Mambo 6 Kiboko ya Usaliti katika Ndoa/Mapenzi.

G.T.L

JF-Expert Member
Jul 15, 2012
775
1,249
  1. Juhudi katika utafutaji wa kipato.Kutokana na mahitaji kuongezeka katika miaka ya karibuni,inalazimu mwanaume na mwanamke wote kwa pamoja washiriki katika kujiongezea* kipato ili kujitosheleza walau kwa mambo muhimu ya kila siku.Kiukweli ni nzuri sana kwa mwanamke kuepukana na hari ya utegemezi kwa kiasi kikubwa,Hii itajenga upendo wenye heshima na itamwongezea mwanaume kutambua umuhimu wa uwepo wa mwanamke umuhimu ambao ni adimu sana kuupata hasa kwa jamii za kiafrika.
  2. Maarifa juu ya mapenzi na tendo la ndoa.Mapenzi na tendo la ndoa ni vitu tofauti japokua tendo la ndoa ni kipengere mojawapo katika mapenzi.Ni wajibu wa kila mmoja kuhakikisha mwenziwake anafurahia mapenzi yenu ima kwa kujariana,kushauriana,kusikilizana na kuheshimiana.Linapokuja swala la tendo la ndoa ni wajibu wa kila mmoja kuhakikisha anajua ashughulike vipi ili kutoshelezana.Mambo haya ni muhimu sana katika tendo la ndoa
i-Kuandaana kisaikolojia kabla ya tendo la ndoa kwa mfano;kutumiana meseji endapo mpo mbali kidogo,kusuluhisha kama kuna mgogoro.
ii-Kuzijua sehemu za hisia za mwili wa mwenzi wako(sehemu za mwanamke zipo 12 na kwamwanaume zipo 5)
iii-Unadhifu na Usafi wa mwili kabla ya tendo la ndoa.
iv-Ushirikiano wapamoja wakati wa tendo la ndoa,Mfano;Mikao(style) ambayo italeta hari ya hisia zaidi,Mideko na kilio cha wastani toka kwa mwanamke humuhamasisha zaidi mwaume,kubembelezana na lugha za upole.

  1. Urafiki wa karibu zaidi.Unaweza ukawa na ndugu yako au mpenzi wako lakini asiwe rafiki yako.Urafiki ni hari ya kushirikishana mambo mengi pamoja naya siri binafsi.Kwaiyo,mfanye mwenza wako awe rafiki yako 100%.Mshirikishe mwenzako *mambo yote yanayokusibu,mfanye awe mshauri na mfariji wako ni jambo ambalo litamfanya ajisikie fahari kuwa na wewe kwa kutambua uwepo wake.
  2. Utu.Jijengee hari ya usawa kwa mwenzako.Mfanyie mwenzako ambayo hta wewe ungependa akufanyie.Ifanye akiri yako iijengee roho yako mazingira ya kua upendo na jamii inayokuzunguka.Kua mwepesi wa kusaidia,kushirikiana na kujari wanajamii wenzako.Jamii inapotambua mchango wako ni dhahiri utasifika na kuheshimika.Hivyo utamfanya mwenzako akupende zaidi na kuiga mfano toka kwako.
  3. Ukweli na uwazi.Huu ni msingi wa uaminifu katika kukuza upendo wa mwenzako.Uwongo hubeba tabia zilizojificha ndani yake(eg:Dharau,kiburi,Unafiki).Jitahidi kuwa mkweli kwa mwezako,kama kuna jambo hupendezwi nalo kuwa muwazi umweleze kwa lugha ya upendo.Usithubutu kuwa msiri katika mapenzi.Mnapokuwa faragha mueleze mwenzako hisia zako.Unapoona tatizo kuwa wa kwanza kushiriki katika utatuzi.
  4. Imani za kidini.Jifunze kuwa na maadiri mema.Jitahidi kushika mafundisho mema ya dini yako hususani wakristo na waislamu wote tunafundishwa kutoka nje ya ndoa ni dhambi mbele za mwenyezi Mungu.Kwahiyo,Imani yako imara itakufanya umuogope muumba wako na itakuepusha dhidi ya fikra potofu za usaliti.Pia itakurahisishia kujenga familia nzuri yenye furaha,amani na upendo.
NB: Kushauriana ndiyo busara ya mwisho katika mapenzi ya dhati,Uvumilivu wa ukimya ni mwanzo wa kujenga hira potofu na kufanyiana visa.
Huu ni uchambuzi binafsi.NAWASILISHA
 
tumesikia, ila hatufuati ng'o.

Shetwain keshakula oblongata.

note: asante kwa mchango endelevu.
 
Katika yote uliyoongea nashukuru ila chonde chonde NITAJIE HIZO SEHEMU MIE!!!! HUENDA NAZIJUA ILA LABDA WAJUA ZAIDI!!!! TUFUNDISHANE REAL THING SIO THEORY ZA JUU JUU!!! NASUBIRIA HIZO SEHEMU KABLA SIJALALA!!!

NOTE: KESHO CHURCH HERI UZITAJE USIKU HUU TUMAKIZIE NAJISI KABISAA!
 
Katika yote uliyoongea nashukuru ila chonde chonde NITAJIE HIZO SEHEMU MIE!!!! HUENDA NAZIJUA ILA LABDA WAJUA ZAIDI!!!! TUFUNDISHANE REAL THING SIO THEORY ZA JUU JUU!!! NASUBIRIA HIZO SEHEMU KABLA SIJALALA!!!

NOTE: KESHO CHURCH HERI UZITAJE USIKU HUU TUMAKIZIE NAJISI KABISAA!
Kwa Mwanaume: 1.Uume(kichwa) 2.Kifua 3.Masikio 4.Midomo(lips) 5.Mgongo
Kwa Mwanamke: 1.Matiti(chuchu) 2.Nywele 3.Midomo(lips) 4.Masikio 5.Mgongo 6.Kitovu 7.Mapaja 8.Shingo(Nyuma) 9.Nyuma ya Magoti 10.Kisimi(clitoris) 11.G-Spot 12. Vidole & Mikono.

NOTE:Kila mtu anasehemu yake yenye hisia zaidi na kuna utaalamu jinsi ya kushika na kupapasana sio kumshika chuchu mwanamke kama unakamua maziwa ya ng'ombe.
 
Uwazi , uaminifu, kujaliana na style ndio mapenzi hasaaaa.
4 sure, ili kupata Mapenzi ya dhati inakulazimu uwe Mzingatiaji & Makini sana katika kutekeleza wajibu wako juu ya kulitumukia Penzi.
 
Back
Top Bottom