jmdume45
Senior Member
- Jun 10, 2016
- 162
- 67
MAMBO 10 YA KUZINGATIA ILI KUPUNGUZA UZITO WAKO KWA URAHISI NA HARAKA ZAIDI
- Pata kifungua kinywa chenye protein kwa wingi. Kula kifungua kinywa chenye protini kwa wingi imeonekana kupunguza ulaji wa calorie nyingi kwa siku .
- Kuepuka vinywaji vyenye sukari na juisi ya matunda.
- Kunywa maji nusu saa kabla ya milo. Utafiti unaonyesha kwamba ukinywa maji nusu saa kabla ya milo kuna uwezekano wa kupunguza kasi ya kuongezeka uziti kwa 44% katika kipindi cha miezi 3
- Kuchagua vyakura rafiki vitakavyo kuasidia kupunguza uzito . Baadhi ya vyakula ni muhimu sana kwa kupoteza mafuta kama vile , mboga za kijani,Viazi vya kuchemshwa, Maharage na kunde , avocados, Mafuta ya nazi. nk
- Kula nyuzi mumunyifu (dietary fiber). utafiti unaonyesha kwamba nyuzi mumunyifu inaweza kupunguza mafuta, hasa katika eneo tumbo.
- Kunywa kahawa au chai. Kama wewe ni myaji mzuri wa kahawa au chai itakusaidia kuongeza metabolisim ya mwili kwa 3-11%.
- Kula zaidi vyakula visivyo koborewa.
- Kula taratibu hufanya kujisikia umeshiba zaidi , na inaongeza homoni za kupunguza uzito .
- Kutumia sahani ndogo. utafiti unaonyesha kwamba watu hula kidogo wakati wakitumia sahani ndogo.
- Kupata usingizi mzuri, kulala vizuri, kila usiku. kutopata usingizi mzuri usiku ni moja ya sababu kubwa zinazo pelekeaongezeko la uzito, hivyo kulala vizuri ni muhimu .