Mama Magreth Sitta kukuunga mkono ni lazima?

Mama Magreth Sitta kukuunga mkono ni lazima?

MPAMBWE

Senior Member
Joined
Apr 4, 2015
Posts
137
Reaction score
29
Kwa kweli niajabu sn kwa mwanasiasa mkongwe kama Magreth Sitta kufanya siasa za kinyesi kwa kiasi hiki yaani huyu mama badala ya kushawishi watu wa muunge mkono amekuwa anatumia nguvu nyingi kuwa kawanyanyasa watu wote wasio muunga mkono mfano mdogo hapa Urambo kuna saluni moja vijana wanaofanya kazi kwenye ile saluni wanajitambua hawamuungi mkono kbs yeye na chama chake kwa kutumia uwezo wake ameamuru saluni ile ifungwe yeye akiwa anaamini ndio njia sahihi ya kuwabadilisha vijana wale, naomba mnisaidie na kwingine hali ilivyo nikama huku kwetu?
 
Hayo ni maelezo yako,tunaomba tupate na maelezo ya upande wa pili ndio tutoe hukumu.
 
yeye aliamuru ifungwe kama nani?nijuavyo saluni ni biashara na kuifunga ni lazima taratibu zifuatwe km ilivyokua wakati inafunguliwa.
 
Anafungaje saloon huyo kijana kwa maagizo ya magreth? huyu magreth ni nani hapo urambo zaidi ya kuwa mgombea ubunge? Kama leseni anayo na hana tatizo na manispaa sijaona sababu ya hao vijana kufunga hiyo saloon, wakiambiwa waondoke urambo wataondoka pi? Acheni ujinga#hakuna dhambi mbaya kama uoga.
 
Back
Top Bottom