falcon mombasa
JF-Expert Member
- Mar 5, 2015
- 9,186
- 9,291
Ni jambo la kushangaza ama kuvunja nguvu mno watanzania wanaposhuhudia baadhi ya viongozi wakitumbuliwa haraka sana kwa tuhuma za kutokuwa makini kazini tena bila hata kujitetea.
Ila inastajaabisha zaidi serikali hiyo hiyo ya rais huyo huyo wa chama hiko hiko anamuacha mkuu wa mkoa wa dar es salaam mwenye kashfa kubwa zaidi ya kukosa sifa za kielimu lakini bado yupo ofisini tena akiwa na majibu ya kishujaa kabisa dhidi ya tuhuma hizo.
Huu si wakati wa kuburuzwa ni muda sahihi serikali kueleza sababu za msingi za kuendelea kumbakisha huyu mwenye kashfa madarakani.
Ni jambo la fedheha mno kuona taasisi kubwa kama ikulu kujibu tuhuma ambazo si za kweli kwakuita vyombo vya habari na kukana taarifa fulani za uzushi kuwa si kweli, lakin inashangaza zaidi kuona huyu mwenye kashfa kubwa zaidi ya kudhalilisha serikali nchi na aliyemteua bado anadunda ofisini kama vile hakuna mwingine mwenye sifa kuwa mkuu wa mkoa Dar es salaam
Mitaani maneno yameanza kuibuka kuwa huenda yupo kwa ajili ya kumnufaisha aliyemteua, wengine wakihoji huenda sababu wote wametoka kanda moja. lakini kama suala ni kuchagua wa kanda moja mbona wako wengi wenye sifa.
Kwakweli ni wakati maalum kwa chama kujitathmin kama 2020 kinapaswa kuendelea kung'ang'ania nafasi hiyo ya urais
My take:
Tanzania ni ya watanzania wote sio ya mtu fulani au kabila fulani