Mama wa rafiki yangu alikuwa mchawi

Mama wa rafiki yangu alikuwa mchawi

BABA TUPAC

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2015
Posts
1,533
Reaction score
3,837
Wakuu,

Rafiki yangu huyu wa miaka mingi toka utotoni tulikuwa karibu sana japo watoto wengi walimtenga kwa kuwa kulikuwa na taarifa za chini kwa chini kuwa mama yake ni mchawi.

Miaka ikaenda sana, ikafika kipindi baba wa rafiki yangu akaanza kuugua mguu. Mguu huo aliwahi kupata ajali ya gari miaka kadhaa iliyopita, hivyo watu wakasema chuma alichowekewa mguuni labda hakikukaa vizuri hivyo kinamsumbua. Lakini akawa anazidi tu kuumwa, akalazwa hospitali muda kidogo huku anaumwa sana lakini kila wakipima hamna ugonjwa mwingine zaidi ya mguu.

Siku moja ndugu mke wa huyu mzee alikuwa ametoka hospitali kidogo hivyo ndugu wa mzee katika maongezi ongezi pale wakasema amelala sana upande mmoja tumgeuze alalie upande mwingine. Katika kumgeuza yule mzee alikuwa anapiga makelele sana kwamba anaumia alipoulizwa kwanini akasema ana kidonda mgongoni ikabidi wafunue kumuona, walichokuta hawakuamini. Alikuwa na kidonda kikubwa ambacho kinaonyeshwa nyama ya imekatwa kabisa mgongoni karibu na kiuno

Mama aliporudi akaulizwa mumeo kumbe ana kidonda kikubwa mgongoni kwanini hutuambii wenzio? Akasema daktari alisema cha kawaida tu, kimetokana na kulala sana. Jambo ambalo halikuwaingia kabisa akilini Wasukuma wale

Inaonekana hicho kitu kiliwapa maswali sana ukizingatia ndugu yao anaumwa mguu tu lakini ikafika hatua haongei hata kuongea lakini hana ugonjwa mwingine. Basi wale ndugu ikabidi waende kwa waganga wa kienyeji, walienda kwa waganga watatu tofauti na jibu walilopewa ni kwamba mmechelewa kuja, ndugu yenu ameshaliwa nyama hawezi kupona tena. Huyo mwanamke ni mshirikina aliambiwa imefika zam yake kutoa nyama achague kutoa kati ya mtoto wa kwanza ambaye alikuwa chuo kikuu mlimani au mme wake kipindi chote hicho alishindwa kuchagua na alikuwa hataki kabisa wenzie wakamjia juu kwamba yeye wakati anakula nyama za watoto wa wenzie alijua haiumi? Sasa zamu yake na yeye

Kwahyo mpaka mwisho mama hakuchagua, hivyo wachawi wenzie wakajichagulia mme wake.

Ndugu waliporudi kutoka huko walikoenda ilikuwa mtiti, mtaa haukukalika wala kulalika wakitaka kueleza kwanini amekula nyama ya ndugu yao. Haikuisha hata wiki yule mzee alifariki

Haya mambo yasikie tu kwa jirani lakini omba yasikukute
 
mmmmmmh noma sana nawachukiasana wachawi wanarudisha maendeleo ya mtu nyuma
 
borq nikae na mwizi chumba kimoja kuliko kuishi na mchawi ata kama anakaa mtaa wa 9
 
Mwenyezi mungu atunusuru, hata sijui hawa viumbe wanapata faida gani kwenye fani hii..
 
Aise watumia simu, labda laptop, wa Google na kuwepo kwenye social media.
BADO UNAAMINI NGUVU ZA GIZA NA IMANI POTOFU?!
Umaskini na ujinga hautakutoka kamwe!
 
Back
Top Bottom