Mama ni mama kwanini unamdharau?

Mama ni mama kwanini unamdharau?

ladyfurahia

JF-Expert Member
Joined
May 10, 2011
Posts
14,758
Reaction score
9,589
Habarini wadau wote


Natumai mko wazima buheri wa afya na mnaendelea na kazi zenu vyema na wale wanaosoma vilevile

Marafiki zangu imenibidi niongee nanyi haya machache ambayo nimeona mahali fulani kweli yamenifanya nitokwe na machozi na vilevile imenipelekea niweze kuwafunda VIJANA wa kisasa ambao wao kwao
HESHIMA NA ADABU imewapita kando wao wanajiona fahari sana kuwatusi, kuwadharau na kuwabedha
WAZAZI wao hususaniMAMA.

Sijui vijana wameingiliwa na kitu gani yaani vijana sasa wamekuwa kama helkopta wanajiona fahari sana
na wanajiona wana akili nyingi sana kuzidi wazazi wao hasa MAMA, wameshikwa na dharau ya nje nje
hawakumbuki kuwa MAMA alibeba mimba zao miezi 9 akakufyatua duniani ukaiona nchi leo hiii unamwona
takataka asiye na akili asiye na maendeleo.

Hata kama ana gari basi kama si mjuzi wa kiufundi gari linapo haribika basi unaleta dharau hivi kwanini mmekuwa hivyo vijana wenzangu?

Nimeongea haya kwani nimeona sana siku hzi adabu haipo kwa wakubwa na ukitaka kuwakemea na kuwaonya
hayo maneno utakayomwagiwa utaomba ardhi ipasuke udumbukie humo ndani yaani bora tuwafunde hapa
hapa kwani mnakoelekea si kuzuri.

Acheni kuiga mambo ya ughaibuni eti daddy atanifanya nini nami ni kidume kama ayeye nani amekufundisha maadili mabovu kiasi hicho? mbona mimi na daddy yangu watu8 namheshimu sana pamoja na mumy measkron nawaheshimu na kuwapenda vijana badilikeni Mungu hapendezwi na mtu
ambaye yu kinyume na wazazi wake.

Heshima ni kitu chema na ndicho kinakupatia baraka toka kwa Mungu kuipitia hao wazazi wako kwani Mungu alikuwa na makusudi ya kukufyatua wewe uwepo duniani na ni miungu wako hapa duniani.

Kijana hususani VIJANA WA KIUME tambueni hilo na muwe na staha, heshima kwa MAMA zenu hata kama ana elimu kuliko wewe ni mama huyo, hata kama ana sura nzito ni MAMA huyo hatakama si lolote wala chochote kwako hutapata MAMA mwingine kama huyo mmpende, mmheshimu na mtii
ndipo utaona baraka za Mungu zikikukufuata bestito.

Hili ni somo lenu ambalo nimeona niwafunde hasa vijana wakiume mmezidi sana mnadharau BADILIKENI



Wasalaamu.


Ladyf

CCC: Mamndenyi, Passion Lady, charminglady, Kasinde, Lady doctor, mwallu, Christine Denzi, Nivea, The secretary, Munkari, lara1, miss neddy, @Kwantwe, Zinduna, measkron, Kongosho kingasti, Heaven on Earth, sister, Paloma, lady gaga, Madame B, madame A, na marafiki zangu
wote niliowasahau kuwataja hapa karibuni tuongee jambo hili kwani halipendezi kabisa kuwepo kwa watoto wetu
 
Nani kama mama heshima kwa maama uliteseka siku ya kunitoa dunianii nikupe nini thamani uazime malezi yako siwezi kuyalipa


naimba tu mwite
Christian Bella
 
hakuna kama mama jamani na hao wanaowadharau mama zao ni kwa sababu wapo pamoja nao mpaka wakati huu,ngoja watoweke ndo wataujua umuhimu wa mama,unajua ukiwa na kitu sikuzote huoni umuhimu wake ila ngoja ukipoteze hicho kitu ndo utaiona.
 
Nampenda sana mama yangu.... I don't want even to imagine my life without her.....ila sometimes we quarrel....huwa najisikia vibaya sana kwa kweli
 
Nampenda sana mama yangu.... I don't want even to imagine my life without her.....ila sometimes we quarrel....huwa najisikia vibaya sana kwa kweli
Baba yako humpendi.... That's not fair.
 
Unazungumzia vijana wa rika gani? Coz hata a 35yrs old dude is considered kijana..!
 
Brain washed creatures. Mnaomdharau baba ambaye MUNGU amemfanya kichwa cha familia mnamkosea MUNGU. Hangaikeni na mama peke yake wakati huyo mama anamtegemea huyo baba.
 
Labda wewe ndo uko brainwashed kwani nani hapa cacoment kuwa anamdharau baba?kwani mwanzisha thread kaongelea kumdharau mama au baba?unataka watu wachangie tofauti na thread ilivyoazishwa,hakuna anayemdharau baba na sijaona yeyote aliyecoment kuonyesha anamdharau baba i love both my parents and respect them as well japo mama ana upekee wake.
brain washed creatures. Mnaomdharau baba ambaye mungu amemfanya kichwa cha familia mnamkosea mungu. Hangaikeni na mama peke yake wakati huyo mama anamtegemea huyo baba.
 
Back
Top Bottom