Mama nae atimuliwa baada ya binti kutorudi nyumbani


kilimasera

kilimasera

JF-Expert Member
Joined
Dec 2, 2009
Messages
3,073
Likes
24
Points
135
Age
42
kilimasera

kilimasera

JF-Expert Member
Joined Dec 2, 2009
3,073 24 135
BAADA ya binti kutoweka nyumbani na kutopatikana kwa takribani wiki na zaidi nyumbani, baba wa familia {jina kapuni} ameamua kumtimua mke wake akamsake mwanae kwa kudai anajua binti huyo alipokwenda.
Hatua hiyo imekuja baada ya baba huyo kutomuona binti huyo nyumbani hapo na kumuamuru mama huyo anajua binti huyo alipo kwa kuwa yeye alikuwa anamtetea kwa matokeo hayo.

Akiongea na nifahamishe kwa njia ya simu jana, mama huyo alidai kuwa hayupo nyumbani kwake kwa kuwa mume wake alimtaka asirudi nyumbani kwake hapo mpaka ampate binti huyo.

Mama huyo ambaye ni mtumishi wa Serikali alidai kuwa mume wake alidhani kuwa yeye ndiye aliyemfundisha atoroke nyumbani hapo kwa kumuhofia angepigwa na baba yake.

Alidai kuwa mume wake alikuwa na hasira kali sana kuhusiana na majibu ya mtoto wake huyo kwa kuwa alimsomesha kwa gharama za juu na katika shule za binafsi na alimpa kipaumbele kwa kuwa ni binti pekee katika familia hiyo.

Mama huyo alidai kuwa mumewe ni mtumishi katika Wizara nyeti nchini aliomba kutotajwa katika habari hii, alidai kuwa binti huyo alipokimbia ndio amemzidishia hasira ya kumuadhibu kwa kuwa anahisi huenda akawa ametoroka na kwenda kwa wanaume na kudai hicho ndicho kinachomuuma zaidi.

Mama huyo alijaribu kujitetea kwa mumewe huyo na alidai hakumuelewa na kumtaka amsake binti na arudi nae nyumbani hapo.

Mama huyo katika juhudi za kumsaka hapahapa jijini kwa ndugu zake wa karibu hazikuzaa matunda na kudai aliomba ruhusa kazini ya wiki moja kwa kuongopa kuwa anaumwa ili aende kwao Tanga na kwingineko akamuiangalie huko huenda atakuwa amejificha huko.

NIFAHAMISHE ilijaribu kuwasiliana na mama huyo leo asubuhi majira ya saa 4 mama huyo alidai yuko kwenye basi la Raha leo akielekea Tanga kwenye zoezi la kumsaka binti huyo.
 

Forum statistics

Threads 1,251,538
Members 481,766
Posts 29,775,489