Phillipo Bukililo
JF-Expert Member
- Dec 29, 2015
- 18,487
- 13,612
Nimeiona habari moja inamhusu mama moja wa kule Tarime, anaitwa Sophia Manguye. Jeshi la polisi mkoani Mara limemzawadia shilingi laki tano kwa ushujaa wake wa kuweza kupambana na jambazi aliyekuwa na bunduki aina ya SMG, na akaweza kumzidi nguvu na kumnyang'anya. Huyu mama anastahili kupewa nishani na rais, tena katika siku ya mashujaa wa nchi.
Baada ya kuisoma hii habari nikakumbuka miaka ya 90 nikiwa kule Ulaya Mashariki, mimi na watanzania wenzangu tuliokuwa tunasoma kule tulikuwa tunashangazwa kuwaona makonda na madereva wa treni za umeme za mijini, wakiwa ni kina mama wa kirusi. Tukaambiwa kuwa baada vita kuu ya pili kumalizika, wanaume wengi walikuwa wamefia vitani, hivyo kinamama wakazichukua kazi zote zilizokuwa zinafanywa na kinababa.
Niliporudi nchini mwanzoni mwa miaka ya 2000, nikakutana na makonda wasichana, yaani jamii nzima ilikuwa ikiwatazama kama vile wanajidhalilisha, kuliko na aina fulani ya dharau na kejeli katika sura za wanaume wengi waliokuwa wakipanda mabasi ambayo makondakta ni wasichana. Lakini naona taratibu hii hali ya wanawake ambao ni makondakta kudharaulika inaanza kutoweka miongoni mwa watanzania.
Yote kwa yote Mama Sophia Manguye amefanya jambo ambalo wanaume wengi hawana uthubutu wa kulifanya. Kuna wanaume ambao wakiona panya anatoka ndani ya kabati, wanatimua mbio mpaka barabarani!, hawa hawawezi kujaribu kumnyang'anya jambazi bunduki, tena akiwa amevamia sehemu kwa ajili ya kufanya uharamia. Kinamama wanaweza, Mama Manguye amethibitisha ukweli huo.