Mama na Mwana wapigania uhuru wa Tanganyika

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,881
30,226
Nyumba ya Mama yake Sheikh Haidar Mwinyimvua, Bi. Mwamtoro Bint Chuma ndiyo iliyobaki na Historia ya Uhuru wa Tanganyika

Angalia picha ya Bi. Mwamtoro bint Chuma mama yake Sheikh Haidar Mwinyimvua akipiga kura Uchaguzi Mkuu 1970.

Bila ya shaka yoyote kura yake ilikwenda kwa Julius Kambarage Nyerere na chama chao cha TANU.

Bibi huyu aliishi zaidi ya miaka 100 na alifariki tarehe 11 May 1981.

Nyumba yake ilikuwa Mtaa wa Kariakoo na New Street No. 69 nyuma ya ofisi ya TAA miaka ya 1930 na TANU katika miaka ya 1950.

Hii nyumba bado ipo katika mikono ya familia ya Mzee Haidar Mwinyimvua na sasa iko nyuma ya Ofisi Ndogo ya CCM.

Nyuma ya nyumba hii kwa upande wa Mtaa wa Udoe Mzee Haidar Mwinyimvua mtoto wa Bi. Mwamtoro alikuwa na nyumba yake mwenyewe ambayo ikitumiwa zaidi kama mlango wa kutokea wanawake waliohudhuria mikutano ya TANU ya ndani kwenye nyumba hiyo ya mama yake, Bi. Mwamtoro bint Chuma iliyopakana na ofisi ya TANU.

Siku zile ua wa makuti ndiyo uliokuwa unatenganisha ofisi ya TANU na nyumba ya Bi. Mwamtoro.

Siku ya mkutano wa ndani wa TANU haya makuti yakiondolewa hivyo kuunganisha nyua hizi mbili kuwa ua mmoja.

Wanawake wakikaa nyuma na wanaume wakiwa mbele katika ua wa nyumba ya TANU New Street sasa Lumumba Avenue na akina mama wao wakiwa uani kwa Bi. Mwamtoro.

Huo ndiyo ulikuwa uwanja wao akina Bi. Titi Mohamed, Bi. Hawa bint Maftah, Bi. Tatu bint Mzee, Bi. Chiku bint Said Kisusa kwa kuwataja wachache.

Wakimaliza mkutano wanawake walikuwa wanaingia kwenye nyumba ya Haidar Mwinyimvua ambayo mlango wake uko Mtaa wa Udoe kuondoka kuepuka kupishana na wanaume.

Wakati wa uhai wake marehemu Rashid Mfaume Kawawa aliwaambia ndugu zake Sheikh Haidar Mwinyimvua kuwa nyumba yao hii imebeba kumbukumbu nyingi ya harakati za kupigania uhuru wa Tanganyika na endapo watataka kuiuza basi wakifikirie chama kwanza kabla ya mnunuzi mwingine.

Picha kushoto ni Bi. Mwamtoro bint Chuma na mwanae Haidar Mwinyimvua wote wapigania uhuru wa Tanganyika.

Picha ya tatu ni nyumba yenyewe kama inavyoonekana hivi sasa.

Screenshot_20211112-063934_Facebook.jpg
 
Waiuze tu kwa ccm sasa hilo gofu mjini kati linachafua mazingira
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom