Mambo 5 usiyoyajua kuhusu China | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mambo 5 usiyoyajua kuhusu China

Discussion in 'International Forum' started by ugaibuni, Jan 8, 2012.

 1. u

  ugaibuni Member

  #1
  Jan 8, 2012
  Joined: Jan 5, 2012
  Messages: 15
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kwa miaka kadhaa nimekuwa nikisikia neno China China, hili linamaanisha kila kitu, siku za hivi karibuni neno hili limehusishwa sana na ufake,kutodumu nk. Binafsi nikiwa fans wa made in China, iwe kwa kukosa njia nyingine au urahisi ninaweza kusema machache ambayo nadhani yatakuwa na msaada kwa wengine. Nikiwa Mtanzania niliyeishi China kwa miaka zaidi ya sita, ninapenda kushare nawe mambo machache ambayo wafanyabiashara hawawezi kukuambia kuhusu Made In China.
  [​IMG]
  [h=2]1. Kuna Vitu China ni Ghali kuliko hata Tanzania[/h]Unaweza kusema kivipi, ila ni kweli, ukiwa Uchina na unataka kupata kitu chenye ubora mzuri, ni dhahiri unatakiwa kulipia zaidi. Binafsi nimekuwa nikipokea simu nyingi mno toka nyumbani wakitaka kunitumia pesa niwanunulia komputa nk. Ukienda sokoni kompyuta ya kawaida ambayo ni bora inaanzia yuan 2000, tena hiyo ni ile ya kiwango cha chiiini kabisa, ila ukiipeleka kwenye dola ni kama mia tatu kadhaa, ukijumlisha na utumaji mpaka inafika nyumbani ni kama dola mia tatu na nusu au mia nne. Hapo ndio unapata kompyuta ya kawaida mno kitu ambacho kwa mtanzania wa kawaida lazima aone ghali kwani akienda sokoni anaona DELL kibao kwa laki tanotano.

  [​IMG]
  [h=2]2. China kuna bei tatu[/h] Kama umewahi kufika Uchina ni dhahiri utakubaliana nami, ukienda dukani unaulizwa unataka ipi, Hao(nzuri), Yiban(Ya kawaida) Shuihuo(Dump aka fake). Kwenye kila kundi ubora ni tofauti,ingawa kwa macho zote zinaonekana sawa. Pindi ununuapo ni lazima uhakikishe unapata kulingana na mapenzi yako. Hongera kwa wafanyabiashara WENGI wa Kichina ni kuwa, atakuambia. Hii ni nzuri na hii ni mbaya. Pia hata kwenye hiyo nzuri nayo kuna makundi yake humo ndani.hehe. Hivyo kabla hujanunua ni lazima ujue nini unataka na lazima muelewani na muuzaji.

  [h=2]3.Kitu cha 100Yuan si cha 80Yuan.[/h] Kwa wale waliowahi kukutana na Watanzania au wageni kadhaa walioishi Uchina kwa miaka mingi watakubaliana nami, jinsi muda uliokaa China unavyooongezeka ndivyo uwezo na ari ya kupatana bei inavyokwisha. Binafsi ni mara chache mno ukaniona ninapatana bei. Hii ni kwa sababu tayari wanafahamu hili. Kuna siku niliambatana na dada mmoja kununua simu, alipofika kule simu aliyopewa ilikuwa ni ya mia nane, akazidi kupatana (pianyipianyipianyi) basi mwisho yule mchina akakubali, yule dada akasema nachukua hii, mchina aliwaka kama kawekwa petroli. Akibwabwaja "haiwezekani,hii ni ghali nk) mwisho ikabidi mdadaa aongeze pesa.

  [h=2]4. Kuna maduka yanayojulikana kwa ufeki na ubora.[/h] Kila sehemu wana mila na tamaduni zao, ukiwa China, kama unataka kupata kitu chenye hadhi na ubora mzuri basi unashauriwa ukanunue kwenye maduka makubwa, kwa mfano unataka kununua TV ya nyumbani basi nenda kwenye maduka kama ya Sunning, Gomao,carrefour nk kwani mengi ya maduka haya yana mkataba wa ubora na bei na serikali. Kuna kipindi Carrefour walipandisha bei kiholela kwa baadhi ya vifaa vyao, walipigwa faini na ikawacost mno. Binafsi mwaka jana nilinunua simu ya mkononi "Nokia", wiki iliyopita kilitokea kitendo kilichonisukuma kuandika makala hii.
  Nikiwa barabarani kwenye pikipiki simu yangu ilidondoka, nikasikia mchina akiita "simu imedondoka" nikasimama na kuangalia kumbe ni simu yangu. Kwa bahati mbaya ilikuwa katikati ya barabara hivyo sikuwa na cha kufanya zaidi ya kuiangalia ikikanyagwa na basi la abiria, baada ya lile basi kupita taa nyekundu ikawaka na nikakimbia kuangalia masalio ya simu, nikaona kioo kimevunjika, nilipoishika nikaona ukiondoa kioo hakuna kingine. Niakajaribu kupiga simu ikawa inaita bila matatizo. Kesho yake nikaipeleka kwa wenyewe Nokia, wakaiangalia wakasema ukiondoa kioo hakuna tatizo. Ni kweli nimebadirisha kioo na sasa inadunda bila wasi.

