Mama hamtaki mchumba wangu

Wamama wengi Wa kichaga hawapendi wakwe zao asilimia kubwa.( wapora)
 
Vijana wengine upenda kusingizia mama hakutaki kumbe yeye mwenyewe kasha badili mawazo.Kama uko serious na penzi ulilonalo sizani km mama anaweza kuwa tatizo,unatakiwa umwambie ukweli na ajue msimamo wako atakuacha na mpenzi wako ila wewe mwenyewe kama unaonekana mguu nje mguu ndani lazima atakyumbisha tu. Kuwa na mpenzi wa kupanga nae maisha ya baadae sio kitu kibaya na wazazi wanakibariki sana labda km wewe hujitambui au kuna jambo hujaliweka wazi hapa.mwanaume wa kweli anajisimamia sio mama mama,simama na usimamie msimamo wako kwa faida yako na mpenzi wako.
 
Kama utakuwa na ujasiri wa kumuacha ni vema kwa sababu mbili kuu. 1. Mama yako tayari hamtaki huyo mkwe na hatopata amani kuja kwako au hata wajuu wake hatowapenda. 2. Ulifanya kosa kubwa kuruhusu mchumba wako akajua kuwa mama mkwe hampendi. Kwa kawaida wanawake wakiolewa huwa wamejiandaa kufanya mapambano na mama mkwe na mawifi na huo huwa ni mzozo pozo ambao huibuka anytime ukipata activator. Sasa kama wanajiandaa kupambana hata bila tatizo itakuwaje ikiwa ameshajua mama kajiandaa kupambana?. Unaweza kuoa na ukaishi nae ila ujue mama yako hatakuwa na amani kwako. Wazazi wanamacho ya rohoni na tambua wanawake wanajuana sana na kwakuwa mama yako hayuko inlove na huyo mdada basi yeye huyaona mapungufu mengi usiyo yaona kwani sasa wewe ni kipofu kwa penzi la huyo Salome wako.

Usikubali goli kama Tambwe utaharibu samani za nyumba yako.
 
TULIA KWANZA!!Maana Umepanic..Kama Mama Kagoma Hamna Uhusiano Hapo Mkuu,Kunywa Maji anza Kusaka Upya Bottom Line!!!
You think so? Kwanini sasa?

Akimkataa na huyo mwingine? Wamama wengine hawana sababu, wanakataa tu. Kama hana sababu wala usimsikilize na hautapata cha laana wala shida yoyote
 
HAYA MASWALI KWELI NI YA MSINGI UKIYAJIBU MAJIBU YATAPATIKANA KWA URAISI Na pia kabila lako na la msichana ni lipi?

Ila kiufupi, usikate tamaa endelea kumuelewesha mama, chakushukuru hana sabab, kwahiyo usichoke tumia hata viongozi wa kanisa analoswali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…