Mama hamtaki Mpenzi wangu

Usithubutu kumuamini. Watu wasanii kwenye kutaka kufanikisha mambo yao. Usimlie yamini mlevi anayesema anafanyia kazi ulevi wake kwa ajili yako.
ni kweli ila sio kwamba ndio nmeingia kichwa kichwa tatizo nataka kuenjoy moment(when there is peace in the jungle, you gotta enjoy the quiet )
itakapoishia basi hamna neno tukishindwana ila hata hilo linashindikana kwa maneno ya bi mkubwa
 
Na hivyo vitu sio kivile, pombe ameacha tangu nimwambie mi pia staki hivyo vitu akishindwa kuacha tutakua tu casual amenielewa anayafanyia kazi hayo

ukimuuliza anasema umemtukana
sio kivile ndio jibu gani sasa? kwenye nyeusi weka nyeusi si habari ya kijivu,kama anakimbiza mwenge na kunjwa pombe msikilize mama.
 
Miezi mitatu michache sana...Kaa naye hata mwaka huweza utagundua dosari anazoeleza mama yako..
.halafu unataka kuolewa sababu nawe hujasoma na huna kazi? Hakuna kingine kinachowaunganisha zaidi ya hicho? Unamkubali sababu wapenzi wengine walikusumbua? Huna sababu nyingine? Nadhani mama ana point msikilize fanya uchunguzi.
 
Ndo nilitakaa niseme mie amuulize huyo mama ake, yeye kuwa na baba ake alichaguliwa au kwa ridhaa yake, wala hakuna heshima kuvunjwa anapaswa kumuuliza.
 
-ana vuta bangi/pombe
Asiefunzwa na mamaye hufunzwa na Ulimwengu, aliemtanguliza kukuonyesha jua anakwambia achana na hii takataka umeng'ang'ania wembe ukishakukata unarudi tena kwa mama unakua ushajikata na wembe, mwanakulitafuta mwanakulipata endelea na huyo Kiranga komo yakikukuta usiseme hukuambiwa
Sasa hapo nifanyaje wakuu?
Msikilize mama yako ukiumwa maututi yeye ndie atakaekua anakupikia uji nyumbani na kukuletea hospitalinu sio hilo kulumbembe kashalistukia liweke pembeni wamama wanaona mbali usimdharau mama yako ipo siku utajuta utasema mama aliniambia Mimi Juu nimesema umsikilize Mama Ila nilipofika hapa naomba umshirikishe mtu mwingine Shangazi, Mama mdogo au Mkubwa km wapo emu jaribu kuwashirikisha Jambo lako na wao waone je kweli mama yupo sahihi au kuna Jambo nyuma ya pazia ukiona na wao wanasema achana na huyu mtu aseee usibakize mda, watu wana macho na macho ya watu wanaona, haya mfikishe nilipokueleza nenda kwa Shangazi mwambie Shangazi nimemleta mwenzangu km utani tu ampigishe story amfahamu kidogo km kumpigisha interview ndogo kumjua na kumdadisi akitoka mpeleke kwa Mama mdogo au Mkubwa nae ampige interview ndogo amjue amdadisi kidogo, alafu wao wawili watacompare convo zao je anakufaa ikisoma NO hakufai asee usilazimishe utakutana na balaa la dunia huko mbele watu wana macho na macho hua yanaona mbali Wote kwa pamoja hili suala inabidi mshirikishe na watu wengine ndugu na jamàa ili mpate muafaka kua kweli jamaa anakufaa ama hakufai wao wataona km anakufaa au anapretend kwa muda mbele atakugeuka watamshtukia mapema tu unajua mapenzi na moyo wa mtu ni kichaka
 
Kama ku enjoy wewe enjoy tu maisha yenyewe nsio haya haya
Ndo mama hataki
sasa nashindwa nifanyeje kuna mda nawaza au nipotee tu out of the blue
wasinione tena kwa miaka kadhaa nikaoumzishe kichwa mahala
maana stress za maisha ukichanganya na haya mambo naona naelemewa na hakuna wa kujali
 
mimi nataka kwanza mahusiano wala sina haraka ya ndoa, ni mama tu anapeleka mambo mbele
pia kinachofanya nimpende, ni upendo yeye amenipenda nimerudisha upendo na hio ni sheria yangu tangu zamani... amenionyesha upendo kipindi ambacho nimeuhitaji sana
 
Wapo wavuta bangi na wanywa pombe si malaya. Umalaya ni hulka, wala haichochewi na vitu tajwa.

Swala la kuwafundisha watoto, wapo walimu watamsaidia. Tupo ambao wazazi wetu hawajui hata 'a' wala 'be' lakini walitusimamia kisawasawa.

Si vema sana kumkatalia mwanao kuolewa kwa sababu tajwa hapo juu. Kama kaacha bangi na pombe, basi yupo vizuri. Maisha ya kawaida si hitimisho. Watapambana watajenga yao.
 

ariana

Pole kwa hili, kinyamwezi wanaita dilemma.

Hata hivyo, ingawa vitabu vinasema waheshimu Baba na Mama, msisitizo ni kuwaheshimu kwenye kutenda righteousness (yanayompendeza Mungu).

Sasa basi, uchaguzi wako ni ima kuacha na kijana uambatane na Mama ama uachane na Mama kisha uambatane na kijana.

Mbili, kumbuka maisha ni kubahatisha maana hakuna aijuaye kesho.

Ushauri wangu, as long as mnapendana na kijana, nyie songeni mbele. Yakiwashinda mtaanza upya. Mapenzi hayalazimishwi wala mtu hachaguliwi wa kuambatana naye. Bible inasema mali na Fedha zinatoka kwa wazazi, mke/mume mwema ni biashara za Mungu hizo.

Kila la heri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…