Mama mkwe wangu akianza kupiga watoto haachi hadi awaume na damu zitoke

Nazjaz

JF-Expert Member
Jan 20, 2011
7,684
8,833
Nimekuja ukweni kuwaleta watoto baada ya kufunga shule Ijumaa ya juzi, waje kwa Bibi yao, Babu yao alishatangulia mbele ya haki.

Hapa mama mkwe anaishi na watoto wake wawili wa kike ambao nao Wana watoto, hivyo basi mama mkwe anaishi na wajukuu zake pia.

Kuna kitu kiko very weird nimekiona. Mama mkwe ni mkali sana, ana hasira sana, akianza kupiga, hasira hazimuishi mpaka amuume na amtoe damu huyo anayempiga ndipo hutulia.

Jana nilipofika, mtoto wa nyumba jirani alikuja kuchota maji hapa, akaondoka akaacha maji yanatiririka bombani, mama mkwe akafoka sana kwa hasira na ukali wa juu.

Akaenda kwenye nyumba jirani akakavuta hako katoto, kakapiga sana kisha akakauma Sana mpaka damu zikamtoka, hakika kamjeruhi mtoto was watu. Wenye mtoto wamepeka malalamiko serikali ya mtaa kesho kaitwa ofisini akajieleze.

Leo mjukuu wake wa form 2 ambaye ni mtoto wa wifi yangu kasahau biblia Kanisani kwa bahati mbaya, kapigwa Sana, Kisha akamuuma begani, kamuachia kidonda kikubwa Sana.

Nilikuwa nimepanga tukae Hadi X mas, lakini kwa haya ninayoyaona, asije pandikiza hayo maroho kwa wanangu, kesho naanza maandalizi ya kurudi.

Je hivi hili nyie wenzangu mnalionaje?
 
IMG-20191201-WA0001.jpg
 
Ana roho mbaya ya jini makata huyo. Huwa halitulii bila kuonja damu. Sio kwamba nakutishia. Sasa dawa ni weye kuondoka na vitoto vyako kwa kuwa tiyari umeshaonywa kumhusu huyo jinamizi.
Ondoka taratiibu kuwa umeitwa kazini au uliyemwachia chumba anaondoka ghafla kwa matatizo yaliyotokea kwao. Hivyo hatahisi umemng,amua kiu yake ya damu.
Pole sana kuolewa kwa wanywa damu za watu. Vipi macho yake; Mekundu mekundu hivi?? Hiyo nayo dalili ya uzimwi zimwi hivi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom