Mambo 10 usiyoyajua kuhusu Tanzania

Mambo 10 usiyoyajua kuhusu Tanzania

kabwinyola

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2016
Posts
560
Reaction score
682
Kuna watu wanaweza kuwa wanaish Tanzania lakin kuna mambo yanayofanyika yanashangaza wengi wanaochungulia.

1. Ndo nchi pekee ambayo mwanachama wa upinzani anashangilia serikali kukwama na mapato kushuka hajui akiwa kwenye matatizo ya kutaka huduma atakwama hata yeye pia,

2. Nchi pekee dunian ambayo mpinzani akibambikiziwa kesi mwananchi wa chama tawala anashangilia , hajui IPO siku naye anaweza kuwa mpinzani , mfano lowassa alitoka Ccm akaenda upinzani

3. Ndo nchi pekee ambayo wanasiasa ni waongo na wasahaulifu kupita kiasi , na wanabadilisha maneno kila kukicha,

4.Ndo nchi pekee ambayo MTU anaweza kuchagufuliwa kwa miaka zaidi ya nane kuwa fisadi lakin pesa zikamfanya malaika ndani ya Siku moja,

5. Ndo nchi pekee mwanafunzi wa form four aliyepata division four na zero anaenda chuo kukuu kisa ni mtoto wa mkubwa , na wenye sifa wakiomba haki yao wanapigwa mabomu,

6. Ndo nchi pekee ambaye askari wake analalamika akiwa nyumbani kwake kuhusu mwanaye MKOPO wa chuo kuchelewa na kumwambia akadai haki yake lakin anawaza jinsi ya kutekeleza agizo LA kupiga mabomu watoto wa wengine wanaoandamana kudai haki kama mwanae

7. Ndo nchi pekee ambayo inaongozwa na misingi ya MTU ambaye ashatangulia mbele ya haki,

8. Ndo nchi pekee ambaye inamiliki maliasili physically, lakin economically wananufaika wengine, kama mlima Kilimanjaro kutumiwa na Kenya

9. Ndo nchi pekee ambayo vijana wanaojiita wapinzani hulalamika nitandaoni badala ya kuchukua hatua, wanaonekana kuwa na hoja nzuri na kusema tarehe moja kitanuka wakati hata majina wanayotumia ni fake na hawajuani

10. Tanzania ni nchi pekee ambayo MTU anatetewa sana na kuonekana hana kosa hata kama kabaka au kahujumu uchumi, kisa anatokea kanda fulan

NOTE THAT Ndo nchi pekee ambaye mwenyekiti wa tume ya uchaguzi wa sehem yake (zenji) analindwa kuliko rais wa marekani

Mwaweza ongezea mengine
 
Ndio nchi pekee ambayo African language(Kiswahili) hutumika kufundishia elimu ya msingi halafu ghafla hutumia kiingereza kufundishia elimu ya sekondari na vyuo. Ndo maana tunakuwa na PhD holder hawezi kuongea Kiingereza, na je hakukariri aliwezaje kujifunza kwa lugha asiyoielewa!
 
1.Nchi peke ambayo sheria zinawekwa kuwa zuia wapinzani huku sheria hiyo hiyo papo kwa hapo ikivunjwa na mkuu mwenyewe.

2. Nchi pekee ambayo wakili wa jamuhuri ana muamuru wakili binafsi asimtetee mteja wake eti kisa jamuhuru ina muhitaji wakili huyo awe shahidi wao. Ni Tanzania pekee
 
ni nchi pekee ambayo chama cha upinzani kinadai demokrasia wakat huo huo hivyo vwama vikiwa havina demokrasia.
 
Back
Top Bottom