kindikwili
JF-Expert Member
- Oct 5, 2016
- 1,862
- 2,876
North Korea ni nchi inayochafuliwa sana na propaganda za Marekani kupitia media zao. Ila ki ukweli yapo mambo mazuri sana huko NK ambayo hayapatikani katika nchi nyingi hapa duniani .Yafuatayo ni mambo hayo kumi unayopaswa kuyajua kuhusu NK
1. Kiwango kidogo cha uhalifu (Low crime rate)
Nchi ya korea kaskazini kiwango cha uhalifu ni mdogo sana ukilinganisha na nchi nyingi duniani. Korea kaskazini hata mwanamke anaweza kutembea usiku wa saa nane akiwa peke yake mtaani na mtu asimbugudhi. NK hakuna watu wanaojinyonga na ina zero suicide cases kwa mwaka hii ni kwasababu wananchi walio wengi wameridhika na aina ya maisha wanayoyaishi.
2.NK ni moja ya nchi yenye jeshi kubwa duniani
Unapolinganisha uwiano wa wanajeshi na wananchi basi NK wana kiwango kizuri sana, karibia watu 1.2M ni wanajeshi huko NK na wanatumia karibia $10b kwa mwaka katika miradi ya kijeshi
3.Mandhari mzuri (Beautiful land scape)
NK ina madhari nzuri sana za asili zinazovutia sana japo kiwango cha watalii wanaotembelea hiyo nchi ni ndogo sana kutokana na uhasama kati yake na America na washirika wake wa ulaya na vikwazo wanavyopambana navyo.
4. Watu wa NK ni wakarimu na wenye mioyo mizuri sana (None guilty and good hearted people) Huwezi kuwalinganisha na watu wa nchi nyingi hapa duniani kwa ukarimu, ni watu wenye nidhamu na wana huruma sana.
5. NK wanatoa makazi na matibabu bure (Free housing and medical care)
Katika nchi chache duniani zinazotoa huduma ya makazi na huduma za afya bure kwa wananchi wake NK ni moja wapo.
6. Utamaduni uliotunzwa kisawasawa (well preserved culture)
Kutokana na kutokuingiliana sana na watu wa duniani nyingine, ukosefu wa TV za nje na huduma za mitandao ya nje , nchi ya NK imeweza kutunza utamaduni wake kwa karne nyingi bila kupotea. Yaani wamezidi hadi wamasai kwa kutunza utamaduni wao
7.Maliasili (Natural resources)
NK ina utajiri wa maliasili nyingi sana , kuna madini ya aina nyingi sana NK kama madini ya chuma, makaa ya mawe na magnezium. Nchi ya china ndiyo wawekezaji wakubwa katika sekta hizi japo si kwa kiwango kikubwa.
8. Uchafuzi mdogo wa mazingira (Less pollution)
NK kiwango cha uchafuzi wa mazingira ni mdogo sana ukilinganisha na nchi nyingine duniani. Hii ni kutokana na uchache wa viwanda na magari, ukiwa NK unaweza ukadhani uko Edeni kutokana na hali yake ya hewa.
9. Kiwangi kidogo sana cha matumizi ya umeme (very low electricity consumption)
Nchi hii ya NK wanatumia kiasi kidogo sana cha umeme, kutokana na uhaba wa viwanda
10. Elimu bure na kiwango kikubwa cha watu wenye elimu (Free education and high literacy rate). Elimu katika nchi ya korea kaskazini ni bure kwa maana ya bure na hupatikana kwa wote. Ni bure kutoka primary hadi vyuo vikuu. Kiwango cha watu wenye elimu (literacy rate) kwa NK ni sawa na United States na United Kingdoms.
BONUS
Rais wa NK ndiye rais kwasasa duniani mwenye physical fitness na mazoezi mazito kuliko Rais yeyote. Akiwa na mwili ulioshiba kiasi anaweza kufanya mazoezi makubwa sawa na wanajeshi wa nchi nyingi. Ni mtu anayefanya mazoezi mzito sana na mara zote yuko fiti kiasi kwamba ukimuweka na Trump wapambane kwa ngumi anaweza asimalize naye hata dk 10 kwenye ulingo, kwa kifupi atakuwa tayari kashamsindikiza ahera.