Mama makinda amesahau...!!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mama makinda amesahau...!!!!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Shagiguku, Dec 15, 2011.

 1. Shagiguku

  Shagiguku JF-Expert Member

  #1
  Dec 15, 2011
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 400
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 45
  Mama Annah Makinda yawezekana amesahau kule alikotoka kutokana na kile kinachoonekana kukitetea na kukiamini, mama yangu huyu ninaye muheshimu kwa sana tu amesahau kuwa hoja aliyoitumia katika kujaribu kuharalisha na kupitisha posho za wabunge ni ya kizembe na ya kitoto kabisa na hata watoto wakiambiwa hoja hiyo wataikataa sana tu.

  mama yangu huyu leo hii amesahau kuwa, kupanda kwa maisha hakuko dodoma tu bali ni nchi nzima na duniani kote (kwa sisi tunaotoka nje ya nchi mara kwa mara tunalifahamu hili),

  mama yangu huyu leo hii amesahau kuwa, hakuna soko maalum la wabunge la kununulia bidhaa zao wao na familia zao bali watu wote tunaingia katika soko moja la kununulia bidhaa iwe hapo dodoma ama hapa mwanza, iweje lewo uwepo ubaguzi wa kuwabagua watanzania kwa kuwaongezea posho baadhi ya watanzania na kuwaacha walio wengi wakipiga miayo kwa wimbo wa maisha magumu dodoma...??

  mama yangu huyu leo hii amesahau kuwa, hata akiacha kuwafikiria basi watanzania wengine wote katika nchi hii, basi ajaribu kuwafikiria watanzania waliopo hapo dodoma tu (kwa kuwa maisha yamepanda dodoma) kwa kuwapatia nao hiyo posho mpya ya "maisha magumu dodoma" na hapa nazungumuzia: walimu, wauguzi, madaktari, makatibu muhtasi, mapolisi, magereza, wakulima, wasukuma mikokoteni, wauza nyanya, mama lishe, ma-hausi gero, ma-baa medi, wanafunzi nk, nk, nk, nk,nk....!!!! (orodha ni ndefu waweza kuongezeapo na wewe msomaji....!!)

  mama yangu huyu leo hii anasahau kuwa, walimu bado wanaidai serikali hii hii ya bunge hili hili analoliongoza ma-milioni ya fedha kama siyo mabilioni, hapo sijasemea mapolisi, madaktari, wahasibu, magereza, wafanyabiashara, nk, nk, wanaidai kiasi gani serikali hii, maana kama ni madeni basi serikali inaongoza kwa kudaiwa na watumishi wake.

  mama yangu huyu leo hii, anapata wapi nguvu za kusimama mbele ya watanzania wote na wananchi wa jimbo lake waliompigia kura ili awatetee kwa kuaamua kukitetea kikundi kidogo tu cha watu (wabunge) wasiozidi hata mia nne katika nchi yenye watu zaidi ya milioni 40....!!!???
  ukiacha hao wabunge wake anawatazama vp watumishi wengine wa ofisi ya bunge wasio wabunge (ambao naamini kuwa posho hizi haziwahusu maana siyo wabunge) pale watakapokuwa wakiwasainisha wabunge hiyo nyongeza ya "posho ya maisha magumu dodoma...!!!???"

  mama yangu huyu leo hii amesahau kuwa, serikali hii hii ilikataa kuongeza kima cha chini cha watumishi wake ili kiwe 350,000/= kwa madai kuwa haina fedha...?? sasa hizo za kuwaongezea posho wabunge (hapa naamini atanijibu kuwa "aah wabunge si ni wachache tu ukilinganisha kwa mfano na walimu..?" zimetoka wapi...???

  jamani jamani jamani jamani, mama yangu huyu amesahau, amesahau, amesahau, amesahau, amesahau, amesahau, amesahau.

  kwa kweli amesahau mambo mengi sana, amesahau kuwa hata kama atawaongezea mapesa mengi kiasi gani hakuna hata siku moja yatatosha kukabiliana na "maisha magumu ya dodoma" kwa nini asiwe na mawazo sasa ya kufikiria kuzifuta posho zote za wabunge na kuushusha mshahara wa wabunge (hapo pa gumu) ili kutimiza maneno ya katiba "binadamu wote ni sawa"...???

  ntalia mimi.......!!!!


  :A S thumbs_up: :couch2: :couch2::A S thumbs_up: :poa
   
 2. KakaKiiza

  KakaKiiza JF-Expert Member

  #2
  Dec 15, 2011
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 10,543
  Likes Received: 2,248
  Trophy Points: 280
  Umekosa watu wakuwaheshimu na wewe!!!Dikiteta wa siasa wewe unamchukulia value!full crap!
   
 3. Linyakalumbi

  Linyakalumbi JF-Expert Member

  #3
  Dec 15, 2011
  Joined: Jul 28, 2011
  Messages: 259
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Anatokea maeneo ya Uwemba pale Njombe,Kaangalie wakazi wa pale wanavyoishi kutegemea Viazi visivyo na soko na ni masikini wanaoishi kwa buku na kanga za magamba wakati wa kampeni!!!!Rahisi kununulika balaa ndicho anachojivunia huyu Bi Kiroboto
   
 4. C

  CHUAKACHARA JF-Expert Member

  #4
  Dec 15, 2011
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 12,210
  Likes Received: 3,819
  Trophy Points: 280
  Mwenye shibe hamjui mwenye njaa
   
 5. d

  dada jane JF-Expert Member

  #5
  Dec 15, 2011
  Joined: Dec 8, 2011
  Messages: 566
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hivi hao wabunge na spika wao wasipigwe ban ya kutokuwa wabunge maishani maana kufuru walioifanya haitofautiani na wanafunzi wale wa UDSM.
   
 6. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #6
  Dec 15, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,317
  Likes Received: 438
  Trophy Points: 180
  tuwaundie Regulatory authority..wakijiamulia upuuzi tunafinya!
   
 7. Jakubumba

  Jakubumba JF-Expert Member

  #7
  Dec 15, 2011
  Joined: Mar 5, 2011
  Messages: 1,627
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Kudadadeki makinda
   
 8. shizukan

  shizukan JF-Expert Member

  #8
  Dec 15, 2011
  Joined: Jan 16, 2011
  Messages: 1,158
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Mama anadhihirisha jinsi alivyostahili kupewa ile nishani na Mh. Dokta.

  Mimi nifikiri hawa wabunge na mama yao wangeingia mtaani hapo Dodoma kuomba ushauri kwa Walimu, Polisi, Wauguzi na watumishi wengine wa serikali juu ya namna ya kupanga bajeti. Kama mbunge anashindwa kubajet 70,000 kwa siku basi waombe ujuzi kwa hawa wenzetu wawaeleze wanawezaje kuishi kwa 149,461 kwa mwezi.

  Hii ndio shida ya kupeana madaraka kwa kujuana, huyo ndio SPIKA WA BUNGE.

  Na hii ndio namna wanawake wanavyowatetea wanawake wenzao waliopo vijijini.

  Na hiki ndio chama chetu ambacho kura kinapata huko huko vijijini kwa kuwa huku mjini tumeshtuka.

  Kwa kweli madudu ya serikali yamekithiri mpk Wakili wa CCM Faiza Foxy kaingia mitini
  .
   
Loading...