa unafanywa jioni Sana kiasi kwamba Majani hayakauki.
4. Mbolea: Kuna uwezekano mkubwa mkulima aliweka Nitrogen zaidi kwa kuangalia ukubwa wa mmea na idadi ya matunda haviendani...
Sijasema kilimo hakina hasara, [binafsi nimepata ya kutosha] Ila maandalizi mazuri yanapunguza uwezekano wa kupata hasara.
Tujifunze kupitia magumu tunayokutana nayo ili kuweza kuvuka vikwazo katika kilimo.... Naunga mkono hoja ya kushirikishana changamoto kwani kupitia hizo tuta fine tune mipango yetu.
Kuna uzi wa kuangukia pua kwenye kilimo upo..watu wamefunguka mengi..utafute utajifunza mengi pia...kuna msemo wa kizungu unasema..our pictures looks happier than our really life.