Hi wapendwa wangu! Jamani nisaidieni mwanaume kuzaa nje ya ndoa halafu anaomba radhi kwa mke wake na mke anamsamehe kwa moyo mweupe na kumweleza amlete mtoto nyumbani wamlee pamoja. Baada ya mke kuuliza kama alishawaeleza ndugu zake mume alikataa katakata na akaleta mtoto wakisubiri siku wawaite ndugu wa mume waelezwe. Baada ya muda mke aligundua mama mkwe anajua na huyo mjukuu anamjua mke alihuzunika sana lakini mama mkwe aliona mke hastaili kuchukizwa na jambo hilo. Jamani kosa la mke huyu ni nini hapa?