Mama Nanihii darasani! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mama Nanihii darasani!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Sep 25, 2009.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Sep 25, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  KAMA ulizaliwa, ukakua na mpaka sasa hujui kuna mchezo wa kitoto unaoitwa kujipikiliza, basi kimbia harakaharaka kwa Manyaunyau akakunyweshe damu ya nyau, kwa sababu utakuwa umepungukiwa akili kama si mwanga au msukule.

  Hatua hiyo ni muhimu kwa makuzi ya mtoto yeyote yule, ndiyo hatua ambayo mtoto anaanza kutambua umuhimu wa kuwa na baba na mama nyumbani. Mtoto anajua ni nani kichwa ndani ya nyumba, ukiachana na haya mawazo ya Beijing, bila shaka jibu utalipata kuwa ni Adam.

  Ukidhani wewe ni bingwa wa kubisha basi jikumbushe maana ya jina binadamu ndipo utakapoona kuwa hakuna kiumbe anayeitwa binhawa au bineva, kamwe hutakaa usikie kiumbe kinaitwa hivyo. Ukishajua hilo, basi ujue kichwa cha familia ni nani.

  Ubishi wa kiuendawazimu utakufikisha kutaka kutuaminisha kuwa Mungu ni mwanamke huku ukijua kuwa anaitwa Baba uliye mbinguni na si Mama uliye mbinguni.

  Lakini ndiyo sababu Yesu a.k.a Nabii Issa, hajawahi kuonekana amevaa sketi na kukudhihirishia ni nani akafuga ndevu.

  Mazingira yoote haya hujaamini tu kuwa mchezo ule wa kitoto wa kujipikiliza ulilenga kutuelewesha dhana hii? Ili kujiepusha na kunywa damu ya nyau kwa Manyaunyau, ni bora ukakubali yakaisha tukaendelea na topiki nyingine.

  Sawa, wakati tulicheza kujipikiliza akiwapo baba, mama na watoto wao, bila shaka tulijifanya kupika hata panzi tukiwafananisha na samaki, tukapika majani kwa kuyafananisha na mchicha na ndipo walipofikia watoto wenzetu wengine vibaka kuiba nyanya nyumbani, kuchota chumvi na kila aina ya viungo.

  Hiyo ilitokana na imani ile kuwa sisi ni baba na mama na hawa ni wanetu. Tuliiba vijimkaa na kwa kweli wapo walioungua. Mambo mengine ya wakubwa hatukuthubutu, kwanza hatukujua, kwa sababu baba na mama tulizoea kuwaona mama jikoni, baba akisubiri kula tu.

  Na tulivyozidi kukua, wazazi nao walikuwa beneti na sisi, walijua kama tutaendelea kujipikiliza huku tukikua na sauti za vidume zikianza kubadilika na wengine kuanza kuotaota vindevu na vya kike kuanza kuvimbavimba vifua, basi hatari ilitunyemelea.

  Lakini ilikuwa ni kama bahati tu kuwa enzi hizo ni visichana vichache sana vilivyokuwa vinadanganyika. Na vilikuwa havidanganyiki kwa dhati kabisa, achana na hivi vya HakiElimu ambavyo havidanganyiki geresha tu.

  Ni bahati mbaya kuwa hivi vya HakiElimu vimekuja kutuharibia vibinti vyetu, hebu katume dukani umekapa Sh 10,000 kakakununulie gozo la kizungu a.k.a sigara, tena moja ili kakurudishie chenji, hakakuletei kwani mwenye duka akikarudishia kanaruka kimanga “aka thidanganyiki ng’o!” Sasa hii nini kama si uchuro?

  Enzi hizo kama nilivyosema hapo juu, tukaishi maisha ya adabu kweli kweli, vitoto vya kike vikipelekwa unyagoni kabla ya kuolewa na vidume vikipelekwa jandoni.

  Vijike vikiambiwa ukiingia shuleni hakuna mchezo wa mapenzi na vidume halikadhalika.

  Hata walipokuja Wakoloni, msimamo ukabaki ni huohuo mpaka serikalini kuwa mtoto asome amalize la nne au akiendelea mido skuli poa, mpaka amalize la nane na kama atavuka hapo poa mpaka amalize la kumi na mbili na kisha Makerere.

  Ukifika Makerere huko ah ilikuwa sasa mtu umeshakua unajua baya na zuri unajua mbichi na mbivu, hapo sasa hufuatwifuatwi. Hata alipoondoka Mkoloni tukajitawala wenyewe, serikali ikasema yeyote atakayebainika amefanya mbaya na kujaa shule hana, na aliyemjaza atakiona cha mtema kuni.

  Watu wakaogopa kujaa, wakaogopa kujaza hasa pale vidume na midume ilipoambiwa ukimjaza mwanafunzi tu jela miaka saba hakuna cha msalie Mtume. Katika jamii, mibishi haikosekani, mijitu ikaendelea kujaza mianafunzi ambayo nayo ilikuwa limbukeni.

