Mambo 10 niliyoyaona Yanga Vs Al Hilal jana

Mwishokambi

JF-Expert Member
Nov 23, 2020
304
1,162
1. Mchezo ulikuwa mzuri sana na Yanga walitaka kumaliza mchezo mapema lakini game approach iliwashinda.

2.Yanga wamekamilika kwenye idara ya goalkeeping otherwise Al Hilal wangefuzu hapa hapa kwa Tanzania.

3. Mabeki wa Yanga wanafanya sana makosa, Bangala, Job, Kibwana na Djuma Shaaban hawakuwa na maelewano mazuri, walikuwa wanakatika sana.

4. Khalid Aucho na Feisal Salum hawakuwa mchezoni, Feitoto hakupiga hata shuti moja jana na alionekana sana kucheza chini tofauti na alivyo sasa ambapo anacheza inside 10. Kama ulikuwa ukicheza kiungo wa kati then ukawa unacheza inside 10, mara nyingi naona ile calibre ya kucheza kiungo wa kati inapotea, mfano Yussuf macho, Gagarino walipoacha kucheza namba 8 na kuhamia namba 10, namba 8 ziliwashinda. Hicho kilitokea kwa feitoto jana.

5. Al Hila wazuri lakini sio timu ya kuisumbua Yanga, ina wachezaji wa kawaida sana, basi tu Yanga walijichanganya wenyewe.

6. Morrison ni mtu hasa, mimi nina uhakika Simba walicheza mchezo mchafu kumpeleka Yanga under the pretext kuwa hana nidhamu. Ndiye aliyeonyesha uwezo mkubwa dimbani jana.

7. Fiston Mayele ni mtu hatari sana, kama Nabi atabadilisha game approach ugenini, yanga wanaweza kufanya maajabu kwani jamaa hawezi kukosa nafasi 3 zote, lazima moja ateteme

8. Mashabiki wamehamasika sana, rai yangu kwao kama huna subira na huamini kama yanga anaweza kutoa sare au kufungwa, achana na mpira au shabikia kule kwa Karim Mandonga. Mpira ni mchezo wa makosa.

9. Tuisila Kisinda anahitaji muda, hata chama aliporudi kutoka Berkane alionekana amekwisha, Tuisila anahitaji mechi kama 5 hivi arudi kwenye ubora wake.

10. Simba na Yanga zinahitajiana sana ili kuleta heshima kimataifa, Yanga wamepata sare kwa sababu Ibenge aliwahi kuambiwa siri za Simba, Leo amezitumia kuikabili Yanga na amefanikiwa. Nawapa siri mwarabu alipoambiwa fitina imefanyika wafe mengi Taifa, wakapiga kitabu cha haja, paka saba walikufa kwa kitabu tu. Mnaweza ona naleta utani but that is the fact. Tuache usaliti.

11. Nabi hana mbinu, niliwahi kulisema hili na nitalisema, anabebwa na mambo mengi ya mpira wa bongo, ataondoshwa na Al Hilal, Yanga watapelekwa kwenye Confederation nako atakufa pia. Sijaona ufundi wowote pale uwanjani jana.

12. Aziz Ki, ni mchezaji mzuri lakini namna kocha anavyowapanga dimbani ili kuwafurahisha mashabiki ndio maana anaonekana wa kawaida.

13. Yanga haina cha kuwahofia Al Hilal, mambo ya kuwa kwao wana fitina cjui nini sio kweli, St George wameenda pale wamefungwa bao dakika za mwisho, kama wangekuwa serious na kupata bao moja tu, Al Hilal walikuwa wamepoteana.

14. Michuano ya CAF ni sayansi, Malengo, mikakati, mbinu, uzoefu na mipango, Yanga hilo hawana.
 
Yanga jana walikuwa wanapigwa si chini ya goal tatu. Yaani washukuru sana kupigwa kimoja tu.
 
Tatizo lipo kwa kibwana na farid wale hawana uwezo wa kuchezo mechi za kikubwa.
Pia sabu ya mapema kwa khaleed ingefanyika

Yanga Out jana
Azam out jana
Simba Out leo.
 
Uchafuuu huu
 
Kibwana Shomari hana uwezo wa kucheza Cafe.

Yanga imsajili Msonjo au Kenedi kwa ajili ya namba tatu. Bangala siyo pure defender wamsajili mtu wakati kusaidiana na Job.

Aziz anahitaji kucheza free zaidi hivyo anahitajika mtu kazi namba sita ili pale kati pasiwe na ombwe.

Yote kwa yote mechi yyte ya caf Kibwana asikae hata benchi hana uwezo wwte ni Bora ya Onyango mara 20 kuliko kibwana. Hana mikimbio, Hana umakini, Hana target, yeye amebaki na ufupi kama dumu la maji...
 
dahh eti kama dumu la maji we jamaa
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom