Asanteni wote mlioamua kusema hapana na mengine mliyoongeza.
Kwa wale ambao hawajaelewa hii; SEMA HAPANA KWA TABIA YA KUPOTEZA MUDA KWENYE MTANDAO iko wazi kabisa wakuu. Kuna kutumia mtandao kwa faida, kama tunavyofanya hapa na kuna kutukia mitandao kwa kupoteza muda.
Kwa mfano mtu kila kuda anachungulia facebook nini kinaendelea, instagram nani kafanya kweli, twitter nani katweet nini hapo bado ana wasap yenye magroup kama kumi hivi, group la siasa, la michezo, la vichekesho, la shule ya msingi, la sekondari, la kijijini mlikotoka na kadhalika, mtu huyu anaweza kufanya kitu cha maana kwenye siku yake kweli?