Mama Gaudensia D. Kabaka Achaguliwa Mwenyekiti Umoja Wa Wanawake Tanzania ( UWT) Taifa

KADA08

Member
Dec 2, 2017
44
152
Hatimaye wajumbe wa mkutano mkuu wa Jumuiya ya wanawake wamemchagua Dkt Gaudensia Kabaka kuwa mwenyekiti wa jumuiya hiyo ngazi ya Taifa kwa kipindi cha miaka 5.

Kwa nafasi yake atakuwa mjumbe wa kamati kuu, halmashauri kuu na mkutano mkuu wa CCM Taifa. Kwa mujibu wa kanuni za Jumuiya hii katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 Dkt Kabaka atakuwa mbunge wa viti maalum moja kwa moja.
 
Jana Mzee alisema,anataka UWT mpya,anataka UWT kama ile ya kina Sofia Kawawa.Mzee akasema UWT ya sasa ni hovyo sana,ilikuwa ukitaka kuwa Rais wa nchi hii lazima "umkamate" mwenyekiti wa UWT ili uungwe mkono na akina Mama wa CCM.

Anasema ilifikia mahali mwenyekiti wa UWT anakuwa mali ya mgombea Urais na akihama basi anahama nae kifikra na kimatendo,ila kimwili anabaki CCM.Sasa Mzee anasema anataka mwenyekigoda wa UWT awe tofauti na yule aliyehama na mgombea aliyeshindwa kura za maoni 2015.

Mama Kabaka ndio chaguo lake kwa kina Mama,na kwa vijana chaguo lake ni yule mpwa wake.Lazima mzee apange safu yake kuelekea 2020.Yaliyompata wakati wa kampeni 2015 yanamuumiza sana na jinamizi lake bado linamuandama.Maana 2015, si UWT wala UVCCM wenyeviti wake wote walikuwa "Team Kishindo Kikuu toka Monduli".

Baada ya uchaguzi huu,masalia ya "Monduli" yote yatakuwa kwenye kapu la "wasiotakiwa".Na Mzee haamini sana watu toka upende mwingine zaidi ya mwambao mwa Nyanza Province
 
Safi sana.. Ndio CCM inayobadilika na kuangalia uwezo wa mtu na si kigezo cha anatoka wapi.. Huyu mama namkubali sana ni jembe kweli kweli na ili jembe liweze kufanya kazi hasa lile la mkono ni lazima liwe na mpini.. Tusubiri tuone huo mpini
 
Wadau
Safu ya uongozi ndani ya Umoja Wa Wanawake Tanzania ( UWT Taifa) imekamilika.
Kada mkongwe Mama Gaudentia Mugosi Kabaka amechaguliwa kwa kishindo kuongoza Umoja huo.

Mama Kabaka amewahi kuhudumu kama Waziri Wizara ya Kazi na Ajira, Naibu Waziri Sayansi, Teknolojia na Elimu ya Juu na iliyokuwa Wizara ya Elimu na pia kuhudumu kama Mbunge viti maalumu.

Hongera sana UWT kwa kuendesha uchaguzi wa kidemokrasia.
 
Hongera kwao wakina mama leo wameonyesha UMAMA hasa sio USICHANA

Nikiumbuka kikao kilichopita walishindwa kumchagua mwenyekiti kisa alikuwa na skendo za kuiba waume za watu. Leo nimefurahi aisehh hawajaniangusha. Sasa wafanye kazi sio kuleteana fitna mara huyu hajaolewa, mara mdangaji mara nini. Fanyeni kazi sasa

[HASHTAG]#HAPAKAZISASA[/HASHTAG]
 
Jana Mzee alisema,anataka UWT mpya,anataka UWT kama ile ya kina Sofia Kawawa.Mzee akasema UWT ya sasa ni hovyo sana,ilikuwa ukitaka kuwa Rais wa nchi hii lazima "umkamate" mwenyekiti wa UWT ili uungwe mkono na akina Mama wa CCM.

Anasema ilifikia mahali mwenyekiti wa UWT anakuwa mali ya mgombea Urais na akihama basi anahama nae kifikra na kimatendo,ila kimwili anabaki CCM.Sasa Mzee anasema anataka mwenyekigoda wa UWT awe tofauti na yule aliyehama na mgombea aliyeshindwa kura za maoni 2015.

Mama Kabaka ndio chaguo lake kwa kina Mama,na kwa vijana chaguo lake ni yule mpwa wake.Lazima mzee apange safu yake kuelekea 2020.Yaliyompata wakati wa kampeni 2015 yanamuumiza sana na jinamizi lake bado linamuandama.Maana 2015, si UWT wala UVCCM wenyeviti wake wote walikuwa "Team Kishindo Kikuu toka Monduli".

Baada ya uchaguzi huu,masalia ya "Monduli" yote yatakuwa kwenye kapu la "wasiotakiwa".Na Mzee haamini sana watu toka upende mwingine zaidi ya mwambao mwa Nyanza Province
Ni wawajibikaji na " Waaminifu"!
 
Hatimaye wajumbe wa mkutano mkuu wa Jumuiya ya wanawake wamemchagua Dkt Gaudentia Kabaka kuwa mwenyekiti wa jumuiya hiyo ngazi ya Taifa kwa kipindi cha miaka 5.

Kwa nafasi yake atakuwa mjumbe wa kamati kuu, halmashauri kuu na mkutano mkuu wa CCM Taifa. Kwa mujibu wa kanuni za Jumuiya hii katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 Dkt Kabaka atakuwa mbunge wa viti maalum moja kwa moja.
KADA08 roho ina kuumaje? kufuatia ushindi wa Mama Kabaka
 
Ubunge wa viti maalum + uwaziri.
Kama aliyetolewa bado anapigania kuwezeshwa. Ugonjwa wa viti maalum
 
Back
Top Bottom