  [​IMG]
  [h=2]5. Nokia si sawa na NokIa, pia Samsung si Sunsung.[/h] NImekuwa nikisikia na kuona watu wengi wa nyumbani wakitumia simu wanazoziita Nokia ya Mchina, au Sumsung ya Mchina, hakuna kitu kama hicho huku. Wengi wanaotengeneza hizo simu ni viwanda vidogovidogo ambazo ubora wake ni hafifu mno. Wengi wamekuwa wakiongopewa kuwa inaitwa hivyo kwakuwa imetengenezwa China. Wafanyabiashara wengi wamekuwa wakijilimbikizia faida kwa kununua simu hizo kwa bei ya chee halafu kuwaongopea Watanzania. Chukulia mfano simu ya Nokia E72i inauzwa kuanzia 1800 hadi 2000yuan. Ila kwa zile mbofumbofu aka NoCia(NokIa) inauzwa kwa 500Yuan. Simu hizo sio tu hazina ubora bali pia ni hatari kwa afya yako kwani wakati wowote inaweza kukulipukia, inakulisha mionzi ya ajabuajabu nk.
   
 2. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #2
  Jan 8, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,466
  Trophy Points: 280
  asante..............
   
 3. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #3
  Jan 8, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,466
  Trophy Points: 280
  umesahau kuwaonya ndugu zako
  adhabu za wanaopatikana na madawa ya kulevya
  pamoja na mfumo wa kimahakama wa china.....
   
 4. u

  ugaibuni Member

  #4
  Jan 8, 2012
  Joined: Jan 5, 2012
  Messages: 15
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mkuu stay tuned, tutakuwa tunachambua moja baada la lingine kuhusu maisha na mambo ya Uchinani kwani kwa siku za karibuni namba ya Watanzania wanaohudhuria China imekuwa kubwa mno, kuanzia wanafunzi,wafanyabiashara nk.

  Kwa msaada wa Ughaibuni.com tutakuwa tunakuletea mengi. Kufuatilia mambo yanayoendelea Uchinani nenda Hapa au kama una swali la moja kwa moja unaweza Uliza kwenye kipengele cha China Hapa
   
 5. kamikaze

  kamikaze JF-Expert Member

  #5
  Jan 8, 2012
  Joined: Jan 25, 2011
  Messages: 202
  Likes Received: 138
  Trophy Points: 60
  Mkuu ukweli ni kwamba china kuna vitu vitu ghali kuliko hata ulaya na kuna vitu vya bei rahisi kuliko Tanzani, ukienda dukani sema unataka kununua kitu cha shilingi ngapi maana kwa mfano saa unaweza kupata ya shilingi za kitanzania 5000/= mpaka milioni 100 nazungumzia saa ya mkononi
   
 6. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #6
  Jan 8, 2012
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  谢谢你对了现在知道了
   
 7. trachomatis

  trachomatis JF-Expert Member

  #7
  Jan 9, 2012
  Joined: Jun 7, 2011
  Messages: 3,653
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 145
  nimeipenda elimu hii sana kwani imenifanikisha kuweza kutofautisha kati ya bidhaa za ''Ki-China'',na za ''Ki-Chinese''
   
 8. u

  utantambua JF-Expert Member

  #8
  Jan 9, 2012
  Joined: Aug 1, 2011
  Messages: 1,373
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Pamoja na maelezo mazuri ya utetezi wa MLeta thread kwa China Swali langu ni kwanini serikali ya china inaonekana ku-condone hizo bidhaa feki ambazo wasema zinatengenezwa na viwanda vidogovidogo? Wadhani hili kwa ulaya lingevumiliwa/kufumbiwa macho? Yaonekana ni kitu ambacho kiko institutionalized kabisa ati wataka bidhaa ya ubora, ya wastani ama mbaya? Jamani China mtatuua
   
 9. sblandes

  sblandes JF-Expert Member

  #9
  Jan 9, 2012
  Joined: Apr 25, 2010
  Messages: 2,457
  Likes Received: 788
  Trophy Points: 280
  China ajiona mjanja wa kuwa na matabaka ya vitu,lakini imeishaanza kumgharimu kwani watu wa ASIA hasa south east asia hawapendezwi na magreen ya China wanamuita kuwa anakula bila kunawa hivyo huvisusia vitu vya kichina simply made in china.
   
 10. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #10
  Jan 9, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  east asia wamethubutu!
   
 11. mpinga shetani

  mpinga shetani JF-Expert Member

  #11
  Jan 9, 2012
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 3,268
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  Samaki mmoja akioza wote wameoza China is synonimous with fake. period
   
 12. N

  Nkwama welding Member

  #12
  Jan 10, 2012
  Joined: Oct 2, 2011
  Messages: 61
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Vipi kuhusu madawa ya kutibu binadamu nayo wanauza nzuri, kawaida na fake na serikali yao inaruhusu?
   
Loading...