  Serikali ikaifunga tu bila hiyana, lakini haikuacha, ikaendelea kung’ang’ania kama kunguru wa India. Serikali ikafikiria kuwa mijitu ni saratani hii, hivyo turuhusu tu hata wanaojaa uzito wazae na kurudi skuli vitoto mabibi walee.

  Sisi tuliozingatia maisha ya kijadi tukachachamaa tukaja juu kwelikweli iweje sasa vitoto vizae vitoto vyenzao!

  Serikali ikatanguliza ubinadamu, sasa ifanyeje, ana uzito ni adhabu na sasa umtimue shule adhabu nyingine, ajifungue tena kwa kisu ni adhabu!

  Mh hatujakaa sawa juzi Mahiza akamaliza, akasema vielowai vya darasa la saba kama vina uzito visizuiwe kufanya mitihani yao ya kumaliza visubiri seko!

  Vifanye tu, vikifanikiwa kushinda basi viachie mabibi vitegemezi na vyenyewe viende seko visome ili baadaye vilee vitoto vyenzao. Hebu fikiria darasani itakuwaje katika miaka hii ijayo ya ruksa mimba shuleni!

  Jifikirie darasani ambapo sasa mwanafunzi mwenye mtoto atakuwa anaandikisha kwa jina la mtoto wake, mathalan Mama Jose, Mama Juma, Mama Esther, Mama Brian, nakadhalika!

  Uitaji wa majina ya waliopo na wasiopo kwenye rejesta buku ndicho kitakuwa kimbembe:” Mama Jane…anaitika (Nipo); Mama Amina…..(kaenda kunyonyesha); Mama Filipo…..(kaenda kliniki); Mama Silas…..(mwanawe anaumwa); Mama Glory….(Nipo); Mama Theo….(mwanawe katahiriwa), nakadhalika.

  Hapo sasa hata ratiba itabidi zibadilishwe kuwa itakapofika saa nne asubuhi ratiba ioneshe ‘Chai/Nyonyo’, hapo akinamama wanafunzi watakuwa wanaruhusiwa kwenda kunyonyesha vitegemezi vyao kwa nusu saa hivi na urejea darasani.

  Lakini kwa upande mwingine wale walimu wa kuuza kashata na karanga na visheti, watatakiwa kuwa pia na udongo wa Pemba kwa vijanauzito, wale wauza embe mbichi na ndimu nao wasicheze mbali.

  Huku ndiko kunufaishana. Nadhani Wizara imeliona hili la walimu kuwa na biashara mbadala ndani na nje ya darasa ili waache tuisheni. Alamsiki! (JK).

  http://www.habarileo.co.tz/safu/?n=3621
   
 2. Sinkala

  Sinkala JF-Expert Member

  #2
  Sep 26, 2009
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 1,505
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Haa haa haaaa ! Kama ticha anayeita majina ndiye baba wa Filipo, Akilifikia jina la mama Filipo itabidi aite ... 'Mke wangu ....' :D
   
 3. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #3
  Sep 26, 2009
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,578
  Likes Received: 543
  Trophy Points: 280

  aaah aaaah aaah hii kali
   
 4. b

  bnhai JF-Expert Member

  #4
  Sep 26, 2009
  Joined: Jul 12, 2009
  Messages: 2,208
  Likes Received: 1,373
  Trophy Points: 280
  Ukweli hali imefika pabaya saaana. Lakini nini hasa kimetufikisha hapa? Ni utamaduni wa kuiga au utandawazi. Maadili yameondoka katika jamii.
  Tangazo la sidanganyiki nadhani kuanza kwa kulihukumu ni matokeo na wao wanajaribu kuonyesha wapi tumefika sasa. Maana mafunzo si dukani kununua sigara na kuitwa darasani. Kwanini tusizungumzie yanayowakuta hao watoto kabla ya ujauzito na wakitumwa dukani. Tena wengine wanayofanya haya ni wale wa middle school na enzi za kujipikilisha.
  Pia naiona makala kama imejaa lawama bila ya kutoa mbadala. Wanafunzi wamepata mimba, tufanyaje sasa? Tangazo lilivyo, je lingekuwaje?
  Ni suala la jamii nzima, hii kuvizia vitoto ambavyo haviwezi hata kureason na kuvidanganya ni tabia chafu saana. Na haikubaliki. Ni wangapi leo wanavizia wanafunzi wa sekondari? Tunaenda wapi? Wote tuseme inatosha tucontrol programs za TV kwenye familia zetu na tuongee na watoto wetu na wale wanaosimamia sheria waepuke rushwa kukinusuru kizazi chetu.
   
 5. M

  Magezi JF-Expert Member

  #5
  Sep 26, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  kawaida ya watanzania huwa tunarukia kwenye jibu la haraka bila kufikiri. Huyu anayempa mimba mtoto wa primary adhabu yake ni nini?

  Nashauri Wizara husika ipeleke mswada wa sheria ambapo mtu ukimpa mtoto wa umri mdogo mimba au mwanafunzi primary/sekondari hukumu yake iwe ni kifungo cha maisha tuone vitendo hivi vitaendelea?
   
Loading...