Mama na Wanae Wasali Uchi Mbele ya Shule

Herbalist Dr MziziMkavu

Platinum Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
43,105
Reaction score
34,926
[TABLE="width: 491"]
<tbody>[TR="bgcolor: #E1E1E1"]
[TD]

Mama na wanae walipoamua kumwaga radhi shuleni[/TD]
[TD]
Mama mmoja na wanae wa kike na wa kiume wanashikiliwa na polisi nchini Marekani baada ya kusaula nguo zao zote na kuanza kusali mbele ya shule wakiwa uchi wa mnyama.[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="colspan: 3"]Polisi wa kitongoji cha Upper Darby kwenye jimbo la Philadelphia nchini Marekani wanamshikilia mama mmoja na wanae kwa kusali uchi wa mnyama mbele ya shule.

Taarifa ya polisi wa Upper Darby ilisema kuwa mama huyo mwenye umri wa miaka 43 aliyejulikana kwa jina la Sara Butler akiwa na wanae wa kike Joanne mwenye umri wa miaka 23 na Bessie mwenye umri wa miaka 22 pamoja na mtoto wake wa kiume mwenye umri wa miaka 14 walisaula nguo zao zote na kuanza kusali kwenye maegesho ya magari mbele ya shule.

Taarifa zaidi zilisema kuwa awali siku ya tukio, mama huyo na wanae walifika kwenye shule ya sekondari ya Upper Darby High School wakitaka kumuona mmoja wa wanafunzi wa kiume. Walikataliwa kukutana naye kwasababu mama huyo si mzazi wake.

Mama huyo na wanae waliondoka na kurudi baada ya lisaa limoja na kuanza kusaula nguo zao mbele ya maegesho ya magari wakisali kwa kusauti wakimtaja Yesu Kristo.

Ili waonekane vizuri mama huyo na wanae walijaribu kupanda juu ya gari walilokuja nalo lakini polisi walioitwa eneo la tukio waliwahi kuwatia nguvuni mama na wanae.

Mama huyo na wanae wanaozidi umri wa miaka 18 walifunguliwa mashtaka ya kuvunja maadili ya jamii na kujianika uchi hadharani.[/TD]
[/TR]
</tbody>[/TABLE]

Mama na Wanae Wasali Uchi Mbele ya Shule
 
duuuh kumbe yule mti mkavu ana ndugu mpaka marekani, wachawe kweli hawana aibu
 
Huku kwetu kitendo hicho ni kuhatarisha maisha manake wananchi hawachelewi kukuchoma moto kwa shutuma za kuwanga mchana.
 
duuuh kumbe yule mti mkavu ana ndugu mpaka marekani, wachawe kweli hawana aibu
Asante Mkuu Wachawi sio Watu weusi tu kama mnavyofikiria hata watu weupe wapo wachawi tu si unaoan hivyo wanavyo mwaga Razi?
 
idhani kama kuna kusali ya hivyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…