Mambo ambayo huwezi kuyaona kwenye mtandao ya kijamii yanayohusu Kilimo na ufugaji

mbota

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
859
500
Habari zenu wafugaji wenzangu,

Mimi kama mdau wa kilimo na ufugaji. Napenda kuwashirikisha jambo moja muhimu sana, pale unapoingia kwenye Tasnia ya ufugaji na kilimo jua kama biashara yoyote ile ina changamoto zake kama biashara nyingine. Hizi ni baadhi ya picha ambazo siyo rahisi kukutana nazo hasa kwenye mitandao ya kijamii. Mitandao hii imekuwa ikiaminisha kilimo na ufugaji ni rahisi hasa kwa wadau kupenda kutuonyesha mafanikio tu ili hali kwenye uhalisia wake sivyo.

Mara nyingi mitandaoni huonyeshwa mafanikio tu na si upande wa changamoto.

Pamoja na hayo yote Usikate Tamaa. Unaweza wekeza fedha na muda ukaishia kujifunza tu. Hivyo Jifunze Songa mbele. Picha hizi ni baadhi ambazo tulishare baadhi ya vijana kutoka ukanda huu wa Africa haswa kusini mwa jangwa la Sahara.

Challenge: Unaweza share picha ambazo ni nadra kutoka kwenye hii sekta kwa lengo la kujifunza.

20210523_112037.jpg
 

kijani11

JF-Expert Member
Jan 19, 2014
6,921
2,000
Pole sana mkuu. Ukweli ni kuwa hakuna biashara isiyo na changamoto (risk), kikubwa ni kuzitambua na kutengeneza mbinu/namna ya kupambana nazo.
 

pleo

JF-Expert Member
Jun 20, 2013
2,886
2,000
Kilimo Kama uwekezaji mwingine unahitaji uhakikishe una rasilimali zote zinazohitajika wakati wote wa mradi.

Mkulima anatakiwa kuwa na mpango mkakati wa uzalishaji na wa masoko inayorandana.

Tukirudi kwenye kiambatanisho Cha picha hapo juu;
Mkulima hakujiwekeza kwenye elimu ya ya uzalishaji vyakutosha....
Mfano:
1. Magonjwa ya nyanya: Majani yanakauka kutoka chini kwenda juu; probably Ni late bright.

2. Jinsi ya kulima: angepunguza ukubwa wa eneo lakulima Kisha akainulia Miche kwa kuishikilia na fito.

3. Umwagiliaji: inawezekana kilimo hiki kilifanyika kipindi Bado Kuna mvua au umwagiliaji ulikuwa unafanywa jioni Sana kiasi kwamba Majani hayakauki.

4. Mbolea: Kuna uwezekano mkubwa mkulima aliweka Nitrogen zaidi kwa kuangalia ukubwa wa mmea na idadi ya matunda haviendani...

Sijasema kilimo hakina hasara, [binafsi nimepata ya kutosha] Ila maandalizi mazuri yanapunguza uwezekano wa kupata hasara.

Tujifunze kupitia magumu tunayokutana nayo ili kuweza kuvuka vikwazo katika kilimo.... Naunga mkono hoja ya kushirikishana changamoto kwani kupitia hizo tuta fine tune mipango yetu.
 

mbota

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
859
500
Pole sana mkuu. Ukweli ni kuwa hakuna biashara isiyo na changamoto (risk), kikubwa ni kuzitambua na kutengeneza mbinu/namna ya kupambana nazo.
Na hicho ndio ninajaribu kuwaonyesha kuwa tusihamasike tu kwa picha za mitandaoni tukasahau changamoto zilizopo
 

jiwe angavu

JF-Expert Member
Aug 28, 2015
3,615
2,000
Habari zenu wafugaji wenzangu
Mimi kama mdau wa kilimo na ufugaji...
Kuna uzi wa kuangukia pua kwenye kilimo upo..watu wamefunguka mengi..utafute utajifunza mengi pia...kuna msemo wa kizungu unasema..our pictures looks happier than our really life.

#MaendeleoHayanaChama
 

Tangantika

JF-Expert Member
Aug 12, 2018
2,778
2,000
Na hicho ndio ninajaribu kuwaonyesha kuwa tusihamasike tu kwa picha za mitandaoni tukasahau changamoto zilizopo
Tukianza kujafili changamoto wengi hawatajaribu kulima, wataogopa.Mafa ziwr zaifi za mafanikio kuliko kufeli.

Mtoto wa shule ya msingi ukimwambia unasoma ila kamwe hutakuja kuajiliwa ataipenda elimu?

Motivesheni spika wote hujadili mafanikio sio failure.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom