Mamba huyu mamba gani, mbona hawezi kung'ata?

Mawele

Member
Jul 25, 2023
30
116
Ni kubwa sana kiumbo, ikiwa kwenye hadhira,
Ni Mamba kama wa Mombo, Sema ye hana madhara,
Yakichambuliwa mambo, yatakutia hasira,
Mamba huyu mamba gani, mbona hawezi kung'ata?

Hukaa kimya majini, hutoka mwingine mwaka.
Huletwa vingi vitini, kusoma walo potoka,
Vinasomwa kwa makini, imara bila mashaka,
Mamba huyu mamba gani, mbona hawezi kung'ata?

Huishia tu kufoka, kisha huyo huondoka,
Kama mbwa hubweka, kutaja vyao vichaka,
Ila hana mamlaka, kuwaadhibu vibaka,
Mamba huyu mamba gani, mbona hawezi kung'ata?

Wako wapi wahusika, waliopewa dhamana,
Wasotaka kuwashika, walotajwa mwaka jana,
Au nao wahusika, asa tusemaje tena?
Mamba huyu mamba gani, mbona hawezi kung'ata?

Sioni haja kuwepo, bora tukwepe gharama,
Ni kufukuza upepo, siioni yake dhima.
Kuwajibika kuwepo, irudi yake heshima,
Walishayatoa meno, hawahofii kung'atwa!
 
CAG kamaliza kazi yake, ameshaonyesha wapi panavuja, mwenye jukumu la kuziba mianya hiyo kwa mujibu wa katiba ni Bunge,lakini jee kwa hali halisi ya siasa za nchi yetu tunalo bunge la kuweza kuiwajibisha serikali kwa niaba ya sisi wananchi? Ripoti hizi za CAG zitaendelea kuwa sawa na kumpigia mbuzi gitaa tu.

Serikali imeshindwa kuwawajibisha wezi wa mali ya umma na bunge limeshindwa kuiwajijisha serikali badala yake limekuwa kwaya ya kuimba mapambio ya kumsifu na kumuabudu Rais aliyepo madarakani. Kuwa na bunge la chama kimoja ni hasara kwa umma wa watanzania.

Japo wapo kajamba nani wengi huko CCM walifurahia wizi wa kura uliopelekea tuwe na bunge la hovyo kabisa kuwahi kutokea wakidhani wanawakomoa wapinzani lakini wote tumevuna mabua. Fedha zinazofujwa na watawala na mawakala wao ni kodi zetu woooote bila kubagua vyama.
 
Huishia tu kufoka, kisha huyo huondoka,
Kama mbwa hubweka, kutaja vyao vichaka,
Ila hana mamlaka, kuwaadhibu vibaka,
Mamba huyu mamba gani, mbona hawezi kung'ata?
Hapo ndio ulipo maliza mambo yote.

Mamba anafura,lakini hana uthubutu. Hawezi kamata muogeleaji wala mkimbia riadha. Wale waliopewa meno yakung'ata wazamiaji majini ilishasemekana nidhaifu na vibogoyo.

Mamba anagarimu kumfuga maana hata akamate mwizi wa samaki mfugaji hajishuhulishi
 
Taasisi zingine ni furushi la mizigo mizito isiyo na faida kwetu walipa kodi wa nchi hii.

Yaani ni ujinga ujinga tu na upuuzi basi!
 
Back
Top Bottom