Cherenganya
JF-Expert Member
- Jan 21, 2018
- 2,309
- 1,787
Habari za leo waungwana?
Sala na salam zangu ziwashukie kina mama wote duniani, wenye kujua hasa maana ya nomino yenyewe MAMA na wenye kuitendea haki nomino hiyo kama ambavyo chapisho hili limekusudia kufanya. Mama; je ni cheo, jina, heshima au vyote. kwa muhtasari tu ningependa kuanza kuchanganua labda neno mojamoja kabla ya mjumuisho wa bandiko langu.
CHEO: Hili ni daraja la mtu katika kazi, wale ambao wanamjua mama watakubaliana nami kuwa mama ni kazi haswa, hasa pale unapokua na mtoto kati ya umri wa 0-3 ambapo tafriri ya kila kitu ni kubashiri zaidi juu ya aina ya kilio atoacho; mfano mtoto analia hawezi sema analia nini na mfano wa hivyo.
JINA: Utambulisho wa mtu, kitu au mahali.
HESHIMA: Thamani ya utu, utukufu au daraja (mlinganyo) mara nyingi katika binadamu.
KISA:
Bwana mmoja aliyefanikiwa kwenda ughaibuni na kuwa anamtumia fedha mama yake kwa minajili ya matumizi pamoja na maendeleo, moja kati ya maendeleo lengwa ilikua ni Bwana huyo kujengewa nyumba ili atakapo maliza kipindi chake cha kukaa ughaibuni anakuja kuingia kwenye nyumba yake.
Alipo kuwa Ughaibuni Mama yake alikua akimtumia picha za jengo na kumuaminisha kuwa nyumba yake inaendelea vizuri na ilifikia kipindi aliulizwa hata angependa marumaru za nchi gani na milango awekewe ya aluminiam au ya mbao aidha hata aina ya rangi ambayo angependelea.
Miaka kadhaaa baada ya mkataba wake kwisha, alirejea nyumbani kwa kile alichokipanga kuwa ni (surprise) kwa mama yake na ndugu zake, alipigwa na butwaaa kukuta hakuna nyumba wala kiwanja achilia mbali fedha alizokua akituma.
MAMA; JE NI CHEO, JINA, HESHIMA AU VYOTE?
KISA;
Bwana mmoja aliyeibukia kumpenda sana mama yake kiasi cha kutosikia la MUADHINI WALA LA MNADI SWALA, alikuja kugundua kwamba mama yake ni kinara wa ushirikiana (uchawi) pale mtaani kwao na hili lilithibitika baada ya kamati ya kichawi ya mama yake kuingia "choo cha kike" baada ya kukwiba kitovu cha kichanga cha bwana mmoja mwenyeji wa Kigoma ambaye naye alikua yuko vizuri katika sekta hiyo, na kuamua kuwaanika wale wote walio shiriki kwa namna moja au nyingine katika tukio hilo. Mama huyo alikiri kwa kinywa chake na kutaja nafasi yake chamani (mwekahazina wa miguu, vichwa, mikono, vitovu na majina ya roho za watu ambao waliwaondoa hapo mtaani).

Mama mmoja aliyekimbiwa na Mumewe ((kwa madai kwamba mama yule ni wale wanawake ambao uswahilini kwetu wanawaita MLANGO WA NANE) (wanawake wa mlango wa nane inasemekana ukimuoa huyu mali zako zote zinaporomoka, na usipojipanga hata kazi unafukuzwa, unagombana na ndugu na mambo mengi ya mikosi na mabalaa yasiyokwisha) akaachiwa watoto, ili hali hakuwa na kipato cha aina yoyote na kujitahidi mpaka watoto wake kufanikiwa kumaliza elimu, na kubadilisha maisha ya mama yao na mazingira ya pale nyumbani.

Ahsanteni...