Mama Salma Kikwete akizungumza Clouds Tv

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,410
Mke wa rais wa awamu ya nne Mama Salma Kikwete muda huu anazungumza na watangazaji wa Clouds media group. Hapa anaojiwa na Masoud Kipanya wa Power Breakfast (Clouds Fm), Baby Kabaye wa Clouds 360 (Clouds Tv) na Feza Kessy wa Hard drive (Choice FM).

Mada ni kuadhimisha siku ya Mama
================

Mama Salma- Hakuna mwanadamu lazima awaze siku zijazo atakuwa nani ukiwa katika balehe unakuwa na ndoto za kuwa mama wa namna gani na yeye anamshukuru mama yake Bint Paza bin Shariff na watu walijua mama yake anampenda.

Mama Salma- MImi nafanana sana na Baba yangu, lakini namshukuru mama yangu kwakua alikua ananipenda na sababu zake ziko ndani ya moyo wake. Mimi sikuwa mtoto mtundu ndio maana na hata sasa nikisamama kwenye majukwaa nakuwa najiami sana.

Mama Salma-
Nimesomea shule za msingi za Maida, Raha Leo Igula Mtwara, na Stadium. Nilichaguliwa na nikaenda secondary.

Mama Salma-
Malezi yapo pale pale na hayana tofauti ya zamani na sasa lakini mama yangu alinipenda kwa uadilifu wangu. Mtoto halelewi kwa fimbo ni kwa amelekezo.

Mama Salma- Sio sahihi kuwasukumizia watoto mzigo wa kwamba watoto wa siku hizi hawasikii, ni vema wazazi watumie muda wao vyema kuwalea vyema.

Mama Salma- Mama wa kambo sio mbaya wala mtoto wa kambo sio mbaya, yeye na Kikwete wanajumla ya watoto 9.


Mama Salma- Sio kila linalosemwa linauhalisia mengine hayana uhalisia, uhuru ndio unaoleta hayo na hali ya kuwa mzazi inabakia palepale. Ushauri ambazo sisi kama wazazi wakati mwingine tunajua watoto wetu wanasingiziwa na wanakuwa ni watu wanaotaka kukurudisha nyuma.

Mama Salma- Unapozaa unategemea watoto wako wawe watu wema lakini kinyume cha hayo mzazi au mlezi lazima usononeke, na ulimwengu wa sasa tofauti na zamani. Ndani ya mitandao yako mambo ya msingi unayoweza kuyachukua na kuyaacha na wakina mama wakae na watoto kwasababu ndio watoto wako hivyo ni suala la kushauri na kuwaelekeza.

Mama Salma- Wanawake wananyanyasika sana ndio maana kuna wanawake wanaolea watoto wao peke yao bila ya baba wa hao watoto. Lakini ni vyema watoto walelewe na wazazi wote. Lakini wanawake wawezeshwe kujua namna ya kudai haki zao.

Mama Salma-
 
Back
Top Bottom