Mambo 5 ya police Temeke kujiridhisha kabla ya kuzindua kituo cha police Charambe

dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
11,545
22,050
Habari!

Naomba kutoa rai kwa jeshi la police, mkoa wa kipolice TEMEKE, Katika maboresho ya kituo kidogo cha police charambe, yaliyofanywa na SIMBA OIL PETROL STATION.

Kabla ya yote naomba kutoa pongezi kwa SIMBA OIL PETROL STATION kwa kuguswa na hali duni ya miundombinu iliyopo katika kituo kidogo chenye chenye jengo bovu kabisa na kuamua kuwajengea kituo kipya kwa pembeni mbele ya sheli yake mpya ya mafuta ambamo pia kutakuwa nahuduma ya supermarket.

Lakini pamoja na pongezi hizo; Police nawasihi wajiridhishe na majibu ya maswali haya kabla hawajakipokea na kukizindua kituo hicho kwa matumizi rasmi ya jeshi la police Tanzania.

a. Eneo walilopo kwa sasa je linamilikiwa na nani? Kwa mkataba gani? Je jengo hilo linakidhi viwango vya kiusalama?

b. Endapo watahamia katika jengo jipya walilojengewa. Je wamejipanga kuwa walinzi wa ile Petrol station kwa mda wote?

c. Je Police wanatambua kuwa kitendo cha kukubali kukaa pale itabidi wawe makini zaidi kiulinzi kuanzia Kujirinda wenyewe na kuirinda petrol station dhidi ya majambazi? Kwakuwa Endapo kituo kitaonekana kuwa kikwazo kwa majambazi,huenda majambazi wanaweza kushambulia kituo kwanza kabla ya kuiba pale petrol station.

d. Kama jibu ni ndiyo, na kwa mujibu wa hadhi ya kituo kumiriki silaha, je kituo kile kinauwezo wa kulaza/kuwa na ghala la silaha? Ama italazimika kuwa na Mobile patrol itakayo kuwa na silaha kurinda kituo kile kila siku. Je wapo tayali kwa hilo?

e. Je wapo tayali kwa lawama endapo, Ile petrol station siku moja ikavamiwa na wao wakiwa palepale?

CC; Naomba RPC/OCD/OC-CID/OCS etc TEMEKE wajiridhishe na haya kwanza kabla ya kupokea msaada wa jengo hilo zuri na lenye hadhi lililojengwa pembeni mwa petrol station ili kuhamisha kituo duni kilichopo mbele ya sheli kwa sasa kitakachobomolewa kupisha njia ya kuingia na kutoka sheli. Endapo maswali hayo yatakuwa na majibu basi ni vyema askari wetu wakafanyiwa wepesi wahamie mara moja kwenye jengo hilo jipya lililotayali ili waachane na adha wanayoipata hivi sasa kwenye jengo lisilokidhi hadhi ya jeshi la police.Ahsante
 
Back
Top Bottom